Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Nimejaribu kuvumilia nimeshindwa! Kuna majina huwa yananitafakarisha sana! Kila ninaposoma nyuzi za baadhi ya watu huwa najikuta nalitazama jina la muhusika na kuzama katika lindi la mawazo nikitafakari lina maana gani?

Hivi kwa mfano wewe Imeloa, una maana gani kujipa hilo jina? Ni nini hiyo iliyoloa? Kuna huyu Bwana Utamu nk. Majina yenu kwa kweli huwa yananifanya niwaze na kuwazua. Naomba mtushirikishe maana hasa ya kujiita mlivyoamua kujiita.

Jina lako lina maana yoyote? Tushirikishe tafadhali kwa nini umejipa jina hilo?

Kwangu mimi Elisha ni jina la meanangu. Wewe je? Hebu twende kazi! Kwa nini umejiita ulivyojiita? Hii ni kwa wote tafadhali siyo tu kwa ndugu Imeloa!

Ahsante
Naambiwaga nina tabia nzuri kila napoishi nimeona nijiite tu roho mtakatifu
 
Back
Top Bottom