Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Malingumu, msemakweli, mwendapole na songambele ni baadhi tu ya swaga za majina ya kwetu hususani enzi hizo.
Kipindi tuko form 3 mie nilikuwa sipendi kabisa bookkeeping lakini nilikuwa noma katika kukotoa makabati a.k.a a/c sasa katikapast papers kulikuwa na swali la songambele lugaha na mwendapole kapori ndio masela wakiangalia ninapotoka na hilo jina ikabidi wanibatize. Nililikataa sana lakini jamaa wakanipa jina na kuhadi daima utasonga mbele.
Naamini katika kusongambele, na nyie msongembele na pamoja tunasongambele.
Kama nakufahamu vile.....lol!
KIMA MDOGO hl jina linanikumbusha nikiwa o level, nilikua nasoma shule 1 na kakayng kwakweli tulikua watundu vya kutosha mm nilikua kiranja hlf ni mwanafunzi bora mwenye akili vby sn bro yy zilikua hazipandi, ilikua ikifika LUNCH TIME IKIWA NI BONDO TUNASEPA KWNY MASHAMBA YA SHULE KUCHOMA MAHINDI sk 1 tukadakwa tukapelekwa kwa head master kwa kweli headmaster alikua ananipenda sn hatukuchapwa ila ALITUSIMAMISHA ASEMBLE NA KUWATANGAZIA WANAFUNZI KW BRO YY NI KIMA MKUBWA NA MM NI KIMA MDOGO WATUCHUNGE SN KWANI TUTAMALIZA MAHINDI YOTE. kwakweli linanikumbusha sn shule
CPA- inamaana ni certified public accountant, mi ni muhasibu. Naipenda kazi yangu. Nimetumia jina hilo na cpa, kuonyesha uma kuwa tupo wahasibu tuopinga na hii hari ya baadhi ya wahasibu wenzetu wakishikiriana na mafisadi kuchota mahela ya walipa kodi walio maskin sana hapa nchini, kwa kujinufahisha wenyewe na familia zao. Nawakilisha
Kipindi cha nyuma nshawahi kuwa Dj kwenye sherehe mbali mbali Jijini Mbeya hivyo huwa sisahau kazi yangu ya awali.