BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
- Thread starter
- #281
hA-HA-HA BAK!...Kisa cha kuitwa binti maringo...yaani hata OPP hajakosea kabisa ni kwa sababu ya miondoko yangu na jinsi ninavyongea plus mapozi!....hahaha kwenye kula kama nipo na men ndiyo naweka mapozi ila kama nipo alone napakia bila mapozi aisee!....
Mhhh! naona miondoko yako itakuwa inafanana fanana na ile ya Naomi Campbell au Tyra Banks ambayo inawapagawisha sana njemba wengi. Nilicheka sana siku moja nadhani hapa jamvini dada mmoja aliandika kwamba mumewe anampandishia sana eti anatembea kishamba maana Mumewe anataka atembee kama Naomi Campbell...mhhhhh! Njemba nyingine zina makuu kweli kweli! ukakasirike na kuja juu eti kisa mkeo hatembei kama Naomi Campbell! Hizi ndoa zina matatizo ya kila aina.
Naona kwenye msosi ukiwa mwenyewe wala hujivungi, maringo yote unaweka pembeni na kufukia kama kazi ha ha ha ha ha ha 🙂 Ahsante sana kwa kujibu Binti Maringo.