Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

NAWAPA MSISITIZO.
YESU ALITOA ONYO SANA KWA WATU WANAOFUATA MAFUNDISHO YA WANADAMU.

8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mathayo 15:9

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ufunuo wa Yohana 12:17

KAMA HUFUATI SHERIA ZA MUNGU MBINGU UTAISIKIA TU.
 
UUMBAJI WA MUNGU NA SABATO.

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Mwanzo 2:3

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Kutoka 20:8

9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
Kutoka 20:9

10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Kutoka 20:10

11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Kutoka 20:11

YESU KUFUNDISHA SIKU YA SABATO

Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
Marko 1:21

Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Marko 6:2

Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Luka 4:16

Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;
Luka 4:31

Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.
Luka 6:6

Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.
Luka 13:10
 
TUANZIE HAPA...

Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita." (Ufunuo13:17,18)

[emoji3591]Mambo mawili makuu sana ya mamlaka hii ya Mnyama yanafunuliwa katika Ufunuo
13. "Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio
huru kwa watumwa, watiwe CHAPA [ALAMA] katika mkono wao wa kuume, au
katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala
kuuza, isipokuwa ana chapa [alama] ile, yaani, jina la Mnyama yule, au hesabu ya
jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya
Mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na
sita." Ufunuo 13:16-18.

Kwa mujibu wa Ufunuo 13:17, hesabu ya jina lake itakuwa pia ni hesabu ya
mwanadamu.

[emoji3591] Bila shaka inamhusu mtu yule anayeiongoza mamlaka ile ya Mnyama.
Njia ya zamani ya kuipata hesabu ya jina ni kuchukua thamani ya tarakimu za herufi zote na kuzijumlisha ili kupata jumla yake. Kama tunataka kutumia kipimo hicho kwa Upapa, yatupasa kupata jina la kiofisi [cheo] la Papa, ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo.

[emoji3591] Kama hiyo ni hesabu ya mtu, basi, bila shaka ingekuwa ni ya mtu yule
anayeuongoza mfumo ule [wa dini].
Ni jambo la kuvutia macho kuona kwamba kuna cheo rasmi cha Kilatini cha Papa, cheo ambacho amepewa na Kanisa lenyewe. Cheo hicho kinaonekana tena na tena
katika vitabu vya Kanisa la Roma. Lakini katika gazeti la kila juma la Kikatoliki liitwalo, OUR SUNDAY VISITOR, la Aprili, 1915, tunao usemi wa kuvutia
unaosema kwamba herufi ya cheo hicho rasmi zimeandikwa katika kofia yake ya Kiaskofu (miter or mitre).

[emoji1542] Hapa ni dondoo lenyewe: "Herufi zilizoandikwa katika kofia ya Papa ni hizi; VICARIUS FILII DEI, ambacho ni Kilatini cha 'ALIYE BADALA YA MWANA WA MUNGU' (VICAR OF THE SON OF GOD).

[emoji3591]Wakatoliki wanashikilia [wanaamini] kwamba Kanisa ambalo ni jamii inayoonekana
ni lazima liwe na kichwa kinachoonekana; Kristo kabla ya kupaa kwake kwenda
mbinguni, alimchagua Mtakatifu Petro kuwa kama Mwakilishi wake. Kwa hiyo,
Askofu wa Rumi kama kichwa cha Kanisa, alipewa cheo cha 'Aliye Badala ya Kristo'
(Vicar of Christ)." Kwa siku hizi kofia ya papa [tiara] haina cheo chake cha Kilatini,
lakini maneno hayo yanatumika katika sherehe za kumtawaza kila Papa mpya anayevikwa taji [kofia hiyo]. Basi, tukiwa na cheo hiki rasmi cha Papa mkononi mwetu, tunaweza kuendelea kutumia kipimo hiki cha Maandiko haya.

[emoji1542]Tunaipataje hesabu ya jina lake? Kwa kupata thamani ya tarakimu za Kirumi za cheo chake cha VICARIUS FILII DEI, tunaifikia hasa hesabu hiyo halisi, 666.

[emoji1542]Angalia jinsi hesabu hizo zilivyofanywa hapa
chini, kila herufi ikipewa thamani ya tarakimu yake:
[emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]

V ................. 5 F ..................0 D ............. 500
I................... 1 I ...................1 E.................. 0
C ............. 100 L ...............50 I....................1
A ................. 0 I ...................1 501
R ................. 0 I....................1
I .................. 1 53
U au V......... 5
S ...................0
112
112 + 53 + 501 = 666

[emoji1542]Mmoja anaweza kubisha kwamba hilo linaweza kuwa ni jambo linaloweza kutokea
kwa nasibu. Tunakubali ya kwamba upo uwezekano kwa jambo kama hilo kutokea kwa nasibu tu, kama tungekuwa na pointi moja hiyo tu ya utambulisho ya
kuitegemea. Lakini, basi, ukweli ni kwamba, hiyo ni pointi ya KUMI miongoni mwa orodha ndefu ya ishara za tabia yake ambazo Biblia huzitumia kuitambulisha mamlaka hiyo ya Mnyama.

[emoji3591]Hii inaongezea tu uzito na nguvu kwa yale ambayo tayari
yamekwisha kusemwa kwa kuzitumia [ishara zile] kuionyesha mamlaka hiyo ya Papa.
Ni uthibitisho wa kilele pamoja na zile ishara nyingine zote zilizowekwa kwa wazi sana katika Maandiko.

[emoji3591]Alama Hii ----- Ni Udanganyifu Mkuu
Sasa tuko tayari kuchukua hitimisho la kilele cha udanganyifu huu kwa kadiri
mamlaka hiyo ya Mnyama huyo inavyohusika.

[emoji3591]Tayari tumekwisha jifunza ya kwamba
mamlaka hii ingeweka mafundisho mengi ya uongo kinyume na mafundisho makuu ya kweli zake Mungu. Kwamba [mamlaka hiyo] ilikuwa ni mchanganyiko wa mawazo ya kipagani na mafundisho ya dini ya Kikristo ambayo yamekusanywa pamoja kwa hali inayoleta machafuko [kuchanganyikiwa], yanayoitwa vyema kama
"BABELI" katika Maandiko.

[emoji1542]Mafundisho machache ya uongo yanaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo: badala ya
Neno la Mungu, imeweka MAPOKEO; badala ya Roho Mtakatifu, imemweka PAPA;
badala ya toleo moja tu la Kristo, imeweka MISA [toleo la kila siku]; badala ya
ubatizo, imeweka KUNYUNYIZA; badala ya Meza ya Bwana, imeweka MKATE
UNAOBADILIKA KABISA NA KUWA MWILI NA DAMU HALISI YA YESU
(Transubstantiation); badala ya Sheria ya milele ya Mungu, imeweka SHERIA
ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO [Amri Kumi]; badala ya Zaka; imeweka KODI
[Ushuru] na INDULGENSIA [kuuza vyeti vya msamaha wa dhambi]; badala ya
mauti, imeweka MAHALI PA KUTAKASIA DHAMBI au TOHARANI (Purgatory);
badala ya Muhuri wa Mungu, imeweka ALAMA [CHAPA] YA MNYAMA.

[emoji1542][emoji1484]Hapa tunashughulika hasa na ALAMA YA MNYAMA. Katika Ufunuo 14:9,10
tunasoma hivi, "Mtu awaye yote akimsujudu huyo Mnyama na Sanamu yake, na
kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye
atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo
kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake."

