Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

ELNINO - Nataka mmalize kwanza suala hili la mafuriko - kila mwaka mafuriko mafuriko. hamuwezi kuzuia? na wanaokaa mambondeni wahame. nawakilisha wito wangu kwa JF.
 
VeraCity (au Veracity) maana yake ni UKWELI.
Nimeamua kutumia jina hili kama kielelezo cha mwelekeo ninauotaka au ninaoamini na kuutumia.Uongo kwenye serious forums kama JF unaondoa maana nzima ya kuwepo kwa forum yenyewe.

nilipokuwa sec nilikuwa na ma frnds zangu watatu, tulikatiana hivyo vijina vya ajabu ajabu tu kama hivyo, mie ndio nikakatiwa Nyamayao.

MTM = initials representing majina yangu matatu, M la kwanza, T la pili na M la baba yangu!!

Nyie hapo juu mnazo double ID na nimefanikiwa kuwagundua kwamba:
1. WomanOfsubstance = veracity
2. Babra = Nyamayao
3. De Novo = MTM

Kaazi kwelikweli!

Mkaa Mweupe: kwa kawaida mkaa ukiwa umepoa rangi yake ni nyeusi ila ukikolea moto huwa na rangi nyeupe, hapo kuushika yataka moyo. Ndivyo nilivyo.
 
Tamka 'mtu be'. Ni jina walilonipa marafiki tangu nikiwa shule ya sekondari. Sababu zake zilikuwa mbili: Kwanza umbo langu la mazoezi, wenzangu walikuwa wanadai niko sawa na watu wawili. Pili nilikuwa na tabia (sijui mbaya?) ya kudai shea ya watu wawili wakati tunagaiwa nguna (ugali) kule DH (dining hall) la shule, kila mara nilimwambia mwanafunzi anayegawa nguna siku hiyo anijazie shea ya 'mtu be' (watu 2) kwenye sahani yangu ya bati (TG).

''E banae nigee shea ya mtu be mshkaji wangu, si unajua nimetoka kwenye tizi au vipi!''.

Basi ndio jina likashika tangu wakati huo, kuna wengine tuliosoma shule moja hadi leo hawanijui kwa jina lingine zaidi ya Mtu B.
 
Duuu,,,................................
Niliwahi kufanya kazi Na maprofessor wa Harvard miaka ya 2004 moshi, nikazinguana na mabosi zangu walikua wananilipa vizuri sana kipindi hicho kazi yenyewe nilipata kibahati then nikaacha kazi kwa hasira, nikaingia mtaani nikahustle saana tuu kwa 2 years then nikaishi porini huko tanga kwa mwaka mmoja maji ya madimbwi kuoga ilikua ishu no phone no what msosi ilikua ishu nikarudi mjini nikapigwa miezi sita jela nikatoka nikaenda znz mwaka 1 porini kabisa huko kizimkazi kwenda hta town ilikua ishu nikateseka na wachina kinoma tulikua tunajenga mi kama kibarua then,,,, mwaka jana nikaingia mjini mambo yakaanza kwenda saafi....noti ikakubali na hapo nikafikiriiiiiiaaa weeeee nikagundua kweli "maishapopote" Hiyo avatar ni picha ya arnold schwazernegger akiwa gym miak ile eee kipindi kile akiwania mr olympius then nikaangalia mtiririko wa maisha yake hadi sasa amekua gorvenor bado naamini
maisha popote...........na sikati tamaaa!!!!!!!!!!!
 
ELIMUMALI: Jina hili nilimelichagua kwa kuwa naamini 100% kuwa elimu ni mali, na kwamba humu jamiiforum, nitaelimika. Wengine husema AKILIMALI, ni sawa pia lakini mie naamini kuwa akili unaweza kuwa nayo, lakini elimu ikakupiga chenga kutokana na sababu mbalimbali. Ila mwenye elimu obviously ana akili, otherwise ataelimikaje bila akili? That is:
With Elimu there is akili in it, but
With Akili not necessarily that Elimu will be there but still you can make money (rich)

Au?
 
