Sitaacha kulishujudia jina la Yesu. Kuandika sitamaliza, ila kisa kimoja tu labda kiwakilishe. Mwaka 2021 nilifunga siku 21 nikiwa na mambo tata sana katika maisha yangu, nikaliita jina la Yesu katika hizo siku zote, nilikuwa na maombi yangu 9, nilijibiwa 8, mbili kati yake zolihitaji financial resources, nilipata kwa muujiza sana mpaka mtaani wananiita usalama wa taifa maana kazi haihusiani na na kuiba cha mtu, within few months mambo yalibadilika sana, haukuisha mwaka kujibiwa, it was instantaneous, mengine yalishashindikana kwa muda wa miaka 9 yakafanikiwa within months. Suala moja lilishindikana ambalo najua kulikuwa na weakness ndani yake, nilihitaji Mungu aniondoe katika hali fulani, ndani yake kuna matendo yasiyompendeza Mungu ambayo kila mtu mzima anafanya anyways, most of us, nilifanya hayo maombi nikiwa sijadhamiria kuachana nayo mimi kama mimi ila nilitarajia Mungu afanye muujiza, imeshindikana hadi leo. Lakini prayers zote zilizokuwa 100% clean zilitiki mpaka nikaogopa, naogopa mpaka leo to be honest, ni financial na mostly personal issues. In addition, nina matukio mengi sana ikiwemo healing prayers, mfano, mama yangu alikuwa ameshikwa na matatizo fulani ya ngozi few years back, siku nimeenda kuwaona nikanotice how bad she was hata kuliko alivyokuwq anaelezea kwa simu, nilipoona nikajisikia huzuni sana, nikaingia ndani nililia kimya kimya, usiku kucha nawaza why and how, nikamwambia Mungu heal her ikikupendeza, the next day she was like 60% better, bila intervention ya ziada, mpaka naondoka akawa ameshapona, sikumwambia ila nilijua this cannot just be by chance. Huyu Yesu mwacheni tu, anasema mkiniita kwa nia nitawajibu kwa lolote mliombalo, He does, always, ni udhaifu wetu tu wa imani unatukosesha kunufaika naye ila kama ni miujiza ya mkate unaweza kufanya sana kupitia Yeye. Usilinganishe Yesu na vitu vya ajabu, yeye Mungu katikati yetu, wala hatofautishwi ukuu na Baba, maana wao ni kitu kimoja! Mungu mmoja katika Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mtafuteni tu kwa dhati anajibu, wala humhitaji Mwamposa, padre au mchungaji, you can do it mwenyewe.