Che - ni kiambishi awali cha sifa ya hadhi.
Yaani kama unaitwa Sombi basi ukishatoka jandoni unaitwa
Che Sombi.
Ni kama makabila mengine yanatumia viambishi awali kama
She - Lukindo
Mwa - Kipesile
Se - Kalinga
Se - Ntongo, nk.
Wazungu utasikia wanaitwa
Allex, Mc - Neell
Perez, De - Quere, nk
Mittoga ni jina la hadhi ya ukoo.
Kumbuka ile "Che" ni kiambishi awali cha sifa ya hadhi, na sio jina.
Kwa mfano ukimsaidia mtu ktk tatizo kubwa anakuja kukushukuru hata kama unaitwa Ally hatamki Ally.
Bali anasema
"Usengwile Mittoga" kama ni mwanamume asiye pitia jandoni, kama kapitia jandoni utaunganisha Kiambishi awali cha sifa ya hadhi na jina la hadhi ya ukoo na utatamka
Che mittoga
Kwa maana ya " Asante Ally "
Hapo inamaana wanaume wa ukoo wa "Chapanjila" wote kama yeyote atafanya jambo zuri hivyo kutakiwa kushukuriwa au kuombwa radhi basi jina litakalotumika ni " mittoga "
Asante Che mittoga
Samahani Che mittoga.
Ndio maana nikatumia hiyo
Avatal.
Usengwile makamanda.
Kunjani
Sent using
Jamii Forums mobile app