Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Lily is my real name, na Flower imetokana na ua linaloitwa "Lilies" ndio nikaunganisha Lily Flower na pia ndio nick name yangu tokea nikiwa shule ya msingi mpaka sasa hivi linaendelea, zaidi ya yote I like Flowers.
 
Ziondaughter au Binti Sayuni

Sayuni mji mtakatifu wa Mungu ulioteuliwa kwa ajili ya wateule.Waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache.

AMINA Wajina

Na sisi ni miongoni mwa hao wateule wachache.Jina hili tulikuwa tukiitana shuleni kwa wale mabinti waliokuwa wameokoka
 
Unaweza kumpata kama kweli ulimpenda usikate tamaa, kumbuka milima haikutani lakini binadamu twakutana.
Huwezi amini mie mtu ambaye tulipotezana miaka 13 iliyopita , tumekutana kumbe na yeye hivyo hivyo kama wewe ulivyosema alikuwa ananipenda lakini hakunitamkia chochote. Kumbe alikuwa ananifatilia information zangu kinyemela.
Mwisho ikawaje?
 
Linatokana na simu niliyokua natumia ukitaka kupokea ilikua inabidi uifyatue na inatoa mlio kama mtu anakoki silaha ndio watu wakanipachika mzee wa AK-47
 
Jina langu liko wazi kabisa hata kama nisipoeleza mengi lina direct translation. MCHUKIA FISADI.

Kwa miaka mingi nimekuwa nikichukia sana jinsi mafisadi walivyogeuza nchi yetu kuwa shamba la kuvuna huku wenye shamba hawaambulii hata magunzi tu.

Nilipoifahamu jf kwa mara ya kwanza, wakati huo ikiwa inaitwa Jambo nilivutiwa na michango mingi ambayo ilikuwa inapingana na mafisadi, Kiasi kwamba kwa kipindi hicho ndipo ilitokea seleka ya kukamatwa waanzilishi wa Jambo forum huku wakiifungia na kuzaliwa kwa Jamii forum.

Kwa kuwa nami nilikuwa ni mmoja wa wapingao ufisadi nikajikuta naitwa mchukia mafisadi.

Najulikana hivyo kazini kwa mwajiri wangu na hata mtaani kwangu wananifahamu kwa jina hili hili. Wengine hawajui hata kama nina jina lingine la kanisani kwetu.

Ajabu ni kwamba hata majina yangu halisi yanaanza kwa herufi za M na F.

MF
 
KAITABA, ni uwanja wa mpira upo mkoani Kagera, mama yangu mzazi alikuwa bosi enzi hizo, akiwa anakagua gwaride uwanjani hapo akashikwa na uchungu,

Alipopelekwa chumba cha faragha uwanjani hapo nikazaliwa mimi,

Lakini jina hili pia (Kaitaba) ni aina ya pombe huko Kagera kama sikosei
 
mshiiri = mswahili na mbwatukaji wa jambo ambalo watu wengine ustaarabu wao huwafanya washindwe kujadili au kuuliza jambo fulani. asiyeogopa repercations wala implications BUT the truth and a pain in the ass to wrong doers.
 
Jina langu... linatokana na Beer yangu kipenzi Tusker... niliyoinywa tangu 1990 Moshi wakati ule zikitokea Kenya kwa njia ya magendo na zilikuwa zauzwa sh.250/- na wakina mama wa kichagga walikuwa wanazitoa Himo Eneo la Kitobo kwa viroba...
 
Ahaa! Ni vyema nami mkaelewa maana ya jina langu MONGOIWE; MONGO inamaanisha Supu na IWE ni jiwe hivyo linamaana ya supu ya Jiwe, jina hili asili yake ni kanda ya Ziwa na linatokana na kabila ya KISUKUMA.
Jina hili mimi kwangu nilipachikwa na babu yangu kotokana na yeye kupenda kunitania lakini pia tabia yangu ya kupenda kukimbilia mlimani kilamara kupanda mawe na majabari ya Mwanza.
 
Maana yake halisi ni kuchanganyikiwa unakuwa hujielewi hujui hili wala lile....Ni jina nimeamua kulitumia hapa JF baada ya kutembelea bongo 2005, baada ya kukaa ughaibuni kwa nearly 10 years.Yaani nilikuta bongo iko vile vile hamna mabadiliko yoyote maji tabu,barabara nyingi vumbi,umeme shida,viongozi walewale yaani kwa kifupi nilipata "mauza uza" hii nchi inaenda mbele au inakwenda kinyumenyume.Shida/karaha zilikuwa ni nyingi kuliko raha ya kwenda vacation bongo.Since then naona mauza uza na hali ilivyo na inayoendelea.From bad to worse...!!!!!!
 
I am miner, who explores for value in the forgotten corners and invests in extracting the value, while in the process I unlock the potential of a community (virtual or real).

Since days of old, gold has always been associated with values hence the use of the mineral.

So I am a gold digger, not because I'm someone who develops a relationship with a much older/younger partner for primarily financial reasons, especially to inherit the partner's wealth upon death or any other eventuality.

I am a gold digger because I see value in dirt and I am laborer who is willing to get their hands dirty inorder to unlock value. I am dismissed by many and grab the attention of few, but those who engage me tend to stumble upon a mine of wealth.

I am the gold digger.
 
Ahaa! Ni vyema nami mkaelewa maana ya jina langu MONGOIWE; MONGO inamaanisha Supu na IWE ni jiwe hivyo linamaana ya supu ya Jiwe, jina hili asili yake ni kanda ya Ziwa na linatokana na kabila ya KISUKUMA.
Jina hili mimi kwangu nilipachikwa na babu yangu kotokana na yeye kupenda kunitania lakini pia tabia yangu ya kupenda kukimbilia mlimani kilamara kupanda mawe na majabari ya Mwanza.

asante sana mkulu ila hapa umeongopa supu ya mawe ni gongo ama ile konyagi mwitu if you know what it means.

In between Captain Haddock kwa wale waliowahi kusoma vitabu vya Tintin adventures watajua kuwa ni mtu mmoja ambaye hapendi ujinga ujinga. Ukileta za kuleta anakuporomeshea matusi kama hana akili mzuri. kitu kingine anapenda pombe kali which best descibes me. Lakini kitu muhimu kuliko vyote pale ambapo inaonyesha mtaalam Tintin kaishiwa Captain ndio huokoa jahazi.
In short I sivumilii ujinga na kama isingekuwa sheria za JF ningekuw nawaporomoshea matu wale wote wanaotufanya mizuka
 
Isha Lubuva kwa Kirangi inamaanisha Mwana wa Lubuva kama Wamasai wanavyoitwa Ole Saitoti, Ole Mollel, Ole Lokoine au Waarabu wanavyoitwa El Faid n.k. Aidha unaweza kutumia mkato na kuita Sha Lubuva. Mimi ni mtoto wa Mzee Lubuva. Lubuva inamaanisha mabua yanayobakia shamba baada ya kuvuna na marehem Bibi yetu alipatwa na uchungu na kumzaa Mzee lubuva kwenye (mabua) shamba ambalo tayari lilishavunwa ndipo akaitwa Lubuva. Ingekuwa alizaliwa nyakati za leo angekuwa na aka yake ya LbV
 
Sipo = hili nililipata wakati nipo Sekondari na hata nilipokuwa UDSM liliendelezwa na washikaji zangu kutokana na tabia yangu ya kuruka matukio pale yanapokuwa magumu kwa kukanusha tu kuwa mie sikuwepo bwana wakati ili linatokea.

a.k.a alibi
 
Back
Top Bottom