[emoji3591]Hili ni jambo la KUFA NA KUPONA. Ni lazima tujue kabisa alama hii ni ya kitu gani hasa na jinsi tunavyoweza
kuikwepa.
Kwanza tunaona katika Biblia ya kwamba ALAMA hii daima iko kinyume na
MUHURI WA MUNGU. Katika Ufunuo 7:2,3, tunajifunza ya kwamba Muhuri wa
Mungu unawekwa juu ya kipaji cha uso sawasawa tu na ile Alama ya Mnyama
inavyowekwa juu ya vipaji vya uso. Vitu hivyo viwili [Muhuri wa Mungu na Alama
ya Mnyama] vinaonekana kuhitilafiana moja kwa moja na kila kimoja kiko kinyume
na kile kingine. Vyote viwili vinapokewa katika kipaji cha uso na mkononi. *_>>>

NITAENDELEA (Nasumbuliwa kidogo na tonsils)
pole; nasubiri.>.
 
Yesu alikuwa na kawaida ya kufanya ibada siku ya Sabato

Je huu ulikuwa mwaka 1863

Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; NA SIKU YA SABATO AKAINGIA KATIKA SINAGOGI KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE, akasimama ili asome.
Ndio lakini akiwa MYAHUDI na sio MSABATO.. Acha kupotosha watu
 
1863 ndio mama hellen akaanzisha itikadi ya wasabato
 
Mnyama wa kitabu cha Ufunuo

Watu wengi hawafahamu kuwa mnyama ni nani, na wengi wamejihusisha naye bila wao wenyewe kujua kama wanashiriki na mnyama. Lakini Mungu hajatuacha gizani, hivyo, kwa kupitia neno lake (Maadiko Matakatifu) tunaweza kumfahamu mnyama huyu aliyelezwa katika kitabu cha Danieli na Ufunuo.

Tunapaswa kuyaacha maandiko yajitafisiri yenyewe; kwa maana “hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2Petro 1:20-21. Hatupaswi kumuacha mtu flani atafsri unabii kwa jinsi yake mwenyewe, badala yake tunapaswa kuiacha Biblia ijitafsiri yenyewe.

Katika Danieli 7 wametajwa “wanyama wanne” ambao wanawakilisha falme nne. Kumbuka mmyama wa 4 aliyetajwa katika Danieli 7 ndiye mnyama aliyetajwa katika kitabu chote cha Ufunuo. Hivyo hapa tutaangalia sifa za mnyama wa nne wa kitabu cha Danieli, na mnyama wa kitabu cha Ufunuo, kisha tutaangalia ni wapi hapa duniani ambapo sifa za mnyama zinatimizwa kikamilifu.

1. Mnyama atakuwa na uwezo wa kisiasa na kidini (kanisa na serikali).

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.

Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

Mnyama huwakilisha taifa au ufalme

Danieli 7:17 “Wanyama hao…wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani”

Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”

Kutokana na Ufunuo 17:3, mnyama huyu ana mwanamke aliyeketi juu yake, na kwa sababu unabii unatafisiri mwanamke kama kanisa, na mnyama kama taifa. Je kuna taifa au serikali ambayo imechanganywa pamoja na kanisa kama kitu kimoja? Ndiyo! Vatican, ni serikali au taifa ambalo limechanganywa pamoja na kanisa la Romani Katoliki kama kitu kimoja, na kuongozwa na mtu mmoja ambaye ni Papa.

2. Mnyama atakuwa na kanisa & serikali vimekaa juu ya milima 7.

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…mwenye VICHWA SABA na pembe kumi.”

Vichwa saba katika unabii vinawakilisha milima saba.

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”

Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?

“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.

“Je vilima saba vya Roma ni nini?

Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com

ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma

“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine (#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline, (#2) Quirinal, (#3) Viminal, (#4) Esquiline, (#5) Caelian, (#6) na Aventine (#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –http://www.britannica.com/seo/s /seven-hills-of-rome/

Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali, harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la Romani Katoliki pekee.

3. Mnyama atatoka baharini

Ufunuo 13:1 “Kisha nikaona mnyama AKITOKA KATIKA BAHARI, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Bahari katika unabii huwakilisha watu/jamaa, mataifa, lugha.

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”

Ukatoliki wa Romani ulitokea ulaya ya magharibi pamoja na makutano ya “watu/jamaa, mataifa, na lugha.” Na kwa wakati huu kanisa la Romani Katoliki lina idadi kubwa ya “watu, mataifa, na lugha,” kuliko kanisa jingine lolote duniani mwote. Na sasa, baada ya kuanzishwa kanisa moja duniani, Juni 26, 2000, Papa alichaguliwa kama kiongozi wa makanisa yote ambayo yameungana na lake. Hii ilifanya kanisa liongezeke mara mbili. Na hivi karibuni, makanisa yote pamoja na yasiyo ya Kikristo yatatangaza kwamba Papa ni kiongozi wao mwema.

Na Juni, 2008 mataifa 174 katika mataifa 192 duniani, yana serikali zao zikiwakilisha Vatican. Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabii huu kwa ukamilifu.

4. Mnyama atatawala miaka 1260. (kabla hajapata jeraha la mauti).

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataadhimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake KWA WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI.”

Ufunuo 12:6 “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko mda wa SIKU ELFU NA MIA MBILI NA SITINI.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake MIEZI AROBAINI NA MBILI.”

Danieli 7:25 inaonyesha muda ambao angetawala mnyama, kama wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Ufunuo 13:5 inauonyesha mda huu wa utawala wa mnyama, kama miezi 42, miezi 42 = miaka 3 na 1/2. Hivyo, ukiangalia kwa makini hapa utaona kuwa, wakati = mwaka 1, na nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka.

Kwa hiyo, wakati nyakati mbili nusu wakati = miaka 3 na nusu ya Danieli 7:25, au miezi 42 ya Ufunuo 13:5, au siku 1260. Mahesabu haya yanathibitishwa katika Ufunuo 12:6 ambapo inasema, “Yule mwanamke (kanisa) akakimbilia nyikani…wamlishe huko mda wa siku 1260.” Kwa hiyo miaka 3 na 1/2 = miezi 42 au siku 1260 ambazo mnyama angetawala kabla hajapata jeraha la mauti.

Bado, wengine watakataa na kusema, hapana, miezi 42 haiwezi kuwa sawa na siku 1260, kwa sababu miezi mingine haina siku 30. Lakini katika unabii mwezi 1 = siku 30. Mwanzo 7:11 inasema, mvua za garika zilianza siku ya 17 ya mwezi wa pili, na Mwanzo 8:3, 4. inasema kuwa maji yakapunguka mwishoni mwa siku 150, harafu safina ikatua siku ya 17 ya mwezi wa saba. Hizo ni miezi 5 tangu mvua zilipoanza. Kama ukigawanya siku 150, kwa miezi 5, utapata siku 30 kwa kila mwezi. Hivyo, miezi 42 ikizidishwa kwa 30 jibu litakuwa 1260. Kwa hiyo wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ni sawa na miaka 3 na nusu, au miezi 42, au siku 1260. Kwa hakika, Ufunuo 12:6 inathibitisha mahesabu haya inaposema kuwa watoto wa Mungu watakimbilia nyikani kwa muda wa siku 1260 wakati wa utawala wa mnyama (upapa).

