Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

Hakuna kanisa lililo sahihi yote yana mambo ya kipagani. MUNGU atamhurumia Jacob tu.... Na ataingia AGANO tena na uzao wake tu... Na wote waliohusika ANADili nao sambamba


USIWE MBISHI SANA KANISA LA MUNGU HALIWEZI KUANGUKA.

TAFUTA KUJUA HAPO KWENYE UFUNUO 12.
JE HAO WALIOSALIA NI AKINA NANI??????
WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU
NA KUWA USHUHUDA WA YESU.....

Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;
UFUNUO 12.17.
 
Hiyo mithali unayong'ang'ana nayo ni nani aliiandika ikasomeka kimpangilio hivi?
 
Usabato ni kikundi cha itikadi
Hivyo ni kawaida yenu na itikadi zenu kila siku kuusema ukatoliki

Kati ya makundi yaliyoanzishwa Marekani baada ya utabiri wa William Miller kwamba ujio huo eti, utatokea tarehe 22 Oktoba 1844, lililoenea zaidi ni lile la Waadventista Wasabato (mwanzo rasmi mwaka 1863) ambalo kwa sasa lina waumini zaidi ya 17 milioni duniani kote.

Usabato lasmi ulianzishwa lasmi 1863 na huyo mzungu hapo juu 🤣🤣🤣
 


Mimi sijadili maswala hayo.

Mimi napenda tujadili bibilia.

Tuje na evidence za bible.

Ukija na maneno Nje ya bible na ukashambulia kanisa ninakushangaa.

NJOO NA BIBLE LETE NENO LA MUNGU.
 
Mimi sijadili maswala hayo.

Mimi napenda tujadili bibilia.

Tuje na evidence za bible.

Ukija na maneno Nje ya bible na ukashambulia kanisa ninakushangaa.

NJOO NA BIBLE LETE NENO LA MUNGU.
Mimi nimeongelea usabato ulivyoanzishwa kwani kuna ubaya hapo?
 
Sasa mkuu ipi dini au dhehebu la haki ambalo tunapaswa kuabudu maana hayo makanisa yote yamefata mpaka siku ya sabato Kwa waroma na huku tena inadaiwa hta uislam ni wao waanzilishi kimbilio la mwanadamu ni wapi
Kanisa Ni mkusanyiko wa watu, sio jengo
 
Mimi nimeongelea usabato ulivyoanzishwa kwani kuna ubaya hapo?
Ibada ya Sabato, imeanzishwa na Mungu mwenyewe , wewe ulichoweka hapo Ni historia ya usajili wa SDA, lakini pia William Miller hakuwahi kuwa SDA,

Watunza sabato wapo karne na karne , wamekuwa wanapitia transition period ,


Unawajua WAWALDENSIA ? Papa aliwaua na wengi walikimbilia milimani


Yesu aliwafundisha mitume wake kwamba hawatakiwi kufanya lolote siku ya Sabato lakini kilichoamuriwa “kisheria.” Mathayo 12:12.

Aliwaelekeza mitume wake kwamba Sabato kwa maombi ilipaswa kuangaliwa miaka 40 baada ya ufufuo wake. Mathayo 24:20 (kukimbia kwao kulitokea mwaka 66 BK).

Wanawake watauwa waliokuwa wamekaa pamoja na Yesu kwa uangaifu walitunza siku ya saba baada ya kifo chake. Luka 23:56.

Miaka thelathini baada ya ufufuo wa Kristo, Roho Mtakatifu kwa wazi anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 13:14.

Paulo, mtume kwa Mataifa, aliita “siku ya Sabato” mwaka 45 BK. Mdo 13:27. Je, Paulo hakujua? Au tuwaamini walimu wa kisaa, wanaodai kwamba ilikoma kuwa Sabato wakati wa ufufuo wa Kristo?

Luka, mwanahistoria wa Kikristo aliyevuviwa, akiandika baadaye mwaka 62 BK, anaiita “sikuya Sabato.” Mdo 13:44.

Waongofu Mataifa waliita Sabato. Mdo 13:42.

