Wewe kama ni mkristo na nimeona kwa jinsi ulivyoandika unaamini ukristo,lakini nataka nikushauri kitu Mungu anakupenda na naona unahitaji msaada wake.Hii elimu uliyoleta huna hata andiko moja kutoka kwenye biblia kuisupport hata basi tuletee kama imokwenye Quran.Katika ukristo kujadili jambo bila reference au andiko lolote la kwenye biblia linalosupport hichokitu ni sawa na stroy za kijiweni.
Kama unanielewa njoo,PM,Nimekufuatilia naona umeleta video ya mtu aliyekuwa mtumishi wa shetani na sasa anamtumikia Mungu unataka tumsikilize na tujifunze kutoka kwake.Hiki ulichofanya watumishi wengi wanachemka na wanakosea,Yesu alipoondoka alisema sita waacha yatima nitawaletea msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu,yeye ni mfariji,yeye ni mshauri yeye ni mwalimu.
Kwa kifupi chanzo cha elimu au jambo lolote ambalo wakristo wanatakiwa kujifunza linatakiwa litoke kwa Mungu,hii elimu yako haijatoka kwa Mungu na inapingana na maandiko.
Kwanza nakubali watu wanatofautiana nguvu na nguvu inaweza ongezeka,inaweza pungu ana inaweza isha.Wanafunzi wa Yesu waliletewa mtu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ,wakaomba hakupona.Yesu alipomwombea yule mtu akafunguliwa katika kifungo chake.Wale wanafunzi baadaye wakamuuliza Yesu inakuwaje?Akwaambaia mambo mengine hayawezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba.
Ukisoma Efeso 3:20
"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu"
Hapo juu panaonyesha ndani yetu kuna nguvu na nguvu hiyo haifanani i.e tunatofautiana sasa wewe kusema eti mwanadamu ana nguvu ACD 1 hizi ndizo elimu za kupotosha watu.
Katika kitabu cha mambo ya Nyakati 1 Nya 16:11 "Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote".Unaona hapo maandiko yanaonyesha Mungu ndiye anayetujaza nguvu kwa kadri apendavyo,sasa unaposema wanadamu wana nguvu sawa ni kinyume na maandiko.Assume una watu wawili "A" na mwingine "B".Mtu "A" anabidii sana katika kumtafuta Munguna nguvu zake lakini mtu "B" hana bidii.Iweje hawa watu wawe na nguvu sawa?
Kosa ambalo limekuwa linafanyika katika makanisa ya leo nikuwapa muda waliokuwa watumishi washetani wawafundishe(sikatai mtu anaweza kuwa alikuwa mtumishi wa shetani na akarudi kweli kumtumikia Munghu) lakini hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba hiyo elimu anayowafundisha kanisani imetoka kwa Mungu?Kama haikutokamkwa Mungu na aliipata kwa shetani siyo sahihi kumpa muda awafundishe.Badala yayeye kukaa nyie mmfundishe,yeye anaanza kuwafundisha nyie mambo ya kuzimu ambayo hata hamna uhakika kama anachowaambia ni kweli au si kweli.Tena akiweka na maandiko kidogo ndiyo mnapatikana kweli.Je mmesahau ya kuwa shetani ni baba wa uongo?Je hujui kama shetani kuna muda huwa anasema ukweli kidogo ili akunase?Elimu inayotakiwa kufundishwa kanisani chanzo chake ni lazima iwe Mungu na siyo shetani.Kama Mungu anataka tuyajue yanayofanywa upande wa giza yeye ana uwezo wa kuyaweka wazi.Yesu alipokuwa anatoa pepo alikuwa haruhusu mapepo yaanze kuto maelezo,leo hii eti mtumishi anamsikilza pepo anavyotoa amelezo "tulimtesa sana huyu,bibi yake anamhitaji awe cmhawi,pepo anaongea nawe unasadiki,lakini hapo ujue kuna ukweli umechanganyikana na uongo....".Enzi za Yesu alikuwa anasema "Pepo ninakuamulu ukae kimya na umtoke mtu huyu,leo mtumishi anapiga story na mapepo,"ehe Mlivyomchukua mlimfanya nini...?? .Nawahurumia sana wale manojiita Wakristo na hamna muda wa kusoma biblia na kuyafuatilia haya mambo.Someni biblia ili muijue kweliotherwise utaingia kwenye mitego ya adui.
Kwa hiyo hii elimu yakoya kipimo cha nguvu ni batili,ila kama utaweza kuniletea maandiko kutoka kwenye biblia yanayoisupport yamkini naweza kukubaliana na wewe kama utakuwepo ushahidi.Nawakaribisha Private (pm) kwa ushauri na maswali.