Katika unabii siku 1 ni sawa na mwaka 1,

Ezekieli 4:6 “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.”

Hesabu 14:34 “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…”

Kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu. Je hii ilitokea? Je unabii huu ulitimia? Au Je kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa unabii huu ulitimia?

Kwanza kabisa tunatakiwa kujua ni lini kanisa la Romani Katoliki lilipata nguvu zote za kutawala kama “mwanamke juu ya mnyama” (kanisa na serikali), na kutawala kisiasa na kidini kwa wakati mmoja kama Ufunuo 17:3 inavyosema.

“Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

Hiistoria inathibitisha kuwa upapa umeanza utawala wake kama “kanisa na serikali” mwaka 538 B.K. juu ya amri ya mfalme Jastinian, na chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius. Na unabii unasema mnyama (upapa) atatawala miaka 1260 kabla haujapata jeraha la mauti.

Ukiongeza miaka 1260 katika mwaka ambao kanisa la Romani Katoliki lilianza kutawala kisiasa na kidini, mwaka 538 B.K., utapata 1798 B.K. Hivyo, unabii unasema utawala wa kwanza wa mnyama ungeisha 1798 B.K. Je utawala wa mnyama uliisha mwaka huo 1798 B.K?

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Kwa hakika, hizo ni miaka 3 na 1/2 au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ambazo ni miezi 42 au siku 1260 za unabii ambazo mnyama angetawala kisha angepata pigo la mauti au kuchukuliwa mateka. Je mnyama alipata pigo la mauti mwaka huo 1798 B.K?

5. Mnyama atapokea jeraha la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake lake la mauti likapona…”

Ufunuo 13:10 “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga…”

Kama tulivyoona huko nyuma baada ya mnyama kutawala miaka 1260 angepata jeraha la mauti na kuuawa kwa upanga (upanga = vita). Baada ya mnyama kumaliza utawala wake wa miaka 1260, ambao ulianza 538 B.K. hadi 1798 B.K., Napoleon alimtuma Generali/Jemedari wake Berthier pamoja na jeshi lake, kwenda Roma kuuondoa utawala wa upapa.

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Napoleon alipomtuma Generali wake Berthier kwenda kumuondoa Papa madarakani, hapo ndipo jeraha la mauti lilipompata mnyama, na mwaka uliofuata 1799 B.K. Papa alikufa. Hii ndiyo sababu watoto wa kikatoliki katika parokia hufundishwa kuwa Napoleoni alikuwa mpinga Kristo.

“Nusu ya Ulaya walidhani…kwamba pamoja na papa upapa ulikuwa umekufa.” –Joseph Rickaby “The Modern Papacy” Lectures on the History of Religion, Lecture 24, (London Catholic Truth Society, 1910), p. 1

Lakini unabii ulisema kuwa jeraha hili lililompata mnyama lingepona. Je jeraha hili lilipona? Je utawala wa upapa ulipoondolewa madarakani na Generali Berthier ulipata nguvu zake tena?

6. Mnyama atapona jeraha lake la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, NA PIGO LAKE LA MAUTI LIKAPONA. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”

Kama tulivyoona, upapa ulipata jeraha la mauti mwaka 1798 B.K. Vaticani ilibaki kama kanisa tu bila nguvu za kisiasa, na unabii ulisema jeraha hili lingepona. Je jeraha la mauti lilipona? Baada ya jeraha la mauti kutokea miaka kadhaa badaye katika mwaka 1929 B.K. Italia ikautambua mji wa Vaticani kama serikali ya kujitegemea, hii ilimfanya papa kuwa na nguvu tena kama mtawala wa kisiasa na kidini. kama unabii ulivyosema kwamba jeraha la mauti lingepona, na upapa ungerudishiwa tena uwezo wake wa kanisa na serikali kwa pamoja. Hebu angalia magaziti yaliyotoa taarifa hiyo jinsi waandishi wake walivyotumia lugha ya unabii bila ya wao wenyewe kujua.

Kusaini kwa Mussolini na (Kadinali) Gasspari mkataba wa kihistoria wa Romani

“Suala la Romani usiku huu lilikuwa ni jambo lililopita, na Vaticani ilikuwa katika amani na Italia…katika kuweka sahihi kwenye mkataba wa kukumbukwa kuponya jeraha la miaka mingi, uchangamfu wa kupindukia ulionyeshwa na pande zote.” –The San Francisco Chronicle. Feb. 11, 1929

Papa Amekuwa Kiongozi Wa Serikali Tena

“Roma, Juni 7.–Kutoka saa 5 kamili asubuhi hii kulikuwa na mtawala mwingine wa serikali ya kujitegemea duniani. Katika mda huo waziri mkuu Mussolini, kama waziri wa mambo ya nje Italia akimuwakilisha mfalme Victor Emmanuel–waziri mkuu wa kwanza Italia kuvuka kizingiti cha chini cha mlango wa Vaticani–akibadilishana na kadinali Gasspari, wakala wa serikali ya upapa, akimuwakilisha papa Pius XI, makubaliano ya mikataba yalisainiwa katika ikulu ya Lateran Feb. 11. Kwa kitendo hicho rahisi mtawala wa serikali ya kujitegemea ya mji wa Vaticani amekuwepo.” — New York Times July 7, 1929

Hivyo, unabii huu ulitimia kikamilifu na jeraha la mauti lililoupata upapa 1798 B.K. lilipona kabisa tangu 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za “kisiasa na kidini” au “mwanamke juu ya mnyama.” Kwa kumaliza sehemu hii tunagundua kwamba mnyama huyu ndiye aliyekuwako, naye hayuko, na sasa yupo.

7. Mnyama aliyekuwako, naye hayuko, naye yuko.

Ufunuo 17:8 “Yule mnyama…alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari…”

Mnyama aliyekuwako: ni kanisa la Romani Katoliki tangu lilipoanza kutawala kama “kanisa & serikali” 538 B.K. na likaendelea mpaka. Napoleon alipomtuma Berthier kwenda kuuondoa utawala wa upapa. 1798 B.K.

…naye hayuko tokea 1798 B.K. mpaka kusaini kwa mkataba uliofanyika katika ikulu ya Lateran katika mwaka 1929 B.K. Vaticani ilikuwa kanisa tu bila uwezo wa kiserikali.

…naye yu tayari kutoka 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za kisiasa na kidini, “kanisa & sesikali” au mwanamke juu ya mnyama.

8. Mnyama atabadili majira na sheria za Mungu.

Danieli 7:25 “…naye ataadhimu kubadili majira na sheria…”

Unabii huu ni ushahidi ulio wazi sana ambao karibu kila mtu hawezi kusumbuka kuelewa kwamba ni kanisa gani hapa duniani lililobadilisha sheria za Mungu. Ni kanisa moja tu la Romani Katoliki ndilo lililobadilisha sheria za Mungu kama Danieli 7:25 inavyodai kuwa. Kanisa la Katoliki limebadilisha sheria ya pili inayozuia kuchonga sanamu ya kitu chochote kile (angalia Kut 20:4). Katika katekism kanisa limeirarua amri ya 2 kisha likaigawa amri ya 10 katika sehemu mbili ili kuonyesha amri 10 zote. Lakini Je ni nani hapa duniani anayedai kuwa anauwezo wa kubadili amri za Mungu?