Mimi jina langu nimelimaanisha..am Gender Sensitive na kweli niko hivyo...na hata nikisajisajili kwa jiana lingine nitakuwa namaanisha. My name suggest who iam ..hata kama ningepata fursa ya kujichagulia jina kwenye jina langu halisi basi ningechagua jina lenye maana...pamoja na hayo I like my real name so much ingawaje halina maana yeyote ya msingi.
 
TzPride==kuna mizungu ilikuwa ikipenda kunipachika hilo jina kiutani tukiwa ofisini, hasa kama nikiwasemea mbovu wakati wanaikandia nchi yangu....utawasikia ..mmh Tz pride! Nina matatizo ya kutomvumilia foreigner akiisaga nchi yangu kwa dharau.
 
As beautiful as it is,the way it sound and pronounced,thats me and thats my real name,Thx mum for giving me these lovely name.
 

Mwaka mpya na mambo mapya sio double IDs wewe!!!!
 
Janjaweed... not what you are thinking!!! not central africa rebels ...but jani la akili (smart wheed)
 

Shukrani Mkuu nakubaliana nawe kabisa kwamba maisha ni popote.
 

Ahsante Mkuu nilikuwa nawaza sana huu mkaa mweupe ndiyo mkaa gani tena yarabi! ahsante kwa kutufungua macho.
 
Mie niliamua kuchagua Jina la MAARIFA nikiamini kwa watu wengi huonewa, hukandamizwa, hubezwa, hufanyiwa dhihaka, hurubuniwa na madhira mengi kwa kukosa MAARIFA. Jina hili MAARIFA ni nguzo na taji kwa binadamu yoyote. Humfanya awe huru na aweze kujiamini popote alipo. Huondoa hofu, humfanya mtu kuwa na mang'amuzi ya mazingira yake na hivyo kufanya maamuzi yake yaliyokamilika bila kuyumbishwayumbishwa. Bila Maarifa utu wako haujakamilika. Tutafute Maarifa!!! na Hakika Mungu atatubariki.
 
You can't catch me, I have the ability of escaping or vanishing whenever I like.
 


KAITABA, ni uwanja wa mpira upo mkoani Kagera, mama yangu mzazi alikuwa bosi enzi hizo, akiwa anakagua gwaride uwanjani hapo akashikwa na uchungu,

Alipopelekwa chumba cha faragha uwanjani hapo nikazaliwa mimi,


QUOTE=Mwawado;630106]Mwawado: Ni Upondo,Mti mgumu na una umbo la Fimbo,unatumika na Wavuvi kuweka nyavu vizuri (kutanua matundu ya nyavu za uvuvi) na mara nyingine hutumiwa kama silaha katika majazi.Jina Mwawado asili yake ni kabila la Digo.Miti hiyo mfano ya mianzi huota pembezoni mwa bahari ya Hindi, ukanda wa Pwani kutoka Mwambani mpaka Pangani.Mwawado pia ni jina maarufu la Ukoo huko Tanga.[/QUOTE]

Ama hakika nimevutiwa sana na ufafanuzi wa mjina haya! You have made my day!
 
Wakati niko school A level nilikuwa napenda sana mambo ya diplomasia na nilikuwa na dream kwamba siku moja nami niwe balozi wa Tanzania katika nchi yoyote.
Wenzangu walinipachika jina la Ambassador na wakanishauri nisome International Relations. Matokeo yake? Sikuwa hata balozi wa nyumba kumi! I still treasure and honor my friends, and ofcourse my dream...... With due respect....


NGALIKIHINJA


Very interesting.........!!! 🙂
 

Hili jina limeshika kabisa ijapokuwa silitumii officially...watu wengine hawajui kuwa nina majina mengine!!!



JF is great...and its members are great thinkers!!! Zimenifurahisha sana hizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…