Katika Baraza kuu la Kikristo, mwaka 52 BK, mbele ya mitume na maelfu ya wafuasi, Yakobo anaiita “siku ya Sabato.” Mdo 15:21.

Ilikuwa ni desturi kuwa na mikutano ya maombi katika siku hiyo. Mdo 16:13.

Paulo alisoma maandiko katika mikutano ya hadhara katika siku hiyo. Mdo 17:2-3.

Yalikuwa ni mazoea yake kuhubirikatika siku hiyo. Mdo 17:2.

Kitabu cha Matendo ya Mitume hutupatia kumbukumbu ya yeye kuendesha mikutano themanini na nne katika siku hiyo. Angalia Mdo 13:4, 44, 16:13, 17:2, 18:4, 11.
 
The Seventh-day Adventist Church had its roots in the Millerite movement of the 1830s to the 1840s, during the period of the Second Great Awakening, and was officially founded in 1863. Prominent figures in the early church included Hiram Edson, Ellen G. White, her husband James Springer White, Joseph Bates, and J. N. Andrews. Over the ensuing decades the church expanded from its original base in New England to become an international organization. Significant developments such the reviews initiated by evangelicals Donald Barnhouse and Walter Martin, in the 20th century led to its recognition as a Christian denomination.

Yaani mwanzilishi wenu unasema hakuwahi kuwa msabato bila yeye wewe ungeijua hiyo dini
 
Mleta uzi uko sahihi.

Kwa usahihi zaidi.

Milima saba ni falme saba: Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy. In the days when apostle John received the Revelation: five have fallen (falme 5 zimeshaanguka/zimeshapita); Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece; the one is (this is Rome); the other is not yet come (this is the papacy). When he comes he must continue a short space (1,260 prophetic days which is equal to 1,260 years).

Revelation 17:11 And the beast that was, and is not, even he is the eighth, and is of the seven, and goeth into perdition. Huyu beast ambae ni the eighth and is of the seven, ni upapa "uliofufuka" baada ya kejeruhiwa mwaka 1798 (mwisho wa ile miaka 1,260). Jeraha la upapa lilianza kupona kwa kiasi fulani in 1929. Jeraha la upapa limepona kabisa after 2020 (222 years after 1798).

So the woman who sits on the seven mountains is spiritual Babylon. Spiritual Babylon ana sit on Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy (including the resurrected Papacy).

The great red dragon (wa Ufunuo 12) ni Satan. Note that ana seven crowns on his seven heads. The seven heads are Egypt, Assyria, Babylon, Medo-Persia, Greece, Rome, Papacy (including the resurrected Papacy). Satan huwa anaitwa the prince of this world. Satan yuko nyuma ya falme za dunia ambazo zina mwasi Mungu wa Biblia. Spiritual Babylon ana sit kwenye hivyo vichwa saba.

Ukifika Ufunuo 13, utaona mnyama mwingine, ambaye ana crowns kwenye pembe zake kumi (na sio kwenye vichwa vyake saba). Note that mnyama huyu wa Ufunuo 13, ni kichwa kimoja kati ya vichwa saba (vyenye crowns) vya the red dragon. Kwenye time period ya utawala wa mnyama wa Ufunuo 13, wakati wa utawala wa zile falme 6 (vichwa 6) umeshapita. Mnyama wa Ufunuo 13 anatawala pamoja na wafalme 10 (pembe 10, ndio maana pembe zake 10, zina crowns 10). Mnyama wa Ufunuo 13 ni upapa, na pembe 10 ni falme 10 za Ulaya zinazo shirikiana na upapa (angalia pia Ufunuo 17).

Watoto wa spiritual Babylon ni spiritual Egypt, Sodom, Tyre, na miji/mataifa mingine ya kidunia yaliyo mwasi Mungu wa Biblia. Watoto wa spiritual Babylon ni pamoja na makanisa yaliyojitenga na upapa, lakini bado yanafuata mafundisho ya upapa (kama kusema siku ya sabato imebadilishwa na kuwa Jumapili, kusheherekea 25th December kama Christmas etc).

