Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Au wewe ndio"dowans siijui, mmiliki wake simjui inafanya nini sijui"Mokoyo ni jina langu la halisi, ni jina la kikabila maana yake siijui
atae nipa maana halisi ya Majimshindo nampa zawadi, najuwa wapo, lakini sina uhakika kama wanapitia humu.
Miaka ya 50 babu yangu aligundua gundi akaiita nyamgluu. Wakoloni wakamchakachulia idea yake. Kwaio namwonyesha babu kuwa mimi bado namkubali na innovation yake. Kaka wa babu ndie aliyegundua Tanzanite nae wakamchakachua. Alilipwa sh 20! Dah if only....
Mimi ni mtu wa furaha muda wote, napenda kusifu, napenda kushangaa na kushangalia. Ninahakikisha kabla ya kulala ninaingia kitandani nikiwa na furaha, nikiamka ninatafuta sababu ya kuwa na furaha. Siku inapita, maisha yanakewnda. MAMMAMIA is an Italian expression!
Nikiona zuri, Mammamia!; baya, Mammamia!; mchangiaji ameweka vitu safi, Mammamia!; hata anayeboa, Mammamia!; msichana aliyeumbika, oooooh, Mammamia!
Otherwise ningeweka OMG (Oh My God), lakini hii nimeipenda zaidi.
Tangu nilipojiunga na JF miaka takriban minne iliyopita, Forum hii imeendelea kuwa mwiba kwa serikali. Big Up kwa members waanzilishi, na wengineo wengi ambao mmeiwezesha JF kuwa gumzo Bungeni na kwa viongozi wengi wa Vyama na serikali Tanzania.
mbu, who's mbu?![]()
"If you think you're too small to be effective, you have never been in bed with a mosquito."
Tangu nilipojiunga na JF miaka takriban minne iliyopita, Forum hii imeendelea kuwa mwiba kwa serikali. Big Up kwa members waanzilishi, na wengineo wengi ambao mmeiwezesha JF kuwa gumzo Bungeni na kwa viongozi wengi wa Vyama na serikali Tanzania.
Kwangu mimi naichukulia JF kama mdudu mbu, ambaye hata ujifunike chandarua, bado atakuimbia usiku kucha na kukunyima usingizi. JF ni forum, binafsi kama mwanachama wa JF najichukulia kama miongoni mwa mbu tuliogawana majukumu ya kumpigia kelele "mlalaji" aka serikali kwa namna moja au nyingine!
Big Up kwa wanachama wote wa JF, We Make A Difference!
Mimi naukumbuka ule mwiba wa Mchongoma....teh teh teh
...we acha tu, ilikuwa..."kuupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma!"
...we acha tu, ilikuwa..."kuupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma!"
Ila ID za JF members wa zamani me nayakubalia sana....cheki list hili
- Mbu
- Chloroquine
- Malaria Sugu
- Asprin
- Nyani Ngabu
- Bubu Ataka Kusema
- Kichuguu
- ................
Nimelikumbuka hili jina la mchongoma. Kuna wakati nikawa nakutafuta hapa jamvini maana nilikuwa napenda kusoma michango yako. Nadhani nikaulizia jamani yule mchongoma yu wapi? Ukanijibu kwamba umeamua kubadili jina maana kuna njemba moja ilikuwa inakusumbua. Ahsante sana Mbu, kweli JF ni kama mbu mpaka inawatia kiwewe watu wa ngazi za juu kabisa na hivyo kuwakosesha usingizi.