Regards
Aqua
Mtumishi nimekuelewa kwanza Mimi namkubali zaidi mtu aliyekuwa gizani au aliyekuwa mtumishi wa shetani na akaacha na akaamua kumtumikia Mungu,huyu ndie mtumishi sahahi ambae Bwana amemuita sababu alikuwa kwa shetani akiamini ndie nguvu kuu kuliko Yesu,katika misukosuko yake shetani akashindwa kumsaidia na kumuokoa dhidi ya kombora toka kwa Yesu akageuka sasa kama shetani mwenyewe niliyekuwa namuabudu namtegemea amekula kona kaniacha nipambane na hali yangu dhidi ya Yesu, au walipokuwa wakienda kwenye nyumba za watu wa Mungu wanakuta moto wa gesi,mlima mkubwa,barafu,nk au walipokuwa wanaenda mahospitalini kuchukua vitoto vichanga vyenye ulinzi wa Mungu awasogei yaani wanakutana na moto wa kwann mtu huyu asione kumbe Yesu ndie mwenye nguvu zaidi kuliko shetani, kama shetani mwenyewe anakimbia. Utapambana vipi na shetani kama umjui vizuri anavyotenda Kazi, ukitaka kumjua adui ni vyema umjue. Kuwa mtumishi wa Mungu kwa kujifungia tu kwenye elimu ya Ukristo pekee bila kujifunza elimu zingine wewe bado ni mchanga, utajua vipi sasa utendaji Kazi wa ulimwengu wa roho, maana huwezi ongoa roho kama uujui vizuri ulimwengu wa roho. Hawa waliokuwa watumishi wa shetani wanaujua vizuri tena in deep zaidi ulimwengu wa roho kuliko mtu aliyepata elimu tu ya darasani bila vitendo. Zipo shuhuda za watu walikuwa gizani leo ni watumishi au ni Wakristo wazuri zaidi ya waliozaliwa kwenye Ukristo baada ya kuijua kweli,Tazama mtume Paulo kabla ndie aliyewaua Wakristo wengi sana kabla ajakutana na nguvu ya Yesu akiwa kwa shetani akiamini ndie nguvu kuu kuliko,baada ya kupata wongofu akawa Mkristo ndie aliyeanzisha makanisa mengi Sana na ndie aliyechangia Sana kuenea kwa Ukristo asia ndogo na ulaya mashariki,mtu alikuwa mchawi na jambazi Sugu ameua maelfu leo anamuhubiri Kristo akinifundisha ubaya wa dhambi kwann nisimuamini zaidi. Mimi nazungumzia elimu ya ulimwengu usioonekana tena elimu ya jumla sio category ya Christianity au Quran. Ukitaka kuujua ulimwengu usioonekana ambao upo pande mbili wa giza na nuru usijifungie tu kwenye elimu yako tu jifunze pia imani zingine wao wanasema nini.
Sijasema wanadamu wote Wana nguvu ya imani sawa ,nimesema mwanadamu kiasili ana asilimia moja, asilimia ya nguvu ya imani upanda au ushuka kulingana na mtu anavyotumika na upande aliouchagua.Wapo watu Wana nguvu kuliko majini kulingana na jinsi walivyojitoa kwa shetani, na kuna watu Wana nguvu ya imani asilimia 90 karibia ya Jesus.
Watu watajuaje madhara ya dhambi uchawi, wizi, nk kama wasipofundishwa na kupata shuhuda, mtu aliekuwa kwa shetani akatoka ni rahisi kwa anaetaka kuingia kwa shetani kusita sababu tayari anajua madhara kabla ya kuingia. Hio Efeso 3.20 tayari hapo ushataja nguvu kuu ambayo mwanadamu kajiunganisha nayo, sasa kama huna nguvu uliyojiunganisha nayo utasemaje unayo nguvu, maana nguvu yeyeto ni lazima itoke kwenye asili ya hio nguvu. Si Quran na Biblia pekee ndo zina habari kuhusu ulimwengu usioonekana, zipo elimu zingine zimeeleza kwa kina zaidi.
Yesu Kristo alikuja kuwakomboa watu watakao kukomolewa dhidi ya nguvu za giza so alikuja kuhubiri juu ya ufalme wa Mungu baada ya kuona wanadamu wanaangamia, wanateswa, akasema Mimi ndie njia ya uzima na kweli kwa jina langu mtazishinda nguvu za giza. Hapa Yesu kaongea kwa ujumla, sasa utazishindaje nguvu za giza kama ujui zitendavyo kazi Ili umshinde adui ni lzm umjue adui. Yesu hakufundisha kuhusu nguvu za giza lakini mwanadamu anateswa na nguvu za giza.
Waliokuwa watumishi wa shetani kama Sauli to Paulo ndio watumishi sahihi maana walikuwa kwenye giza wakidhani wapo kwenye nuru, baada ya kuijua Nuru ya kweli huwa watumishi wa kweli na sio watumishi wa sadaka. Mimi nimezungumza uKuu wa jina la Yesu kwa elimu ya jumla ikiwemo hata walio nje ya Ukristo.
Mtumishi usijifungie kwenye Ukristo pekee soma pia elimu zingine Ili uimarishe imani yako. Binafsi kupitia elimu zingine nje ya Biblia nimejifunza hakuna jina jingine kuu lenye nguvu kuliko jina la Yesu kwa ushahidi wa hata elimu zingine.