“Papa anauwezo wa kubadili majira, kubadili sheria, na kuachana na mambo yote, hata maagizo ya Kristo!” “Papa anayo mamlaka na mara nyingi ameyatumia, kuachana na amri ya Kristo.” –Decretal, de Tranlatic Episcop. Cap. (The Pope can modify divine law.) Ferraris’ Ecclesiastical Dictionary.

“Papa ni wa mamlaka kuu na nguvu kiasi kwamba anaweza kurekebisha, kuelezea au kutafsiri hata sheria za Mungu…Papa anaweza kurekebisha sheria ya Mungu, kwa sababu nguvu zake si za mwanadamu, bali ni nguvu za Mungu, na hutenda kama mwakilishi wa Mungu juu ya dunia.” –Lucius Ferraris,Prompta Ribliotheca, “Papa,” art. 2, translated.

Tangu kwamba papa ana mamlaka na maranyingi ameyatumia kubadili majira na sheria za Kristo, Je alibadili sheria ya Sabato? Je kanisa katoliki liliibadili Sabato ya siku ya saba ya wiki kwenda siku ya kwanza ya wiki? Kwa hakika kanisa lenye linakubali!

“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” –Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

“Swali: Siku ipi ni siku ya Sabato?
Jibu: Jumamosi ni siku ya Sabato.
Swali: Kwanini tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi?
Jibu: Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa katoliki, katika balaza la Laodikia (364 BK) liliihamisha kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.” –The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine,p. 50, 3rd ed.

“Kanisa la Romani (Katoliki) liliigeuza amri ya nne kwa kuiondolea mbali Sabato ya neno la Mungu, na kuanzisha Jumapili kama siku ya mapumziko.” –Nicholas Summerbell, History of the Christian Church, 3rd edition, 1873, p. 415 [Christian Church (Christian Connection)].

“Na ni wapi tumeambiwa katika maandiko kwamba tutunze siku ya kwanza kabisa? Tumeamriwa kutunza siku ya saba; lakini hakuna sehemu yoyote tuliyo amriwa kutunza siku ya kwanza. Sababu ya kutunza siku ya kwanza ya wiki kitakatifu badala ya siku ya saba ni kwa sababu ile ile kwamba tunatunza mambo mengine mengi, siyo kwa sababu ya Biblia, lakini kwa sababu kanisa, limeyaingiza [limeyaamuru].” –Isaac Williams, Plain Sermons on the Catechism, vol 1, pp. 334, 336 [Anglican].

Hivyo, kanisa la Romani Katoliki liliibadili sheria ya Sabato na kuwaamuru watu watunze jumapili badala yake. Na mwaka 1582. Papa Gregory XIII, alianzisha kalenda mpya. Kwa vyovyote, ni Vaticani ndiyo ilitimiza unabii huu kwa ukamilifu kabisa, hakuna jumuiya, wala shirika, wala sehemu yoyote ya kidini au isiyo ya kidini ambayo imetimiza unabii huu, kama ilivyo Vaticani. Ni kanisa la Romani Katoliki pekee ambalo lilibadili sheria, na majira, na kuamuru siku ihesabiwe kuanzia saa sita usiku kinyume na Maandiko yanayothibitisha kuwa siku huanza kuhesabiwa jioni.

Mwanzo 1:5 “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.”

9. Mnyama atanena maneno ya makufuru juu ya Mungu.

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu…”

Ufunuo 17:3 “…nikaona mwanamke ameti juu ya mnyama…mwenye kujaa majina ya makufuru…”

Ufunuo 13:1 “…nikaona mnyama…mwenye…vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena makuu, ya makufuru…”

Kukufuru katika Biblia inaelezewa kama hali ya mtu kujifanya yeye mwenyewe kama Mungu.

Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwamadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.”

Je nani hujiita na kujifananisha na Mungu hapa duniani?

“Papa siyo mwakilishi tu wa Yesu Kristo, yeye ni Yesu Kristo mwenyewe, amejificha chini ya uficho wa mwili.” –Catholic National July 1895.

“Kwa kuwa wewe u mchungaji, wewe u tabibu, wewe u mwongozaji, wewe u mkulima, hatimaye wewe u Mungu mwingine duniani.” –Labbe and Cossart’s “History of the Councils.” Vol. XIV, col. 109

“Tunapachukulia juu ya dunia hii sehemu ya Mwenyezi Mungu…” –Pope Leo XIII Encyclical Letter of June 20, 1894,

Katika “The Bull Unam Sanctam” iliyotolewa na Papa Boniface VIII inasomeka kama ifuatavyo…
“Papa wa Roma huukumu watu wote, lakini yeye haukumiwi na mtu. Tunatangaza, kutetea, kuelezea, na kutamka; kutawaliwa na Papa wa Roma ni kwa kila kiumbe cha mwanadamu muhimu kwa ajili ya wokovu ambao ulisemwa na Kristo ‘Ameviweka vitu vyote chini ya miguu yake’ inaonekana vizuri imethibitishwa kwangu…Nina mamlaka ya Mfalme wa Wafalme. Mimi ni yote katika yote na juu ya yote, hivyo basi, Mungu Mwenyewe na mimi, kasisi wa Mungu tuna usawa mmoja, na ninaweza kufanya yote ambayo Mungu anaweza kufanya.”

“Mwokozi mwenyewe ni mlango wa zizi la kondoo; ‘Mimi ni mlango wa kondoo’. kwenye zizi hili la Yesu Kristo, hakuna mtu anayeweza kuingia mpaka awe ameingizwa na Papa mtawalawa na ni pale tu kama wameunganika naye ndipo wanadamu wanaweza kuokolewa, kwa sababu Papa wa Roma ni kasisi wa Kristo na ni mwakilishi wake kwa nafisi duniani.” –(Pope John XXIII in his homily to the Bishops and faithful assisting at his coronation on November 4, 1958).

Kudai kuwa Mungu duniani Biblia inathibitisha kuwa ni kukufuru ju ya Mungu aliye hai. Kufuru nyingine ni kudai kuwa na uwezo wa kusamehe dhambi.

Marko 2:7 “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi ispokuwa mmoja, ndiye Mungu?”

Je makuhani wa kanisa la Romani Katoliki hudai wana uwezo wa kusamehe dhambi?

“Kuhani kiukweli kabisa husamehe dhambi kwa uwezo aliopewa na Kristo.” -Joseph Devarbe’s Catechism, p. 279

“Dhambi zinaweza kusamehewa kupitia sakramenti pekee…wote makuhani na sakramenti ni vifaa ambavyo Kristo anavitumia kukamilisha msamaha ndani yetu na neema ya utakaso.” -Catechism of Trent, p. 115.

“Haya mamlaka ya jaji (Judicial authority) yatajumuisha hata uwezo wa kusamehe dhambi.” –[The Catholic Encyclopaedia Vol 12, -article “Pope” pg 265]

“Na Mungu mwenyewe analazimika kufungwa na hukumu ya kuhani wake na ama kutokuomba msamaha au kuomba msamaha, kutokana na kama wanakataa kutoa ukamilifu, unaotoa toba inayoridhisha.” –Liguori, «Duties and Dignities of the Priest», p.27

10. Mnyama ana jina lenye namba 666.

Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, ispokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinaadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”

Biblia inatuambia kuwa hesabu au namba ya jina la mnyama ni 666

Kanisa la Romani Katoliki hudai kuwa Papa ni kichwa cha kanisa au mwakilishi wa Yesu.