Kumbuka Babylon (Babel) ilianza toka Genesis 11. 666 ni namba ya uasi wa mwanadamu dhidi ya Mungu wa Biblia. Ni namba ya uasi wa mamlaka/ufalme wa mwanadamu dhidi ya mamlaka/ufalme wa Mungu wa Biblia. Uasi huo unakataa the holy covenant and mercy, and the gospel of Jesus Christ. Uasi huo unakataa amri za Mungu (YAHWEH), na injili ya Bwana Yesu Kristo (Bwana Yahushua Mashiach). Uasi huo unakataa sabato ya siku ya saba (Jumamosi).

Soma pia vitabu vya Ranko Stefanovic (huyu ni SDA), Revelation of Jesus Christ, na Plain Revelation (google utaviona). Ni vizuri sda wote watanzania, wanaojua kiingereza kuvisoma hivi vitabu. Ranko Stefanovic amepatia vizuri zaidi (sehemu nyingi sana) kuliko Uriah Smith (huyu nae ni SDA), kwenye kitabu chake cha Daniel and the Revelation.

Ukisoma vitabu hivyo vya Ranko Stefanovic, utaelewa vizuri sana sana sana kuhusu kitabu cha Ufunuo, na 666. Kuna sehemu chache sana ana kosea: 1) Revelation 4 ina maanisha YAHWEH yuko kwenye his holy temple in heaven, na YAHWEH anatawala, na anaabudiwa (YAHWEH reigns, and is being worshiped), so it is not necessarily a judgment scene. 2) Parapanda ya 5 ina ambatana na kuja kwa roho ya mpinga kristo duniani, pamoja na ufalme wa kiroho wa mpinga kristo (yaani ufalme wa mnyama wa Ufunuo 13, ambao ni the papacy). Parapanda ya 6 ina ambatana na ujio wa roho ya nabii wa uongo, pamoja na ufalme wa kiroho wa nabii wa uongo wa Ufunuo 13 (yaani taifa la Marekani).

3) Kuto kupatikana kwa tiara yenye title ya Vicarius Filii Dei haimaanishi kwamba title hiyo haipo. Title hiyo ni mfano wa kujikweza kwa mwanadamu dhidi ya Mungu. Kwa hiyo title hiyo ni aina ya 666. Haijalishi namba zake zinakuwa au haziwi 666 (ingawa incidentally zina kuwa 666).

Ranko Stefanovic amepatia sana zaidi ya mafundisho ya sda wenzake kuhusu story ya kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni. Ila naona ana ogopa kuwa muwazi kusema kwamba Shetani alianguka baada ya wiki ya uumbaji. Kwa sababu akisema wazi atakuwa anapingana na mafundisho ya sda wenzake.

Mapungufu ya mafundisho ya kanisa la sda ni haya:

1) Shetani na malaika zake hawa kuanguka kabla ya wiki ya uumbaji. Kwa sababu malaika wote (including Lucifer, ambae baadae ali muasi Mungu) waliumbwa siku ya pili ya wiki ya uumbaji.

2) Hakuna viumbe wengine kama binadamu kwenye sayari nyingine (kama sda wengi wanavyo fundisha).

3) "The Day of Atonement" ni tofauti na "the Day of Judgment". New tastement fulfilment of the Day of Atonement inaanza baada ya kufufuka na kupaa kwa Bwana Yesu, na inaisha at the end of probation period (karibia kabisa na ujio wake wapili).

4) Wabatize kwa staili waliyoitumia mitume wa Yesu, mtu ana inama kidogo kwa mbele, huku amesimama, huku akidumbukia kabisa kwenye maji. Wasibatize kwa staili ya mtu kalala kwa mgongo, wana mshika na kumdumbukiza kwenye maji.

5) Wasi wapinge sda wenzao, wanao sema kwamba Yesu alizaliwa during the Feast of Tabernacles. Kwa sababu kiukweli Yesu alizaliwa during the Feast of Tabernacles.

