Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kwenye nchi yoyote ya kidemokrasia kunapokuwa na Katiba iliyoandikwa hiyo katiba inakuwa na mamlaka makuu juu ya Taifa zima. Sio Spika, Rais hata Jaji mkuu anaweza kuwa na mamlaka dhidi ya Katiba.
Mamlaka ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanapatikana kwenye ibara ya 64(5) ambayo yameweka bayana kuwa hakuna mtu au sheria yoyote itayotungwa itakuwa kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Kama ninakosea niko tayari kukosolewa, ibara ya 71 (1) (e) imeweka bayana kuwa mbunge atapoteza ubunge wake kama uanachama wake utakoma kwenye chama kilichompa ridhaa ya kugombea ubunge. Hii ni wazi wabunge 19 wa CHADEMA waliofukuzwa sio wabunge halali hata kama waliapishwa kwa kanuni za bunge. Na spika anawatetea kwa sheria gani, au kanuni gani ambazo zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Pia inasikitisha sana Spika wa bunge kudharau maoni ya wastaafu. Kwani ibara ya 71(1)(e) imefutwa? Kwani hii ibara haipo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka spika Ndugai awe anadharau maoni ya wastaafu na kudai hawajui kinachoendelea? Nini hicho kinachoendelea? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebadilishwa? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina mamlaka juu ya spika?
Jambo la msingi ambalo Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa akubumke ni kuwa bunge ni wananchi, ndio maana tunatuma wawakilishi wetu huko,la sivyo kila mtanzania angekuwa mbabe na kujiamulia anavyotaka. Na hakuna mtu kwenye nchi hii aliye juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.