Je, kama wanaume watapewa wanawake wapya na mabikra wapya Mbinguni, sisi wanawake wa Duniani tutapelekwa wapi?

Je, kama wanaume watapewa wanawake wapya na mabikra wapya Mbinguni, sisi wanawake wa Duniani tutapelekwa wapi?

Mabikra 72 kwa mwanaume mmoja???
Hii ni zinaa ya namna gani????
Hapo mzee unakua chombo cha starehe period..
Huko peponi kazi ni moja tu,ufuska mwanzo mwisho..
Wanawake 72 sio mchezo,itakua ni ngono siku zote za maisha yako.
Simple tu mtu duniani unaishi 75yrs na unakua umedate na mademu zaidi ya 20 sasa itashindikana vp kwa maisha ya milele kua mabinti 72?,Kwanza naona M/Mungu katupunja maisha ya milele at least mademu 500
 
Muanzisha uzi naomba nikujibu kwa kifupi sana naamini utaelewa.
Ni hivi,kwanza lazima uelewe kwamba Mungu alianza kumuumba mwanaume kwanza then kutokana na huy hyo mawanaume ndo mwanamke akafuatia.

Lakini baada ya uumbaji huo mwanaume ndyo mtu pekee aliyesimikwa uongozi/ukubwa ili kumuongoza/kumtawala mwanamke,sasa basi hapa Duniani wewe mwanaume umeoa mwanamke na mmeishi maisha ya hapa Duniani kwa kufuata sheria za Mungu na kufanya ibada vzr mpk Mwenyezi Mungu akawaridhia muwe katika watu wa peponi.

Sasa kule peponi kwa vile wewe mwanaume unastahili wanawake wengi(Hawa 72 ni idadi ya mfanya ibada wa kiwango cha chini sana) wanawke ambao atawamiliki kwenye eneo utakalopewa ndani ya pepo ambalo ni kama nchi yako ya pekeako na makasri/majumba mengi yaliyobeba hao wanawake pamoja na WAFANYAKAZI wafanyakazi ambao ni vijana wadogo na ni maalum kwa ajili ya kukutumikia wewe katika maisha ya huko peponi.
Ukumbuke kwamba maisha ya peponi ni jambo la milele na hii ni sababu nyingne kwann unapewa wake wengi ili usichoke na usikinahi....lakini pia kule peponi wewe hutakuwa wa kawaida,Mungu atakuumba upya na huyu mke wako ataumbwa upya isipokuwa sasa huyu mwanamke kwa vile alipitia mapambano ya ibada basi Mungu kwa uwezo wake atamfanya kuwa mwanamke MZURI ZAIDI ya wale wanawake mahur'layn na hao mahur'lain ni wanawake WAZURI kiasi ambacho kwa hapa Duniani hakuna cha kufananisha,sasa huyu mwanamke aliyetoka Duniani anapewa ubora huo wa UZURI, UTUKUFU na CHAGUO MAALUM kwasababu yeye kuna kazi ya ibada aliifanya kule Duniani na sasa huku anapewa tunu maalum kma tusema UMALKIA hv japo idadi hyo pamoja na ya wanawake wale wengine itakuwa chini yako wewe mfalme uwamiliki.

Kule peponi Kuna NGUVU maalum Mungu atakupatia wewe mwanaume ili uweze kuwatosheleza idadi yote ya wanawake utakayopewa na kila mwanamke unakaemiliki kule Mungu muumbaji atawatoharisha/Atawasafisha kwa maana hawatapata ile period zao za kila mwezi na hawatapata ujauzito,hawaendi haja ndogo wala kubwa na kubwa zaidi Mungu atawatoa watu wote CHUKI,FITNA,WIVU na UHASIDI katika nyoyo za watu wote watakaoingia peponi ikiwemo hao wanawake jambo ambalo pia
hawa wanawake watakaokuwa katika milki yako pia watakuwa WANAPENDANA SANA WAO KWA WAO na WATAKUWA WANAENJOY SANA KUKUHUDUMIA WEWE...Mungu atawaumba upya.

Sasa wale mnaosema kwamba pepo itakuwa uwanja wa ufuska...Ni hv ndg zangu,Mwanaume yeyote aliyekamilika Starehe yake kubwa ya kwanza ni Ngono tena ngono si kwa mwanamke mmoja,yan mwanaume aliyekamilika huwa anapenda pia kuwabadili badili hao wanawake,na hii ni NATURE,hata hapa Duniani hakuna Mwanaume anaridhika na mwabamke mmoja huo ndo ukweli,sasa kama wewe ni mwabaume afu unakasirika kuwa na wanawake wengi basi kaa ukijua utakuwa unashida kidogo ya kimaumbile japo ukienda peponi Mungu atakuumba upya(usijali)
Sasa kwa vile Mungu muumbaji anatujua vema ndo akaamua kutuumbia idadi kubwa ya wanawake wakiwa wanatofautiana UZURI NA UREMBO huko peponi.

Lakini pia mbali na hilo la ngono,Huko peponi Mungu ameandaa mito ya maji,mito ya maziwa,mito ya POMBE kwa watakaopenda kuinywa lakini pombe hyo huwezi kutoka akili ukaongea upuuzi kwa sababu peponi hakuna upuuzi,lakini pia kuna matunda, nyama za ndege na starehe mbali mbali zisizokatika.

Wanaosema peponi kwa ajili ya kuimba imba.....jamani hivi kma peponi ndo kuimba imba tu kila siku sasa raha ya hiyo pepo ipo wapi?
Pepo ni ulimwengu Mungu ameandaa watu wema kwenda kustarehe,kule hakuna tena ibada,ibada unatakiwa ufanye hapa sasahv Duniani,hayo mambo ya kuimba kule hakuna msiwakatishe watu tamaa,kule Mungu ataki umuimbie kule anataka wewe ule bata haswa,uenjoy utukufu wake kwa vile alivyokuandalia...Yan ukae unaimba imba afu ukishamaliza kuimba...yan hakuna kula,hakuna kunywa yan ni kuimba tuuu....jaman huo sio mpango wa Mungu,hyo ni mipango ya watu kuwakatisha tamaa ili uhisi kwamba nikifanya wema inamaana naenda kulipwa KUIMBA? hii hapana.
Pepo ni ulimwengu wa starehe,wewe kama akili yako haitaki hulazimishwi,lile jambo la kiimani na ndomaana watakaotunukiwa hyo pepo NI WALE WALIOAMINI.

Fanya sana ibada hapa sasahv,piga swala 5,funga Ramadhani,nenda mecca kama una uwezo lakini pia acha madhambi yote uliyokatazwa na tenda mema yote uliyoamrishwa...UKIFA TU PEPONI,na kwa taarifa tu ni kwamba zile starehe za mwanzo huwa zinaanzia pale kaburini then kule peponi utakabidhiwa starehe iliyokamilika
Na ndio mana hapa duniani mtu anaeishi maisha mazuri utasikia watu wanasema jamaa anaishi kama peponi,why wasiseme kwa mtu anaeimba imba anaishi kama peponi?

Peponi ni bata batani halina mfano shekhe ushahenya na ibada duniani unaenda kula pension yako,yani uhenye duniani kwa maibada kibao peponi ukapayuke kuimba tena ahaaaaa


Achana na hiyo kitu firdaus ni VVIP tujipinde shekhe
 
Simple tu mtu duniani unaishi 75yrs na unakua umedate na mademu zaidi ya 20 sasa itashindikana vp kwa maisha ya milele kua mabinti 72?,Kwanza naona M/Mungu katupunja maisha ya milele at least mademu 500
Zinaa ni zinaa,
Kwanini tunazuiwa duniani tukaruhusiwe peponi?
Think
 
Allah hayupo. Mbingu haipo.