“Maneno yaliyoandikwa katika kofia (miter) ya Papa ni haya, ‘VICURIUS FILII DEI’. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa, ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, alimteua M.t. Petro kuwa kama mwakilishi wake…hata hivyo Askofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.'” –Our Sunday Visitor, (Catholic Weekly) “Bureau of information,” Huntington, Ind., April 18, 1915.

Kwa hiyo “VICARIUS FILII DEI” ndilo jina linalotumiwa na mamlaka ya Upapa na kumthibitisha Papa kama kichwa cha kanisa.

Helufi za kilatini zinaweza kutumika pia kama namba, na siku hizi hujulikana kama “Namba za Kirumi,” na helufi U inaweza pia kutumika kama V.

“VICARIVS FILII DEI”

(Kasisi wa Mwana wa Mungu)

V........5
I........1
C..... 100
A...... 0
R.......0
I........1
V.......5
S.......0
F........0
I.........1
L .......50
I.........1
I.........1
D........500
E.........0
I............1
Jumla= 666

Vicarius inamaanisha, katika nafasi ya
Filii Mwana
Dei Mungu
Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabi huu wa hesabu ya mnyama 666 kwa ukamilifu kabisa.

11. Onyo la Mungu kwa wote walio katika kanisa katoliki.

Mungu anaoya vikali sana juu ya wale wote ambao wanashirikiana na mnyama huyu, kama wewe ni mmojawapo unapaswa kuchukua uamuzi sahihi sasa bila kupoteza muda; kwa maana hukumu itakuja juu ya mnyama na yule kahaba (kanisa Katoliki) aliyekaa juu mnyama. Hili ni onyo la mwisho la upendo na la rehema kutoka kwa Mungu.

Ufunuo 14:9-10. “Na mwingine, malaika watatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Ufunuo 19:20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;”

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amemkumbuka maovu yake…Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemuhukumu ni mwenye nguvu.
 
Attachments

  • Screenshot_20220109-125944_Lite.jpg
    Screenshot_20220109-125944_Lite.jpg
    79.8 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220109-125934_Lite.jpg
    Screenshot_20220109-125934_Lite.jpg
    79.4 KB · Views: 9
1863 ndio mama hellen akaanzisha itikadi ya wasabato
Huyu aliyekuwa na desturi ya kusali siku ya Sabato Ni mama Hellen?

Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; NA SIKU YA SABATO AKAINGIA KATIKA SINAGOGI KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE, akasimama ili asome.
 
Mitume wa kwanza waliabudu siku ya sabato mkuu?

Ushahidi katika vitabu vya Injili
Katika Agano Jipya siku ya kwanza ya juma imetajwa mara 8 tu, na mara zote haijasemwa popote kwamba imetakaswa au kwamba Mungu aliagiza watu watunze siku hiyo.

Katika Kitabu cha Mathayo siku ya kwanza ya juma imetajwa mara moja ikihusiana na ufufuo wa Yesu,
na hakuna ibada iliyofanyika siku hiyo, bali Sabato ilipoisha ndipo Mariamu siku ya jumapili alienda kaburini na akakuta Yesu amekwishafufuka.

Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.”

Tukio hili hili limeandikwa pia katika Injili nyingine zote tatu kama ifuatavyo:

Marko 16:1-2 “Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. 2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;”

Angalia walisubiri Sabato ikaisha jioni, ndipo wakanunua manukato ili jumapili asubuhi wakampake Yesu kaburini.

Yohana 20:1 “Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alifajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.”

Marko 16:9-11″ Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. 10 Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia. 11 Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki”

Yesu aliipomtokea Mariamu Magdarene siku ya jumapili, Alimwambia “enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. 18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.” Yohana 20:17-18. Mpaka Jumapili hiyo aliyofufuka Yesu ilipita, wala Yesu Mwenyewe hakusema, wala hakumwagiza mtu yeyote kwamba kwa sababu amefufuka jumapili basi ameitakasa jumapili na watu wake watunze jumapili badala ya jumamosi.

Tena katika jumapili hiyo ya ufufuo Yesu aliwatokea wanafunzi wake jumapili jioni wamekusanyika kwa hofu ya Wayahudi.

Yohana 20:19-20 “Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. 20 Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.”

Hapa Yesu alipowatokea wanafunzi wake ilikuwa ni Jumapili Jioni na jumatatu ndiyo ilikuwa inaanza kuingia, kama Yesu angekuwa na nia ya kuachana na Sabato ya kiyahudi, na kwamba alikuwa ameitakasa jumapili, hapa ndipo alikuwa na nafasi ya kuwaeleza wanafunzi wake. Lakini ukisoma maneno aliyowaambia siku hiyo katika Yohana 20:19-23, na Luka 24:44-49 utaona kuwa hakuna mahali popote alipowaambia kwamba sasa Jumapili nimeitakasa.

Tukihesabu siku nane mbele kutoka jumapili hiyo tunafika katika Jumapili nyingine ambapo Yesu aliwatokea wanafunzi wake tena.

Yohana 20:26 “Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.”

Milango ilikuwa imefungwa kwa sababu ya hofu ya Wayahudi, na wakati huu wanafunzi wote walikuwepo mahali pamoja, pamoja na Tomaso ambaye pale nyuma hakuwepo. Yesu aliwatokea kwa sababu ya Tomaso ambaye alikuwa hataki kuamini kwamba Bwana amefufuka, na sasa Yesu alishughulika na Tomaso ili apate kuamini. Tena hapa Yesu alikuwa na nafasi ya kuwaambia wanafunzi kwamba ameitakasa Jumapili, lakini katika mazungumzo yake yote na Tomaso siku hiyo hakusema popote kwamba ameitakasa Jumapili, wala hakuagiza amri yoyote kuhusu kupumzika siku ya Jumapili.

Yesu mara kwa mara aliwatokea wanafunzi wake, aliwatokea wanafunzi wawili ambao walikuwa wakielekea kijiji kinachoitwa Emau na akazungumza nao “Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.” (Luka 24:27). Hata hivyo hakusema popote kwamba sasa ameitakasa Jumapili. Wanafunzi hao wawili walirudi kuwapasha habari wale kumi na mmoja kuhusu jambo hilo, tena Yesu akawatoke mara nyingine wakiwa wote na wale kumi na mmoja (Luka 24:36-49), lakini bado hakusema neno lolote kwamba ameitakasa Jumapili. Tukio hili ni lilelile kama la Yohana 21:1-23, ambapo Yesu akimwambia Petro kwamba “Lisha kondoo wangu” (21:17), lakini bado hakuwaambia popote kwamba ameitakasa Jumapili.

Kwa mtu yeyote ambaye ana akili timamu itakuwa ni vigumu sana kuamini kwamba Yesu aliitakasa Jumapili wakati wa kufufuka kwake, na tayari hadi kupaa kwake bado yuko kimya hasemi popote kwamba nimeitakasa Jumapili. Ni kitu ambacho hakiwezekani Yesu kuitakasa jumapili, harafu akakaa kimya siku nyingi namna hiyo asiwaambie wanafunzi wake jambo hilo. Mpaka hapa ushahidi wa vitabu vya Injili vyote vinne viko kimya na havisemi popote kwamba Yesu aliitakasa Jumapili. Vitabu vinne viliandikwa miaka 40 baada ya Yesu kupaa mbinguni, na tayari waandishi wake hawasemi popote kuhusu ibada ya Jumapili.