6) Wakubali kwamba hawa hodhi ukanisa wa kweli, na kwamba endapo kuna wasabato wanaofuata biblia ambao sio sda, wasabato hao hawana tatizo.

7) Waumini wa sda wawe pia na tabia nzuri kwenye maisha yao.

8) Baadhi ya mafundisho ya mama Ellen White ni maoni yake, na sio vitu alivyo viona kwenye maono (visions). Kwa hiyo baadhi ya mafundisho yake yanaweza yasiwe sahihi. Of course mama Ellen White yuko sahihi kwenye mafundisho yake mengi.

9) Ni vizuri wakristo weusi wakajua prophesies mbali mbali za kwenye Biblia, zinazo ongelea kuhusu injili kuja Afrika. Wakristo weusi, tu avoid a white/Eurocentric view of the bible, na tuwe na a true view of the Bible, which is a biblical centric view of the bible. Wakristo weusi tujaribu pia kuwa na makanisa huru yanayojitegemea (tushirikiane na watu wengine, lakini tusiwe tegemezi kwa watu wengine).

Sda wako sahihi kabisa kabisa kabisa kwamba sabato ni siku ya saba (Jumamosi), na kwamba Bwana Yesu Kristo hakubadilisha siku ya sabato. Na kwamba mpinga Kristo ndiye aliebadilisha siku ya sabato kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza ya wiki.

Moral of the story ni: Mkristo yeyote anatakiwa kusikiliza mafundisho yanayoendana na biblia, usisikilize mafundisho ambayo hayafuati mafundisho ya biblia (hata kama ni mafundisho ya dhehebu lako).

So injili ya kweli, ni kwamba Utatu Mtakatifu upo, amri 10 zipo (hazikubadilishwa), sabato ni siku ya saba (Jumamosi), tufuate mafundisho ya Bwana Yesu Kristo kama Biblia inavyosema, na Biblia ni kitabu kitakatifu cha YAHWEH (Mungu wa Biblia). Ukristo ndio dini ya ukweli, dini nyingine zote ni za uongo.

Any way tuendelee na shughuli zetu za maisha hadi siku ya mwisho ya dunia, wakati huo huo tukiendelea kumkumbuka Bwana Yesu Kristo hadi siku hiyo atakapo rudi.
 
Unakopi Wikipedia hujui lolote kuhusu William Miller

Narudia Tena Willam Miller hakuwahi kuwa SDA Wala kusali siku ya Sabato had anakufa


Kasome vzr historia


Na nimekuwekea hapo Watunza Sabato toka Enzi na Enzi
 
Unakopi Wikipedia hujui lolote kuhusu William Miller

Narudia Tena Willam Miller hakuwahi kuwa SDA Wala kusali siku ya Sabato had anakufa


Kasome vzr historia


Na nimekuwekea hapo Watunza Sabato toka Enzi na Enzi
Dini imeanzishwa na binadamu 1863
 
Nasubiri ili ni-note kitu. kila neno yatupasa kulipima, yawezekana kuna asilimia flan za ukweli, hizo ndio nazitafuta
TUANZIE HAPA...


Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita." (Ufunuo13:17,18)

[emoji3591]Mambo mawili makuu sana ya mamlaka hii ya Mnyama yanafunuliwa katika Ufunuo
13. "Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio
huru kwa watumwa, watiwe CHAPA [ALAMA] katika mkono wao wa kuume, au
katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala
kuuza, isipokuwa ana chapa [alama] ile, yaani, jina la Mnyama yule, au hesabu ya
jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya
Mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na
sita." Ufunuo 13:16-18.


Kwa mujibu wa Ufunuo 13:17, hesabu ya jina lake itakuwa pia ni hesabu ya
mwanadamu.

[emoji3591] Bila shaka inamhusu mtu yule anayeiongoza mamlaka ile ya Mnyama.
Njia ya zamani ya kuipata hesabu ya jina ni kuchukua thamani ya tarakimu za herufi zote na kuzijumlisha ili kupata jumla yake. Kama tunataka kutumia kipimo hicho kwa Upapa, yatupasa kupata jina la kiofisi [cheo] la Papa, ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo.

[emoji3591] Kama hiyo ni hesabu ya mtu, basi, bila shaka ingekuwa ni ya mtu yule
anayeuongoza mfumo ule [wa dini].
Ni jambo la kuvutia macho kuona kwamba kuna cheo rasmi cha Kilatini cha Papa, cheo ambacho amepewa na Kanisa lenyewe. Cheo hicho kinaonekana tena na tena
katika vitabu vya Kanisa la Roma. Lakini katika gazeti la kila juma la Kikatoliki liitwalo, OUR SUNDAY VISITOR, la Aprili, 1915, tunao usemi wa kuvutia
unaosema kwamba herufi ya cheo hicho rasmi zimeandikwa katika kofia yake ya Kiaskofu (miter or mitre).

[emoji1542] Hapa ni dondoo lenyewe: "Herufi zilizoandikwa katika kofia ya Papa ni hizi; VICARIUS FILII DEI, ambacho ni Kilatini cha 'ALIYE BADALA YA MWANA WA MUNGU' (VICAR OF THE SON OF GOD).

[emoji3591]Wakatoliki wanashikilia [wanaamini] kwamba Kanisa ambalo ni jamii inayoonekana
ni lazima liwe na kichwa kinachoonekana; Kristo kabla ya kupaa kwake kwenda
mbinguni, alimchagua Mtakatifu Petro kuwa kama Mwakilishi wake. Kwa hiyo,
Askofu wa Rumi kama kichwa cha Kanisa, alipewa cheo cha 'Aliye Badala ya Kristo'
(Vicar of Christ)." Kwa siku hizi kofia ya papa [tiara] haina cheo chake cha Kilatini,
lakini maneno hayo yanatumika katika sherehe za kumtawaza kila Papa mpya anayevikwa taji [kofia hiyo]. Basi, tukiwa na cheo hiki rasmi cha Papa mkononi mwetu, tunaweza kuendelea kutumia kipimo hiki cha Maandiko haya.

[emoji1542]Tunaipataje hesabu ya jina lake? Kwa kupata thamani ya tarakimu za Kirumi za cheo chake cha VICARIUS FILII DEI, tunaifikia hasa hesabu hiyo halisi, 666.

[emoji1542]Angalia jinsi hesabu hizo zilivyofanywa hapa
chini, kila herufi ikipewa thamani ya tarakimu yake:
[emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]

V ................. 5 F ..................0 D ............. 500
I................... 1 I ...................1 E.................. 0
C ............. 100 L ...............50 I....................1
A ................. 0 I ...................1 501
R ................. 0 I....................1
I .................. 1 53
U au V......... 5
S ...................0
112
112 + 53 + 501 = 666

[emoji1542]Mmoja anaweza kubisha kwamba hilo linaweza kuwa ni jambo linaloweza kutokea
kwa nasibu. Tunakubali ya kwamba upo uwezekano kwa jambo kama hilo kutokea kwa nasibu tu, kama tungekuwa na pointi moja hiyo tu ya utambulisho ya
kuitegemea. Lakini, basi, ukweli ni kwamba, hiyo ni pointi ya KUMI miongoni mwa orodha ndefu ya ishara za tabia yake ambazo Biblia huzitumia kuitambulisha mamlaka hiyo ya Mnyama.

[emoji3591]Hii inaongezea tu uzito na nguvu kwa yale ambayo tayari
yamekwisha kusemwa kwa kuzitumia [ishara zile] kuionyesha mamlaka hiyo ya Papa.
Ni uthibitisho wa kilele pamoja na zile ishara nyingine zote zilizowekwa kwa wazi sana katika Maandiko.

[emoji3591]Alama Hii ----- Ni Udanganyifu Mkuu
Sasa tuko tayari kuchukua hitimisho la kilele cha udanganyifu huu kwa kadiri
mamlaka hiyo ya Mnyama huyo inavyohusika.

