Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,303
Isiyo ogopa, yenye kujiamini, liwalo na liwe ili mradi anachokiamini kifanyike, asiye katishwa tamaa,mwenye msimamo, asiyeyumbishwa. Haya yote ni baadhi maneno yanayoweza kutoa maana ya KYACHAKICHE!Wengine je? Kuna majina mengine kama Kyachakiche, n.k
Lekanjobe = Hebu niseme
Babu yangu alikuwa msema kweli, akiwa msuluhishi katika jamii yake. Hakuwa na subira kumwambia waziwazi mtu yeyote anayeharibu "Kubinika!" yaani "Unaharibu!" hata kama ni kiongozi. Wakampachika jina la Kubinika kwa utani na ikamkaa hadi kifo chake.
Madule ni jina la kilugha lenye maana ya viazi vitamu.. huwa linanikumbusha enzi za utoto tukichunga mbuzi na n'gombe kule kikjijini. tulikuwa na kawaida ya kutengeneza kitu inaitwa kabunguja, hutengenzwa kutumia udongo ambapo ndani yake huwekwa moto hadi huwa ya mato red hot then tunaweka viazi tulivoiba mashmabani kwa watu, tuliluwa na style ya kuiba ambayo ilikuwa sio rahisi kukamatwa.kwa kuwa mashmaba mengi ya viazi yaliwa katikati ya shamba la mahindi ma mara nyingi wakina mama walikuwa ndio walinzi, style ilikuwa ni kwamba tukifika hapo tunaanza kusalimia kwa sauti kubwa ( mamaaa shikamooooo!, pole na kaziiiii! mara mamaa mbona upo kimyaaaa! naomba maji ya kunywa!, tukiona kimya tunajua salama, tunajisevia weee, tunahama kama km 3 hivi kutengeneza kabunguja!
Jamani maisha ya utotoni raha saaana. gone those good days
M-bongotz kwa sababu najivunia utanzania wangu pamoja na shida zote tulizonazo.
Silaha ya Masikini wote duniani ni kuwa na msimamo; Jeuri ya Masikini ni kutokubali kuonewa na mwenye nacho!
Masikini jeuri ni jina nililorithi toka Kwa Babu yangu; alikuwa masikini na alibahatika kupata watoto watano wote wa kike; Babu yangu alijitahidi kuwasomesha wote pamoja na itikadi potofu ya wakati huo ya kutomthamini mwanamke!
Najisikia fahari kumuenzi kupitia jina hili! Nimekuwa nikilitumia katika forums tofauti na wale waliobahatika kupiti Young African nililitumia sana huko pia.
Tamka 'mtu be'. Ni jina walilonipa marafiki tangu nikiwa shule ya sekondari. Sababu zake zilikuwa mbili: Kwanza umbo langu la mazoezi, wenzangu walikuwa wanadai niko sawa na watu wawili. Pili nilikuwa na tabia (sijui mbaya?) ya kudai shea ya watu wawili wakati tunagaiwa nguna (ugali) kule DH (dining hall) la shule, kila mara nilimwambia mwanafunzi anayegawa nguna siku hiyo anijazie shea ya 'mtu be' (watu 2) kwenye sahani yangu ya bati (TG).
''E banae nigee shea ya mtu be mshkaji wangu, si unajua nimetoka kwenye tizi au vipi!''.
Basi ndio jina likashika tangu wakati huo, kuna wengine tuliosoma shule moja hadi leo hawanijui kwa jina lingine zaidi ya Mtu B.
Mimi nazani jina langu lina jieleza, Kibanga Ampiga Mkoloni, Nadhani mnakumbuka habari za huyu jamaa enzi zile za primary kwenye vitabu jamaa alimtoa nduki mkoloni kijiji kwao.
Naomba msaada hivi kama kuna post ina muabuse mtu tunafanyaje humu?
Mwazange = kijiji kimoja nyanda za juu mashariki.....kina unasaba fulani hivi na mimi...