Sabato ya kwanza baada ya Yesu kupaa

Tunavuka kutoka vitabu vinne vya Injili hadi kitabu cha Luka cha matendo ya mitume ambacho kinasemekana kiliandikwa miaka 40 au 50 baada ya kupaa kwa Yesu. Hapa ushahidi wa kwanza kabisa tunaoupata ni kwamba, baada ya Yesu kupaa mbinguni mitume walirudi Yerusalemu kusubiri ahadi ya Roho Mtakatifu, na sabato ilipofika iliwakuta wako Yerusalemu, wakaingia orofani walimokuwa wakiishi kina Petro, wakafanya ibada kama ilivyo kawaida kila sabato.

“Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.” Matendo 1:12

Walipofika Yerusalemu, yapata watu mia na ishirini walipanda orofani, walipokuwa wakikaa kina Petro kwa ajili ya kusali, siku hiyo ilikuwa ni siku ya sabato, na Biblia inasema.

“Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.” Matendo 1:14

Katika siku hiyo hiyo ya sabato mtume Petro alisimama akahubiri Injili ya Yesu mbele ya wale watu 120 (angalia Mdo 1:15-20), tena sabato hiyo hiyo walipiga kura na kumchagua Mathiya mahali pa Yuda Iskariote (angalia Mdo 1:21-26). Hii inathibitisha kuwa baada tu ya Yesu kupaa, sabato iliyofuata mitume waliitunza kama ilivyo kawaida ya siku zote. Na siku iliyofuata ilikuwa ni Jumapili siku ya Pentekoste, ambayo tunaelekea kuijadili.

Siku Ya Pentekoste Jumapili.
Baada ya sabato waliyosali mitume kuisha kesho yake ilikuwa ni sivan 6 siku ya Pentekoste, ambayo kwa mzunguko wa mwaka huo iliangukia Jumapili.

Matendo 2:1-4 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”

Mitume walijua kwamba sivan 6 ni siku ya Pentekoste hivyo wasingetoka kwenda popote kama sheria ya Musa inavyoagiza, walikaa pamoja kwa ajili ya pentekoste, na Mungu akashusha Roho Mtakatifu ili kuitimiliza pentenkoste.

Wengi wamekuja kuamini kwamba siku ya pentekoste ndiyo sababu kuu ya ibada ya hadhara kuhamishiwa Jumapili, lakini hii inatokana na uelewa mdogo au kutokuelewa kabisa nini maana ya Pentekoste. Pentekoste inamaanisha “kuhesabu hamsini”, Mungu alikuwa amewaagiza wana wa Israeli kuhesabu siku hamsini tangu 16 nisani hadi 6 Sivan, Pentekoste siku zote huangukia katika siku ya 6 ya mwezi wa tatu wa kiyahudi unaoitwa Sivan, Sivan 6 inaweza kuangukia katika siku ya wiki yoyote ile, iwe ni jumapili, jumamosi, jumatatu au ijumaa, kulingana na mzunguko wa mwaka ulivyoenda.

Katika Pentekoste Mungu haangalii siku ya wiki wala juma, haangalii jumapili wala jumamosi, bali anaangalia tarehe 6 ya mwezi wa tatu Sivan. Katika kipindi cha mitume Sivan 6 iliangukia jumapili, lakini pia ingeweza kuangukia jumatatu au jumamosi kulingana na mzunguko wa mwaka ulivyo. Kulingana na Walawi 23:16-19 kila ifikapo Pentekoste zingetolewa “sadaka za amani” na “sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto”, Hii ingewakilisha vizuri kushuka kwa Roho Mtakatifu kama ubatizo wa moto katika Sivan 6 ambayo ni pentekoste.

Sivani 6 inaweza kuangukia katika juma lolote, haijalishi ni jumapili, jumamosi, au jumatatu. Hivyo kutumia siku ya Pentekoste ili kufundisha watu kwamba ibada ya hadhara ilihamishiwa jumapili ni kwenda kinyume na utaratibu wa Mungu katika mpangilio wa “siku za sikukuu” alizowapa wana wa Israeli.

Hata hivyo, kama Pentekoste ndiyo sababu ya wewe kwenda kanisani jumapili, inakubidi uitendee haki kwa kuhesabu kwanza siku hamsini ndipo uende kanisani. Vinginevyo Pentekoste haihusiani na jumapili kwa jinsi yoyote ile, Pentekoste ilitimia kama Mungu alivyokuwa ameipangilia, Pentekoste ilihusiana na kutimia kwa ahadi ya Roho Mtakatifu na sio siku ya kusali ibada ya hadhara.

Baadhi wanaweza kudhani kwamba kwa sababu pentekoste hiyo Jumapili mitume walikuwa wako mahali pamoja, hivyo Sabato ilikuwa imehamishiwa siku ya Jumapili. Lakini haiungi mkono swala hili hata kidogo; kwa kuwa ilikuwa ni kawaida ya mitume kusali na kumhubiri Yesu kila siku, na hata hivyo siku ya Sabato walipumzika, si kupumzika katika kuhubiri Injili, bali kupumzika kutoka katika kazi zao wenyewe kama sheria inavyogiza.

Luka 24:51-53 “Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. 52 Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. 53 Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.”

Matendo 5:42 “Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.”

Baada ya kupaa kwa Yesu mitume walikuwa kila siku wanahubiri Injili, na hivyo jumapili iliyofuata hata kama ingekuwa sio pentekoste, lazima ingewakuta wakiwa pamoja. Lakini hii haimaanishi kwamba sabato ilihamishiwa siku ya jumapili; kwa maana historia iliyofuata inathibitisha ukweli huu, jinsi walivyoendelea kutunza Sabato, na walifanya kazi siku ya jumapili kama utakavyokuja kuona huko mbele.

Paulo ahutubu huko Troa siku ya Jumapili. Je hii inamaanisha mitume walitunza Jumapili kitakatifu?
Matendo 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.”

Katika Biblia siku huanza jioni na kuisha jioni, hivyo hapa walikuwa wamekutana Jumamosi siku ya Sabato ili kufanya ibada, na Sabato ilipoisha wakati wa jioni, ndipo Jumapili, siku ya kwanza ya juma ikaingia. Kwa sababu mtume Paulo alitaka kusafiri kesho yake asubuhi—neno “siku ya pili yake” la kigiriki ni: ἐπαύριον (epaurion)—na linamaanisha pia asubuhi inayofuata, na kwa kuwa walikuwa wanamega mkate, hivyo ikawachukua muda hadi usiku wa manane. Kesho yake asubuhi ilikuwa ni jumapili, na hawakufanya ibada yoyote, bali Mtume Paulo alisafiri Jumapili hiyo asubuhi.

