Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Njowepo = nami niseme/niseme/naweza sema
Iwe kwako pia Mchungaji, twambie basi maana ya jina hilo. Hiyo picha mhhhhhhh! I reserve my comments hahahahahahah. Mrs hajambo?
Maana yake ni Makutano yenye busura, ama Muungano wenye Busara! Mamaa Mchungaji iko haijambo. Ila sijui kala nini iko tema mate sana
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?
Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.
Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.
Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.
Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.
Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukubi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.
Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
MAHESABU.........! ni....
Kilaza
Tamka 'mtu be'. Ni jina walilonipa marafiki tangu nikiwa shule ya sekondari. Sababu zake zilikuwa mbili: Kwanza umbo langu la mazoezi, wenzangu walikuwa wanadai niko sawa na watu wawili. Pili nilikuwa na tabia (sijui mbaya?) ya kudai shea ya watu wawili wakati tunagaiwa nguna (ugali) kule *DH* (dining hall) la shule, kila mara nilimwambia mwanafunzi anayegawa nguna siku hiyo anijazie shea ya 'mtu be' (watu 2) kwenye sahani yangu ya bati (TG).
''E banae nigee shea ya mtu be mshkaji wangu, si unajua nimetoka kwenye tizi au vipi!''.
Basi ndio jina likashika tangu wakati huo, kuna wengine tuliosoma shule moja hadi leo hawanijui kwa jina lingine zaidi ya Mtu B.