Point and shoot kama jina lilivyo ni zile camera za kawaida ambazo ukiona kitu unapoint camera yako na ku bonyeza button ya kupiga picha na kupiga picha. Hubadili lens, hakuna settings nyingi za ku seti na mambo mengi kama proffesional camera za Dslr na Mirrorless.
Jina jengine wanaita compact camera na utofauti wa muonekano ni kama huu
View attachment 3476020
Kuhusu kwenye uzi wako simu kutoa picha za mb ndogo na camera mb nyingi, most of time default setting za simu hazitumii uwezo wa camera yako 100%, mfano kama hizi S series ultra zenye 200mp ukisema utumie sensor yote file moja la picha ni zaidi ya mb100, ila ukipiga picha za mb 100 ina maana fasta tu simu itajaa hivyo by default wanakuwekea output kama mp12 ama chini ya hapo. Pia simu zina compression, kuna format kama Heif zina compress picha.
Simu zina advantage kadhaa over Compact camera kama
1. Computational photography.
Simu zinakuja na processor zenye nguvu, simu za kisasa hizi zina nguvu kushinda hata desktop zote unazozikuta Agrey pale, ndani ya hizi processor (soc) kuna kitu kinaitwa Isp ambacho kinaruhusu tricks nyingi kufanyika ili kupata picha bora hata kama hardware husika ya camera sio bora.
Chukulia mfano Google pixel, Camera zao (hardware) ni za kiboya sana, wanatumia camera outdated, ndogo ambazo in reality zingewekwa kwenye compact camera picha zisingekua nzuri, ila sababu ya computational photography output ya picha inakua nzuri mno.
Mfano wa hizo trick ni kama
- kupiga picha nyingi na kuziunganisha ili upate picha moja kali, unapopiga picha kwenye simu na sensor yako ya 200mp not necessary simu ikatumia sensor yote kupiga picha moja, bali inaweza piga picha tofauti na kubin zile pixel ili upate picha moja yenye quality kubwa, so unakuta sensor ni 200mp ila picha inatoka 50mp mfano wa hizo binning ni kama Pureview alioyokuwa anatumia Nokia ama Quadbayer hii ambayo inatumika simu nyingi za sasa
Marketing departments are trying to sell you on the wrong thing - resolution isn't why these sensors are good, it's the better image processing.
m.gsmarena.com
-Algorithm
Hii ni interpretation ya data toka kwenye hardware ya camera mpaka output unavyoona, simu zina Algorithm ambayo ni advanced sana, not necessarily ipo accurate ila wanai tune software kutoa picha ambazo zinavutia kwenye macho, hapa ndio unakuta camera nyengine kila mtu anaepiga picha ni mzuri,
2. Hardware
-Sensor
Sio camera zote za simu zinategemea computational photography, baadhi wanaweka hardware za maana ambazo zinapita hata camera za kawaida, mfano simu kama Sharp Aquous kuanzia R6 zina sensor yenye ukubwa wa nchi karibia moja ambayo imepita camera za kawaida na ni almost Dslr level, zipo pia kama Xiaomi ultra Series, Huawei P series, Vivo X series etc wanaweka hizi hardware.
Hii list ya hizo simu kama upo interested
en.m.wikipedia.org
-lens
Simu siku hizi zinakuja na multiple lens, kuna kuwa na Main lens ya kawaida kupiga picha, kuna telephoto ya kuzoom, ultra wide ya kupiga picha pana, Macro ya kupiga vitu vidogo etc, ukiwa na Dslr unaweza kuwa na multiple lens pia ila kwa camera ya kawaida most of time ni fixed.
-stabilization
Hii ipo kote kote kwenye hardware (OIS) na software (EIS) ambapo inasaidia kutoa picha nzuri kwenye mitikisiko, kwenye Video inasaidia mno, ndio maana unaona Video zinazorekodiwa na simu ni much better kuliko hata camera za kawaida. Kwenye professional camera wanatumia vifaa maalum kama tripod zile kupata stabilization ila compact nadra mtu kutumia na tripod hivyo unakuta stabilization ya simu kusaidia kwenye hii situation.
Yapo mambo mengi mno wengine wataongezea.