Hapa Mtume Paulo alisubiri mpaka Sabato ya kiyahudi ikaisha wakati wa jioni, na ilipoingia Jumapili, usiku, akawahutubu watu wa Troa ili kuwaaga kwamba kesho yake asubuhi angeondoka. Swali linabaki kwamba, kama jumapili ilikuwa imetakaswa na mitume walikuwa tayari wanafanya ibada ya hadhara katika siku hiyo kama baadhi ya watu wanavyodhani. Ingewezekanaje mtume Paulo kuendesha ibada Jumapili usiku harafu kesho yake Jumapili asubuhi badala ya kuendesha ibada yeye akaitumia kusafiri? Lakini utasema kwamba walikuwa wakimega mkate Jumapili hiyo usiku, ndiyo, mkate walimega siku zote, na sio jumapili usiku tu. Matendo 2:42,46 inasema “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. . . .46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe.”

Au kama ukisema kwamba Paulo aliwahutubu, ndiyo aliwahubu, wao walihutubu kila siku, na walidumu katika mafundisho ya mitume kila siku, kama sisi leo tunavyofanya ibada majumani mwetu usiku kila siku. Luka 24:53 inasema, “Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.” Paulo “aliwahutubu akiazimu kusafiri kesho yake asubuhi”; na hivyo alikuwa akiagana nao, na kuwasihi kwa machozi kwamba wadumu katika imani ili ibilisi asiwachukue katika mtego wake, kitu kilichomchukua muda mrefu kukikamilisha hadi usiku wa manane; na kesho yake Jumapili asubuhi ilipofika Paulo akaondoka kwenda safari yake. Matendo 20:11 inasema, “Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake.” Alienda zake jumapili hiyo asubuhi.

Kutumia Matendo 20:7 ili kumshawishi mtu kwamba mitume waliachana na Sabato, badala yake wakatunza Jumapili, si kutumia Maandiko kwa uaminifu. Kesho yake Jumapili asubuhi, Paulo alisafiri na hakufanya ibada yoyote. Hivyo makanisa yote yanayosali ibada ya hadhara siku ya Jumapili kwa kisingizio cha fungu la Matendo 20:7, ili yalitendee haki fungu hilo, yanapaswa kufanya ibada zao kila Jumapili usiku, na sio asubuhi au mchana.

Je Wakorinto walitunza Jumapili au Jumamosi?
1 Wakorinto 16:2 “Siku ya kwanza ya juma [Jumapili] kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;”

Je hii inamaanisha kwamba huko Korinto watu walifanya ibada ya hadhara siku ya Jumapili? Kwa hakika hapana! Paulo aliwaagiza Wakorinto vilevile kama alivyokuwa amewaagiza Wagalatia (1 Kor. 16:1) kwamba siku ya jumapili watunze kiasi cha pesa kulingana na kila mtu alivyobarikiwa, ili Paulo atakapoenda Korinto pesa hizo ziwe tayari, na isiwepo haja ya kuchagiza tena. Pesa hizo zilikuwa ni mchango kwa ajili ya watakatifu waliozihitaji huko Yerusalemu, na wakati ambapo Paulo angelifika huko Korinto, angelizikuta zikiwa tayari naye angelizituma kwenda Yerusalemu ili kufanikisha mahitaji hayo (1 Kor. 16:3). Hivyo pesa hizo zilikuwa sio dhaka, wala sadaka, bali ni changizo tu, ambalo wakati Paulo angefika Korinto angezituma zote kwenda Yerusalemu na changizo hilo lingefikia mwisho.

Kwa sababu Wakristo waliruhusiwa kufanya kazi siku ya Jumapili, hivyo kiasi cha pesa ambacho wangebarikiwa na Mungu kukipata Jumapili hiyo, wangekiweka akiba kwa ajili ya mchango uliohitajika huko Yerusalemu. Hii isingewezekana kufanywa siku ya Sabato, Jumamosi; kwa maana hamna pesa yoyote inayopatikana siku hiyo kwa kuwa Wakristo wote hawakufanya kazi Jumamosi.

Wale wanaotumia fungu hili kudai kwamba linathibitisha kwamba Wakorinto walifanya ibada ya hadhara siku ya Jumapili, hii sio kweli. Na ili kuvunja madai haya ngoja tuangalie kama kanisa la Korinto walitunza Sabato au Jumapili. Wengi wamedanganywa kwa sababu wanaposoma fungu ambalo kwanza halisemi wazi wazi kwamba kulikuwa na ibada ya Jumapili hapo, wanakuwa wavivu kuangalia nini zaidi Biblia inasema ili kuthibitisha msimamo wao. Paulo yeye mwenyewe ndiye alianzisha kanisa la huko Korinto, Je Paulo alianzisha kanisa la kutunza Jumapili au la kutunza Jumamosi, Sabato? Kanisa la Wakorinto walitunza Sabato na sio Jumapili.

Matendo 18:1 “Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho.”

Je Paulo alipofika Korintho alitunza Jumamosi, Sabato, au Jumapili? Paulo alipofika Korintho alikutana na Myahudi mmoja anayeitwa Akila, pamoja na Prisila mkewe, hao pamoja na Paulo walikuwa mafundi wa kushona hema, na Paulo akakaa pamoja nao wakafanya kazi ya kushona mahema (Mdo 18:2). Sasa wakati Paulo anaishi huko Korinto na kufanya kazi ya kushona mahema, je alitunza Sabato, Jumamosi, au alitunza Jumapili?

Matendo 18:4 “Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.”

Paulo akiwa Korintho akifanya kazi ya kushona mahema, kila sabato alihudhuria kwenye sinagogi kutoa hoja zake ili awaongoe Wayahudi na watu wa mataifa pia. Kwanini hakufanya hivyo kila Jumapili kama Wakorinto walitunza Jumapili?

Baada ya Paulo kufarakana na Wayahudi, alienda katika nyumba ya mtu mmoja aliyekuwa akiishi karibu na sinagogi, na Wakorinto wengi wakaamini mahubiri yake. Paulo akakaa huko Korinto muda wa mwaka na miezi 6.

Matendo 18:11 “Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu.”

Katika muda huo Paulo alitunza Sabato 72 huko Korintho, na hakuna shaka kabisa kwamba Paulo wakati huo alianzisha rasmi kanisa la kutunza Sabato huko Korintho, na hakuna sehemu yoyote inayosema kwamba hapo Paulo alitunza Jumapili. Ni kweli kwamba Paulo akiwa huko Korintho alikataa sheria za kafara na sikukuu za kiyahudi za miandamo ya mwezi; yaan, sikukuu za kuadhimishwa kwa kufuata tarehe; kwa jina lingine zinaitwa “sabato za mwaka” ambazo zilitokea kwa mwaka mara moja tu katika mwezi ulioteuliwa, lakini alitunza Sabato ya wiki ambayo haihusiani na tarehe wala mwandamo wa mwezi na kanisa aliloanzisha huko ni la watunza Sabato. Hivyo wakati mtu anapotumia 1 Korintho 16:2 kudai kuwa Wakorinto walitunza Jumapili, madai yake si kweli, kwani Wakorinto walitunza Sabato.

Paulo aanzisha kanisa la watunza Sabato huko Antiokia!
Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli [ambaye ni Paulo].”

Kumbuka kuwa kanisa hili lililopo Antioki walikuwa ni watunza sabato kama tunavyoenda kuona hivi karibuni. Kanisa hili walifanya ibada na kufunga na kuomba, na Roho Mtakatifu akawaagiza kwamba wamtengee Paulo na Barnaba kwa ajili ya kazi ya kuhubiri Injiri. Ndipo kanisa hili likaweka mikono juu ya Paulo na Barnaba na kuwaacha waende zao (Mdo 13:3).

