Katika hali ya kustaajabisha mwanzoni mwa mwaka 2012, nyumbani kwetu tuliingia vita ya kiroho kati yetu sisi na jirani aliye kua mganga wa kienyeji (R.I.P)
Yule mganga ilifika kipindi akamtupia pepo la uchizi dada angu awali katika kustaajabu hali kama ile tulianza kwenda hospital kujua hali yake ki afya kama amepatwa na maralia kali au kuna kingine, tulimkuta ana maralia ringi 15 akatumia sindano ya dozi lakini hakutengemaa.
Tuliona ile vita si ugonjwa wa maralia ikabidi tumfanyie maombi maarumu kanisani alikaa siku tatu pale kanisani yale mapepo machafu yalimtoka na kawa safi mpaka leo.
Baada ya mwaka mmoja vita ikarud kwa mama hii haikudumu sana. Naye pia alirushiwa pepo la uchizi akawa anacheka cheka tu kwakua tayari iliwahi kutokea kwa sister tuliingia moja kwa moja kwenye maombi tukitumia mamlaka tuliyo pewa na Mungu kupitia jina la Yesu kristo tukafurumisha mapepo wachafu wakatajana mpka walio watuma wakaondoka.
Miezi michache mbele yule mganga alianza kuugua ugonjwa ambao ulisababisha kifo chake.
Hakika Yesu ni Mkuu alitutendea Makuu bila gharama yoyote.
Sent using
Jamii Forums mobile app