Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Ni jina langu na hata picha ni yangu

Amani Iwe Kwenu
 
Ni jina langu na hata picha ni yangu

Amani Iwe Kwenu

Iwe kwako pia Mchungaji, twambie basi maana ya jina hilo. Hiyo picha mhhhhhhh! I reserve my comments hahahahahahah. Mrs hajambo?

 
M-mbabe = mtu wa undava undava hususani dhidi ya fisadi's
 
Iwe kwako pia Mchungaji, twambie basi maana ya jina hilo. Hiyo picha mhhhhhhh! I reserve my comments hahahahahahah. Mrs hajambo?


Maana yake ni Makutano yenye busura, ama Muungano wenye Busara! Mamaa Mchungaji iko haijambo. Ila sijui kala nini iko tema mate sana
 
Maana yake ni Makutano yenye busura, ama Muungano wenye Busara! Mamaa Mchungaji iko haijambo. Ila sijui kala nini iko tema mate sana

Hahahahahahaha labda ushajeruhi mtu LOL! ngoja tusubiri kwanza kabla hatujawapeni hongera zenu :whoo:
 

Ni mawazo mema, nia njema, pambazuko wakati wa kiza kinene kabla ya asubuhi halisi ndani ya nchi ambayo wengi wameanza kukata tamaa ya kuishi kama wenzao wengine duniani! Ni tunda jipya la kisiasa na kijamii, furaha kwa waliokosa usingizi kwa kulala kwenye vitanda vyenye kunguni, wakianza kufurahia mwanga utakaowaliwaza mpaka asubuhi itakapofika ili wawaue hao kunguni kwa jua kali lisilo na huruma.

Ubarikiwe BAK kwa swali zuri na lenye wingi wa busara ndani yake!
 
Mokoyo ni jina langu la halisi, ni jina la kikabila maana yake siijui
 
mzuanda, ni mtoto wa mwisho,na wazazi wangu wananiita hivyo most of the time wakitaka kunimwagia misifa
 
sulphadoxine ni dawa ya malaria ambaye kwa sasa aipatikani madukani,(sp)nimechagua hili jina la dawa kwa sababu ilikua inanisaidia sana kuliko hizi dawa za sasa hivi(mseto)
 
MPASUAJIPU : Hili jina nilichagua kwa sababu napenda kusema ukweli hata kama unauma.

Unajua jipu linauma sana na dawa yake ni kulipasua na kutoa taka zilzomo ndani yake.

Sipendi kuficha mambo kwani hata jipu ukilificha ipo siku litapasuka lenyewe tu likiiva.

na hisia zangu ni kuhusiana na serikali zote dhalimu na mafisadi wanaodhulumu wanyonge ni kama jipu ambalo km hatukulipasua basi kuna siku litapasuka lenyewe tu.
 
Nilikuwa nimepotea wakati sredi hii inaendelea.

Zakumi - Ni mascot iliyotumika kwenye world cup 2010, nchini Africa kusini. Nilichagua mascot hii ni kwa sababu ni chui (Leopard). Mnyama mwenye kupenda uhuru na kuwa pekee yake (solitary animal). Hawezi kufugwa. Hatabiriki. Instinctive. Territorial. Eat fresh meat. Risk taker.

Hivyo nili-create a character yenye persona za chui kama ifuatavyo:-
---Hakuna urafiki wala kujuana hapa JF (solitary animal)
---Hafuati imani au kundi la watu, yuko tayari kutetea au kupinga ideas hata kama atabaki pekee yake (hawezi kufugwa)
---Hana personal issues ana connect dots tu (Instinctive)
---Ana maeneo na topiki zake (territorial)
---Anapenda idea mpya (Fresh meat Easter)
---Mgomvi wa mawazo na haogopi kujaribu (Risk taker)
 
bob giza, kwa rangi ni kama ile kitu tanesco wanawapa raia kupitia mgao nyakati za usiku...yaani ni full masizi wa kutosha..ni ivo tuu!!
 

Kwenye nyota umenkumbusha Dodoma Hotel(DH).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…