Paulo na Barnaba wakapelekwa au wakaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda Seleukia, Kipro, na katika Salami wakalihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi. Kisha wakenda Pafo, kutoka hapo waekaelekea Perge, na kutoka hapo wakarudi tena Antiokia na siku ya Sabato wakaingia katika Sinagogi.

Matendo 13:14 “Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.”

Basi, wakuu wa sinagogi wakawauliza ikiwa wana neno la kusema, ndipo Paulo akasimama na kuanza kuwahubiri habari za Yesu kwamba ndiye Kristo, akithibitisha kwa maandiko kutoka katika Agano la Kale na kuonyesha utimilifu wake katika Agano Jipya. Na alipomaliza wakamuomba awahubiri tena sabato ifuatayo.

Matendo 13:42 “Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.”

Na watu wengi wakawafuata Paulo na Barnaba. Matendo 13:43 “Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.” Tena Sabato iliyofuata Paulo akaenda kuwahubiri.

Matendo 13:44 “Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.”

Katika Sabato ya pili watu wote wa mataifa pamoja na Wayahudi karibu mji wote walikusanyika kusikia neno la Mungu. Inawezekanaje Paulo kusubiri hadi Sabato ya pili, ikiwa Sabato ilitanguka. Kwanini asingesema wazi kwamba sitakuja sabato ya pili bali ntakuja Jumapili? Baada ya Paulo kuhubiri Jumamosi ile, kesho yake Jumapili alikuwa na nafasi ya kuhubiri, lakini ni kwanini hakuhubiri Jumpili bali alisubiri hata Sabato ifuatayo ndipo akaenda kuhubiri? Na ni kwanini aliwahubiri mambo yote hayo lakini hakusema popote kwamba na Sabato imetanguka? Je Paulo alipojipatia watu wa mataifa karibu mji wote siku ile, aliwaambia kwamba hampaswi kutunza sabato ya kwenye amri kumi? Hapana!

Matendo 13:48-49 “Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.”

Baadaye Wayahudi wakaleta fitina juu ya Paulo na Barnaba, na watu walioamini. Basi, Paulo na Barnaba wakakung’uta mavumbi kisha wakaenda Ikonio (Mdo 13:51), wakawaacha pale “wanafunzi [walioamini] wamejaa furaha na Roho Mtakatifu.” (Mdo 13:52).

Paulo hakuwaagiza mahali popote kwamba waachie kutunza Sabato, ni hakika kwamba kanisa alilolianzisha hapo katika siku ya Sabato hiyo ya pili ambapo mji wote ulikusanyika kumsikiliza, liliendelea kuwa kanisa la watunza Sabato waliojaa furaha na Roho Mtakatifu, waliendelea kufuata desturi ya Paulo mwenyewe; nayo ni amri ya Mungu. Kanisa la Antiokia katika kipindi chote cha mitume walikuwa ni watunza Sabato
 
Ndio lakini akiwa MYAHUDI na sio MSABATO.. Acha kupotosha watu
WOKOVU WATOKA KWA WAYAHUDI ,UKITAKA KUJUA SIKU YA IBADA, NA MAAGIZO YA MUNGU UTAYAPATA KWA WAYAHUDI, SIO VATCAN (ROMA )

YOHANA 4:22

Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

MUNGU ALIWAPA MAAGIZO,MAUSIA, AMRI WAYAHUDI SIO WAROMA

WARUMI 3:1-8

Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
 
Mungu kasema usile nguruwe ni najisi wewe unasema utamaduni
Kwanini mitume wa kanisa la kwanza hawakua wakiabudu siku ya sabato?

Maelezo mengi mno siwezi yasoma mkuu! Okay it means SDA pekee ndio wataenda Mbinguni kwakua wanaishiaka Sheria ya MUNGU tofauti na WAKRISTO wa madhehebu mengine?
 
Okay

Okay okay vyema, Wayahudi hawamtambua BWANA YESU Kama MASIHI hivyo inabidi tuwafate nasisi tusiamini kwakua Wokovu watoka kwao?
 
NAWAPA MSISITIZO.
YESU ALITOA ONYO SANA KWA WATU WANAOFUATA MAFUNDISHO YA WANADAMU.

8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mathayo 15:9

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ufunuo wa Yohana 12:17

KAMA HUFUATI SHERIA ZA MUNGU MBINGU UTAISIKIA TU.
Mkuu uyo mwanamke aliyezungumziwa kwenye ufunuo ndo ELLEN G White?
 
Okay

Okay okay vyema, Wayahudi hawamtambua BWANA YESU Kama MASIHI hivyo inabidi tuwafate nasisi tusiamini kwakua Wokovu watoka kwao?
Mungu kashajibu Hilo swali ,

Warumi 3

Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
 
Kwanini mitume wa kanisa la kwanza hawakua wakiabudu siku ya sabato?
Hao mitume labda kina mwamposa ,Geo Devi, Mashimo, Mwingira ,Nabii Tito

Ila mitume walikuwa wanaabudu siku ya Sabato

Mitume wa Yesu hawa hapa

Matendo ya mitume 16:12-13

“Na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Hata siku ya Sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.” Mdo. 16:12,13.

Hapana. Mitume wasingeweza kufanya jambo lo lote kinyume na Bwana wao! Siku ya Sabato walikuwa wakienda kusali.
 
Maelezo mengi mno siwezi yasoma mkuu! Okay it means SDA pekee ndio wataenda Mbinguni kwakua wanaishiaka Sheria ya MUNGU tofauti na WAKRISTO wa madhehebu mengine?
Uvivu wa kutosoma ndio maaana kina mackenzie, mwamposa,Geo Devi, Mashimo,Mwingira wanawaibieni

“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.” Isa. 66:22,23.

Watu wote wataendelea kuhudhuria mbele za Mungu na kumwabudu kila Sabato, hata katika mbingu na nchi mpya ambazo Bwana atazifanya!

Yesu amekuwa wazi sana juu ya jambo hili kwamba hakuja duniani kubadili amri za Baba yake.

Alikuja kubadili mioyo ya wanadamu ili wamgeukie Mungu na kufanyika watoto wake.

“Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu” (Yn. 1:12
 
Okay

Okay okay vyema, Wayahudi hawamtambua BWANA YESU Kama MASIHI hivyo inabidi tuwafate nasisi tusiamini kwakua Wokovu watoka kwao?
Hao Wayahudi kutomtambua Mungu hakuzuiii uaminifu wa Mungu

Je unajua mji mtakatifu Yerusalemu mpya malango yake yameandikwa majina 12 ya kabila za Israeli?

Je unajua misingi yake imendikwa majina 12 ya mitume wa Yesu?

Je hatuingia sababu Ni WAYAHUDI?

Someni Maandiko acheni kutapeliwa na kuibiwa na hawa wajanja wa mjini
 
Ili utimize Sifa za kuwa Mnyama wa ufunuo 13

Lazima utimize Sifa zote zilizoainishwa Pale

Kitu hiki walikifanya kina Sir Isack Newton , Martin Luther,John Knox, John Calvin, na wanamatengenezo wengi, wakisema waziwazi UPAPA NDIO MPINGA KRISTO baada ya kusoma Maandiko ya DANIEL NA UFUNUO
 
Back
Top Bottom