Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

atae nipa maana halisi ya Majimshindo nampa zawadi, najuwa wapo, lakini sina uhakika kama wanapitia humu.
 
Elimu duni (STD 7) Umasikini wa kipato na umri kuelekea machweo vinatosha kabisa kujiona ni Mwendabure mimi. Jumlisha na siasa mbovu ktk nchi yenye raslimali lukuki naamini mimi ni Mwendabure hakika.
 
kamonga ni jina alipewa baba yangu(RIP) alibakia yeye peke yake kwa baba na mama yake baada ya ndugu zake karibu 6 kufa kila walipozaliwa enzi hizo cjui ni mkunga wa jadi!!!basi yeye aliitwa kamonga yani kamoja tu kaliko bakia!!! he is gone but left four of us to celebrate his uniqueness. i miss u mzee!!!!
 
kilimasera ni mlima mmoja mkali sana katikati ya wilaya za namtumbo na tunduru huko kusini mwa tanzania mkoa wa ruvuma mlima huu ni wa ajabu na una maajabu sana
 
Miaka ya 50 babu yangu aligundua gundi akaiita nyamgluu. Wakoloni wakamchakachulia idea yake. Kwaio namwonyesha babu kuwa mimi bado namkubali na innovation yake. Kaka wa babu ndie aliyegundua Tanzanite nae wakamchakachua. Alilipwa sh 20! Dah if only....

jamani pole.
 
Mimi ni mtu wa furaha muda wote, napenda kusifu, napenda kushangaa na kushangalia. Ninahakikisha kabla ya kulala ninaingia kitandani nikiwa na furaha, nikiamka ninatafuta sababu ya kuwa na furaha. Siku inapita, maisha yanakewnda. MAMMAMIA is an Italian expression!

Nikiona zuri, Mammamia!; baya, Mammamia!; mchangiaji ameweka vitu safi, Mammamia!; hata anayeboa, Mammamia!; msichana aliyeumbika, oooooh, Mammamia!

Otherwise ningeweka OMG (Oh My God), lakini hii nimeipenda zaidi.

na kweli ndivyo ulivyo.
Nalipenda jina lako. Wewe ni she/he?
 
Iholomela, ni jina la manju (Nnengi) maarufu wa ngoma za jadi katika kijiji chetu cha Ndembezi, wilayani Igunga. Nilipokuwa shule ya msingi darasa la tatu nilikuwa mmoja wa wachezaji wa ngoma yake, nikiitwa jina la utani "MAHOFU GALIMISHA" naitikia "MISHAGA NKE WANE TWINYELAGA". Jamaa alishafariki, hivyo naendelea kulienzi jina lake.
 
images
mbu, who's mbu?

“If you think you're too small to be effective, you have never been in bed with a mosquito.”

Tangu nilipojiunga na JF miaka takriban minne iliyopita, Forum hii imeendelea kuwa mwiba kwa serikali. Big Up kwa members waanzilishi, na wengineo wengi ambao mmeiwezesha JF kuwa gumzo Bungeni na kwa viongozi wengi wa Vyama na serikali Tanzania.

Kwangu mimi naichukulia JF kama mdudu mbu, ambaye hata ujifunike chandarua, bado atakuimbia usiku kucha na kukunyima usingizi. JF ni forum, binafsi kama mwanachama wa JF najichukulia kama miongoni mwa mbu tuliogawana majukumu ya kumpigia kelele "mlalaji" aka serikali kwa namna moja au nyingine!

Big Up kwa wanachama wote wa JF, We Make A Difference!
 
Mimi naukumbuka ule mwiba wa Mchongoma....teh teh teh
 
architect is my real proffesion, mimi ni designer wa majengo, na pi mjenzi... Na e.m ni initials za my real name.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
images
mbu, who's mbu?

"If you think you're too small to be effective, you have never been in bed with a mosquito."

Tangu nilipojiunga na JF miaka takriban minne iliyopita, Forum hii imeendelea kuwa mwiba kwa serikali. Big Up kwa members waanzilishi, na wengineo wengi ambao mmeiwezesha JF kuwa gumzo Bungeni na kwa viongozi wengi wa Vyama na serikali Tanzania.

Kwangu mimi naichukulia JF kama mdudu mbu, ambaye hata ujifunike chandarua, bado atakuimbia usiku kucha na kukunyima usingizi. JF ni forum, binafsi kama mwanachama wa JF najichukulia kama miongoni mwa mbu tuliogawana majukumu ya kumpigia kelele "mlalaji" aka serikali kwa namna moja au nyingine!

Big Up kwa wanachama wote wa JF, We Make A Difference!

Mkuu Mbu nimekukubali............

You wanna see a New Dawn in Your Tanzania? Its just mine wish.........
 
...we acha tu, ilikuwa..."kuupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma!"

Nimelikumbuka hili jina la mchongoma. Kuna wakati nikawa nakutafuta hapa jamvini maana nilikuwa napenda kusoma michango yako. Nadhani nikaulizia jamani yule mchongoma yu wapi? Ukanijibu kwamba umeamua kubadili jina maana kuna njemba moja ilikuwa inakusumbua. Ahsante sana Mbu, kweli JF ni kama mbu mpaka inawatia kiwewe watu wa ngazi za juu kabisa na hivyo kuwakosesha usingizi.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...we acha tu, ilikuwa..."kuupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma!"

Ila ID za JF members wa zamani me nayakubalia sana....cheki list hili

  1. Mbu
  2. Chloroquine
  3. Malaria Sugu
  4. Asprin
  5. Nyani Ngabu
  6. Bubu Ataka Kusema
  7. Kichuguu
  8. ................
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

Ila ID za JF members wa zamani me nayakubalia sana....cheki list hili

  1. Mbu
  2. Chloroquine
  3. Malaria Sugu
  4. Asprin
  5. Nyani Ngabu
  6. Bubu Ataka Kusema
  7. Kichuguu
  8. ................

8. Kisura
9. Mwafrika wa Kike
10. Mwanakijiji
11. Fundimchundo
12. ..............
 
Viper au kifutu-msitu this is some crazy snakes man! "not only he`s better looking hez plain better" and that reflects me.. in short najikubali .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimelikumbuka hili jina la mchongoma. Kuna wakati nikawa nakutafuta hapa jamvini maana nilikuwa napenda kusoma michango yako. Nadhani nikaulizia jamani yule mchongoma yu wapi? Ukanijibu kwamba umeamua kubadili jina maana kuna njemba moja ilikuwa inakusumbua. Ahsante sana Mbu, kweli JF ni kama mbu mpaka inawatia kiwewe watu wa ngazi za juu kabisa na hivyo kuwakosesha usingizi.

...acha tu, Anyway,....maisha yanaendelea.
Nimefurahi sana jana nimesoma wakongwe wakijadiliana hii mada https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/127176-chadema-shadow-cabinet-jokers-and-comedians.html just like those Good Olden Days.

nawakumbukia wakongwe kina FMES, Fair Player, Halisi, Mwafrika wa Kike, Game Theory, Saidi Yakubu, Mtanzania, Mzelendo halisi, Kada Mpinzani na wengi wengineo!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom