Je, Kamera ya Simu inaweza kuizidi Kamera ya kawaida kwenye ubora wa Picha?

Je, Kamera ya Simu inaweza kuizidi Kamera ya kawaida kwenye ubora wa Picha?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
15,126
Reaction score
35,515
Habari wakuu,

Kuna uwezekano Picha zinazopigwa na Smartphone hizi za kisasa zikaizidi kiwango kamera ya kawaida? (Sio professional camera)
Nimeuliza kwa sababu simu hasa hizi High end zinakuja na maboresho sana upande wa Kamera huku zikiongezwa lenzi,zooming na Megapixels na idadi ya camera.

Nauliza sababu nimewahi kumiliki Kamera ya Sony DSC-90(nimeweka picha pale chini)
Picha nilizokuwa napiga zilikuwa nzuri sana kushinda picha za Samsung S9,na hata nikiangalia picha za kamera zilikuwa na Mb nyingi zaidi kianzia 5-8 wakati zile za S9 zilikua 1-2.
IMG_20250914_212743.jpg

Je kwa sasa kuna Simu inaweza kuipita kamera ya kawaida kwa ubora wa picha?
2-3---evan-blass.jpeg

Naomba wataalamu na mambo haya mnisadie.

Ahsante.
images.jpeg
 
Sio mtaalamu sana wa Cameras mimi ila nina kaufahamu kidogo kwa sababu nina cameras.

Simu nyingi zinachakata picha automatically mfano una iphone 14 ukipiga picha ina portrait ina blur na kuboresha skin tone kwa sekunde same to samsung na simu zingine.

Lakini kwa camera itapiga picha kali sana bila kuongeza hivyo vitu automatically ila end result yake ni umeme ikishachakatwa
 
Mimi nimwewahi kuwa na samsung s10e ilikuwa na 16mp lkn ilikuwa inazizidi mbali sana tecno zenye 50mp

Mp sio kigezo cha ubora mkuu
Sasa S10 unaifananisha na Tecno?
Hapo ni flagship phone na mid-range phone, pia usisahau iyo picha moja ukiingalia kwenye S9 haitakuwa namwonekano sawa na Tecno kwaiyoo ubora wa display nao utahusika.
Ukipata muda jifunze kuhusu pixcel.
 
Camera ya simu hata iwe latest kama iPhone 17,ubora wa picha hauwezi kua sawa na camera,advantage kubwa ya camera ni sensor na lens..

Kwenye simu picha inaonekana nzuri kuzidi camera sababu ya software za ku enhance ubora wa picha kwenye simu,hivyo vinafanya ubora wa picha kupungua,

Jiulize swali dogo,why camera ya kawaida tu,ambayo kazi yake kupiga picha tu,inauzwa laki 7 but simu Ina dou simcard, internet 5G, OLED screen, calculator,inauzwa laki Tano??..
 
Hapana malengo ya simu si picha lakini malengo ya camera ni picha lakin ubora wa pcha unategrmea na kifaa chenyewe unaweza ukapinga megapixel za kamera ya simu na camera ya kawaida zikiwa sawa ikowapi itatoa picha kali jibu ni camera wala si simu
 
Sio mtaalamu sana wa Cameras mimi ila nina kaufahamu kidogo kwa sababu nina cameras.

Simu nyingi zinachakata picha automatically mfano una iphone 14 ukipiga picha ina portrait ina blur na kuboresha skin tone kwa sekunde same to samsung na simu zingine.

Lakini kwa camera itapiga picha kali sana bila kuongeza hivyo vitu automatically ila end result yake ni umeme ikishachakatwa
Ni kweli na ukitaka kuona ubora picha ya kamera weka kwenye computer halafu zoom
 
Back
Top Bottom