Hizo ni tamaa za wanaume tu zinatumiwa katika hadithi ya kuwanasa kama ulimbo.

Saikolojia ndogo tu ya kuwanasa wanaume.
 
Hiyo dini ni ya kumlinda mwanaume ni mfumo dume angalia tu kule uislam ulikoanzia wanawake wanavyotendewa, hawaruhusiwa kusoma, kuwa viongozi, kumiliki mali, hata kuendesha gari. Uislam unamkandamiza mwanamke mpaka mwisho ingawa wanawake nao ni tatizo kubwa wakiachiwa wafanye wanavyotaka mfano angalia nchi za wazungu
Huujui uislamù na ubaya zaidi unafkiri waarabu ndo waislamu wa kweli. Anyway sio kosa lako
 
Hakuna mbingu, hakuna Mungu.

Hizo zote kamba za watu na siasa zao tu.

Mkuu si mchezo ,unaweza ukawa ushalijibu hili swali siyo mbaya ukarudia kwa faida ya wengi,kama hakuna Mungu je binadamu alitoka wapi? Maana tunaambiwa binadamu aliumbwa na Mungu.

Mkuu nataka kujua tu unaweza ukatujibu simple tu.
 
Swali zuri sana, pengine majibu yatapatikana, yawezekana wanawake hamuendi peponi ndio maana hakuna mlichoambiwa

As-salamu alaykum ndugu zangu.

Naomba kuuliza, Quran tukufu 2:25, 4:57 imeandika kwamba wanaume watapewa wanawake wapya na mabikra wazuri huko Akhera.

Pia ukisoma Quran tukufu 38:52 inaongelea kwamba kuna mabikra tayari wa kutosha huko Ahera wakiwasubiri wanaume.

Zaidi ukisoma Quran tukufu 44:54 inataja sifa za mabikra hao kuwa ni wenye macho mazuri, macho meusi mapana na warembo kwelikweli.

Swali langu ni iwapo wanaume wetu na waume zetu watapewa wanawake wapya na wanawake hao wako tayari walishaandaliwa, sisi wanawake wa Duniani tutapelekwa wapi iwapo waume zetu wa hapa Duniani tayari watapewa wanawake wengine?

Hakuna mahala popte kwenye Quran tukufu ambako sisi wanawake wa Duniani tumeahidiwa chochote huku waume zetu wakiahidiwa wanawake wapya.

Ahsante.
Qur-an 40;8 inakupatia mwangaza
Waislamu tutaingia na wake zetu peponi,ikiwa hawo wanawake watakuwa wema.
Lakini Hao wake zetu watakuwa Malkia, na Hao mahurl Ain ni kama wasaidizi wa malkia.
Jumla ni 70.
Huko ni kula na kupiga Rungu ndiyo mfano rahisi wa maisha ya Peponi.

Kwani hapa duniani tunahangaika kufanya kazi ili tupate nini?
si niKula,
Starehe,
Na kupiga rungu?
kuna jengine katika starehe unazozijua wewe hapa duniani?

Basi peponi kuna Suprize, Hakuna aliye wahi hata ku imagine.
 
Mkuu si mchezo ,unaweza ukawa ushalijibu hili swali siyo mbaya ukarudia kwa faida ya wengi,kama hakuna Mungu je binadamu alitoka wapi? Maana tunaambiwa binadamu aliumbwa na Mungu.

Mkuu nataka kujua tu unaweza ukatujibu simple tu.
Kwanza jina "binadamu" si jina sahihi, kwa sababu linatokana na hadithi ya kwamba mtu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na sisi wote tumetoka kwake, hiyo habari ni ya uongo.

Kwa mujibu wa sayansi ya sasa, ushahidi wote unaonesha kuwa watu wamepata kuwa a species kutokana na evolution by natural selection, si kwa kumbwa na Mungu.
 
Back
Top Bottom