naona watu wanataja kuvuka misukosuko ya maisha kuwa Ni kazi ya Yesu lakini wale tusioamini ktk huyo Yesu tunavuka pia hiyo misukosuko bila kulitaja jina la Yesu Bali kwa imani zetu tunapata kazi,, tunapona ajali,, tunapata nafuu ya maisha,, tunapata uzazi,, tunapona maradhi ya hospitaly na ya kurogwa ,,na tunapata wenza wema, kwa hiyo Kama kigezo pekee Ni kuepushwa na misukosuko ya duniani niseme tu bado sijaona nguvu ya jina la Yesu maana misukosuko inatupata wote na wote tunapona kupitia imani zetu na kufa Kila mmoja atakufa kwa wakati wake bila kujali imani yako ingekua wenzetu hamfi au mkifa mkitaja jina la Yesu mnafufuka hapo sawa. Wandugu tunapona kwa imani ndo maana hata mababu zetu waliokua wakiabudu mawe na Miti mikubwa walikua wakipata majanga wanaenda kutambika na mvua zinanyesha lakini SI kweli kua jiwe au mti Ni Mungu na mkumbuke nabii Ayubu alipopatwa na misukosuko mikubwa hakukuwa na jina la Yesu lakini aliomba kwa imani na akapona. Bali Mungu wetu ni mmoja na Hana uchoyo kwa viumbe vyake humpa yoyote amuombae wakati mwingine bila hata kumuomba kupitia kile unachokiamini lakini siku ya hukumu ndo itajulikana Nani aliabudu Mungu wa kweli na Nani aliabudu vilivyoumbwa na Mungu, hukumu inakuja kwa vile licha ya kuwa Mungu wetu Ni mwenye huruma nyingi lakini pia Ni mwingi wa hasira na mwenye wivu pia katupatia akili na ufahamu wa kufikiri na kutafakari hivo ni wajibu Kila mmoja wetu kufikiri na kutafakari sifa,,ukuu na utukufu wa Mungu na kupima Kama kile unachokiomba na kukiabudu kina sifa na ukuu na utukufu wa kuabudiwa. Mtihani mkubwa upo hapo.
Misingi ya kiimani ya Kikristo imejengwa katika sheria na shuhuda.
ISAYA 8:19-20.
19.Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
20.Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
SHUHUDA = Injili, mahubiri, miujiza na neno la Mungu lililoenezwa na Manabii mbali mbali na Yesu kupitia mwongozo wa Roho Mtakatifu.
1 PETRO 1:19-21.
19.Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20.Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
21.Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
SHERIA = Amri 10 za Mungu zilizoshushwa na Mungu juu ya mlima wa Sinai kupitia Nabii Musa "KUTOKA 31:1-9"
YESU ASHUHUDIA SHERIA ZA MUNGU [emoji116]
MATHAYO 5:17.
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
MAJARIBU/CHANGAMOTO NI SEHEMU YA MAISHA NA YESU ANASHUHUDIA [emoji116]
YOHANA 16:33.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.