[emoji3591]Tayari tumekwisha jifunza ya kwamba
mamlaka hii ingeweka mafundisho mengi ya uongo kinyume na mafundisho makuu ya kweli zake Mungu. Kwamba [mamlaka hiyo] ilikuwa ni mchanganyiko wa mawazo ya kipagani na mafundisho ya dini ya Kikristo ambayo yamekusanywa pamoja kwa hali inayoleta machafuko [kuchanganyikiwa], yanayoitwa vyema kama
"BABELI" katika Maandiko.

[emoji1542]Mafundisho machache ya uongo yanaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo: badala ya
Neno la Mungu, imeweka MAPOKEO; badala ya Roho Mtakatifu, imemweka PAPA;
badala ya toleo moja tu la Kristo, imeweka MISA [toleo la kila siku]; badala ya
ubatizo, imeweka KUNYUNYIZA; badala ya Meza ya Bwana, imeweka MKATE
UNAOBADILIKA KABISA NA KUWA MWILI NA DAMU HALISI YA YESU
(Transubstantiation); badala ya Sheria ya milele ya Mungu, imeweka SHERIA
ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO [Amri Kumi]; badala ya Zaka; imeweka KODI
[Ushuru] na INDULGENSIA [kuuza vyeti vya msamaha wa dhambi]; badala ya
mauti, imeweka MAHALI PA KUTAKASIA DHAMBI au TOHARANI (Purgatory);
badala ya Muhuri wa Mungu, imeweka ALAMA [CHAPA] YA MNYAMA.

[emoji1542][emoji1484]Hapa tunashughulika hasa na ALAMA YA MNYAMA. Katika Ufunuo 14:9,10
tunasoma hivi, "Mtu awaye yote akimsujudu huyo Mnyama na Sanamu yake, na
kuipokea chapa [alama] katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye
atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo
kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake."

[emoji3591]Hili ni jambo la KUFA NA KUPONA. Ni lazima tujue kabisa alama hii ni ya kitu gani hasa na jinsi tunavyoweza
kuikwepa.
Kwanza tunaona katika Biblia ya kwamba ALAMA hii daima iko kinyume na
MUHURI WA MUNGU. Katika Ufunuo 7:2,3, tunajifunza ya kwamba Muhuri wa
Mungu unawekwa juu ya kipaji cha uso sawasawa tu na ile Alama ya Mnyama
inavyowekwa juu ya vipaji vya uso. Vitu hivyo viwili [Muhuri wa Mungu na Alama
ya Mnyama] vinaonekana kuhitilafiana moja kwa moja na kila kimoja kiko kinyume
na kile kingine. Vyote viwili vinapokewa katika kipaji cha uso na mkononi. *_>>>


NITAENDELEA (Nasumbuliwa kidogo na tonsils)
 
Huu Ni mwaka 1863 pale Israel Yerusalemu

Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; NA SIKU YA SABATO AKAINGIA KATIKA SINAGOGI KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE, akasimama ili asome.
Kwa hiyo ndio Dini yenu ilipoanzishwa
 
Kwa hiyo ndio Dini yenu ilipoanzishwa
Kasome Mwanzo 1 Mungu anaanzisha Ibada ya Siku ya sabato


Mngekuwa mnasoma Biblia kwa utulivu Wala msingekuwa mnatapeliwa na kina mwamposa


Nakupa challenge hii ili ujue huko ulipo unaibiwa na kudanganywa


Mwaka 30AD Yesu alitoa utabiri huu kabla hajapaa

Mathayo 24:20

“Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.”


Huu unabii ulitimia mwaka 70AD , yaani miaka 40 baada ya Yesu kuwa ameshapaa mbinguni


Cha ajabu Sasa ,manabii kina mwamposa,Geo Devi,Mwingira , Gwajima ,n.k ,Mapadri wanawadanganyeni SABATO iliishia msalabani

Kama Ni hivo Je Yesu kwanini anatoa unabii wa miaka 40 mbele baada ya kupaa ,Je hakujua Sabato imekomea msalaban Kama Wala nguruwe kina mwamposa wanavyowadanganyeni?


Muwe mnahoji na kuuliza ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…