Je, Kanisa Katoliki hawachanganyi dini na siasa? Au wao ni untouchable!

Je, Kanisa Katoliki hawachanganyi dini na siasa? Au wao ni untouchable!

siasa na dini ni nyanja mbili tofauti, lakini haziko mbali kama watu wanavyodhani. Kiongozi wa dini ni sehemu ya jamii na ana wajibu wa kuwaongoza waumini siyo tu kiroho bali pia kuwasaidia kuelewa mambo ya kijamii ikiwa ni pamoja na siasa.

Hata hivyo, jambo la msingi ni namna gani anazungumzia siasa, kama anapanda chuki, upendeleo au kugeuza madhabahu kuwa jukwaa la kampeni, hapo ndipo tatizo linapotokea. Lakini kama anazungumzia masuala ya haki, amani, maadili ya viongozi, au kuwahimiza waumini kushiriki uchaguzi kwa hekima, hiyo sio kuchanganya dini na siasa, bali ni kutimiza wajibu wa uongozi wa kiroho katika jamii ya kidemokrasia.
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Hakika umeeleweka
 
Issue kubwa kwanini watumie madhabahu kuongelea siasa? Huoni wanachanganya DINI na SIASA? Issue sio kufanya ibada Kila siku au Kila jumapili
IMG_1566.jpeg
IMG_1504.jpeg

Muasisi wa kuchanganya dini na siasa ni CCM, tatizo la CCM viongozi wa kidini ambao ni chawa wao wanaona ni sawa kwao kuchanganya dini na siasa lakini pale kiongozi wa kidini anapokuwa na mitazamo tofauti na ya kwao au anapotaka wajirekebishe pale wanapokosea hiyo wanaona si sahihi na wanaweza hata kumteka na kumtesa kiongozi huyo.
 
kanisa katoliki wana utaratibu wa agenda za misa za kila siku na kila jumapili tofauti na gwajima atakurupuka na jambo la uaraiani au kwenye majukwaa ya kisisa na ndio hilo hilo likawa agenda ya ibada yake kanisani :pulpTRAVOLTA:
Hoja yako haina vigezo kama maksi unapata 0.05%
Pamoja na kuwa na agenda katoliki wa muda maalum wa matangazo kwa waumini. Vivyo hivyo kwa makanisa yote likiwepo la Gwaji boy.
 
Amani iwe nanyi waungwana wa jukwaa hili pendwa kabisa!

Moja kwa Moja niende kwenye mada au swali langu kwenu wakuu, kufuatia press iliyofanywa na mbunge wa kawe na kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima Hon.Dr.Bishop Josephat Gwajima kuhusu Hali ya kisiasa nchini imepelekea kufutwa kwa kanisa lake, Huwa tunashuhudia nyaraka kutoka TEC zinazozungumzia na kuhoji mambo kama hayahaya je kwanini na wao wasifutiwe usajili wao kama walivyofanya haraka sana kwa kanisa la ufufuo na uzima.?

Uzi tayari.
Catholic Church ni kubwa na lina nguvu zaidi ya serikali, chama tawala pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama(wasiojulikana).
 
Katoliki ni taasisi inayojitambua, haifanyi shughuli za kiibada pekee. ina wanadiplomasia mahiri, inajua iseme nini wakati gani na kwanini. Mfano saizi iko kimya inajaribu kupima upepo. Gwajima kumhusisha Rais na utekaji kwa moja kwa moja hivyo alipitoka kidogo. Jamaa wakiamua hatoboi nashangaa walokuwa wakimsifia....kana kwamba yeye ni noma sana kuzidi hat Rais.. nadhani nguvu ya Rais hatuijui...

Mara zote amekuwa akijitahidi kukwepa direct confrotation na Rais, anadeal na kina Bashite nk... awamu ya 5 alisoma upepo akaunga juhudi, sasa awamu hii nadhani alijisahau kidogo. Alimchukulia poa mkubwa (wahenga walisema ndege mjanja hunaswa na tundu bovu - na ni kama amenasa)... cheki kina Manji nk waliyopitia.... nashangaa hata kumhusisha Rais na utekaji wakati ana platforms million kibao ya kudeal na watu akitaka... utakatishaji, madawa ya kulevya (refer manji et al) , ukwepaji kodi, uhujumu uchumi, kufungia vyanzo vya uchumi (refer billicanas)., wanaweza wakasema wewe sio Raia (refer katibu wa TEC kabla ya Kitima) nk nk
Mimi siko hapa kumtetea Gwajima au serikali ila nina Swali vita ya serikali na Gwajima ni dhidi ya nini Serikali inapigania nini? Tuombe Mungu awape busara na Hekima viongozi wote wanaogoza watu
 
siasa na dini ni nyanja mbili tofauti, lakini haziko mbali kama watu wanavyodhani. Kiongozi wa dini ni sehemu ya jamii na ana wajibu wa kuwaongoza waumini siyo tu kiroho bali pia kuwasaidia kuelewa mambo ya kijamii ikiwa ni pamoja na siasa.

Hata hivyo, jambo la msingi ni namna gani anazungumzia siasa, kama anapanda chuki, upendeleo au kugeuza madhabahu kuwa jukwaa la kampeni, hapo ndipo tatizo linapotokea. Lakini kama anazungumzia masuala ya haki, amani, maadili ya viongozi, au kuwahimiza waumini kushiriki uchaguzi kwa hekima, hiyo sio kuchanganya dini na siasa, bali ni kutimiza wajibu wa uongozi wa kiroho katika jamii ya kidemokrasia.
Siasa na dini nafikiri imetangulia Dini then Siasa kigine waumini wa dini ndo walewale wapo kwenye siasa alafu Siasa ni maisha ya kila siku japokua mimi sio mpenzi wa siasa tena za Afrika
 
Mimi siko hapa kumtetea Gwajima au serikali ila nina Swali vita ya serikali na Gwajima ni dhidi ya nini Serikali inapigania nini? Tuombe Mungu awape busara na Hekima viongozi wote wanaogoza watu
Ni kweli kaka, hata hivyo Gwajima alisema Rais ndio ana hilo kundi la utekaji.. that was wrong na ni character assasination. Hata vyombo vya usalama havitakubali.. alichagua vita isiyo na maana.
 
Press ya gwajiboy ni safi, wenye mamlaka walipata shida mwendelezo wake, kwani alikuwa anawachana wanaomshutumu press yake!
 
Amani iwe nanyi waungwana wa jukwaa hili pendwa kabisa!

Moja kwa Moja niende kwenye mada au swali langu kwenu wakuu, kufuatia press iliyofanywa na mbunge wa kawe na kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima Hon.Dr.Bishop Josephat Gwajima kuhusu Hali ya kisiasa nchini imepelekea kufutwa kwa kanisa lake, Huwa tunashuhudia nyaraka kutoka TEC zinazozungumzia na kuhoji mambo kama hayahaya je kwanini na wao wasifutiwe usajili wao kama walivyofanya haraka sana kwa kanisa la ufufuo na uzima.?

Uzi tayari.
Gwajima ni mkuu wa Kanisa duniani lenye makao makuu Tanzania
Ulishamsikia Papa wa katoliki akifanya siasa?
Hayo matamko ya katoliki huwa si ya papa ni ya baadhi ya viongozi .Hivyo si msimamo wa kanisa.Hivyo huwezi futa
 
Ni kweli kaka, hata hivyo Gwajima alisema Rais ndio ana hilo kundi la utekaji.. that was wrong na ni character assasination. Hata vyombo vya usalama havitakubali.. alichagua vita isiyo na maana.
Gwajima ni mtovu wa nidhamu pia huyu mwingine hana Hekima kama kweli huna ilo kundi kwa nini utumie nguvu ya kumshambulia mtu aliyesema una kundi kufanya hivo uoni unatuaminisha kwamba ni kweli. huyu wa pili alitakiwa atumie Hekima
 
Issue kubwa kwanini watumie madhabahu kuongelea siasa? Huoni wanachanganya DINI na SIASA? Issue sio kufanya ibada Kila siku au Kila jumapili
Hivi siasa ni nini? ......kukemea watu kupotezwa,kuuwawa na kunyanyasa wananchi ni kupiga siasa. .......basi kama kukemia ni siasa basi hazitufai TZ hizi siasa
 
Nakubaliana na wewe mkuu 100% (Catholics wanachanganya DINI na SIASA na wao wanastahili kupitia alichopitia gwajiboy)
Sijamwona mwanadamu wa kulifuta kanisa katoliki bado hajazaliwa,wafalme na wafalme walilitikisa lakini likaendelea kusonga mbele.
 
Amani iwe nanyi waungwana wa jukwaa hili pendwa kabisa!

Moja kwa Moja niende kwenye mada au swali langu kwenu wakuu, kufuatia press iliyofanywa na mbunge wa Kawe na kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima Hon.Dr.Bishop Josephat Gwajima kuhusu Hali ya kisiasa nchini imepelekea kufutwa kwa kanisa lake, Huwa tunashuhudia nyaraka kutoka TEC zinazozungumzia na kuhoji mambo kama hayahaya je kwanini na wao wasifutiwe usajili wao kama walivyofanya haraka sana kwa kanisa la Ufufuo na Uzima.?

Uzi tayari.
Huwa hawatoi matamko ya kindezi kama kina Gwajiboy na makanisa Yao ya mfukoni na uchochoro

View: https://www.instagram.com/p/DKbjHx7tiaa/?igsh=MWR3OXN2aWZ4MHFrMQ==

Nao wakivuka mstari watakumbushwa kwamba wanaoeqa siko
 
Back
Top Bottom