Je, Katiba yetu inamruhusu Rais Samia kukaa miaka 15 Ikulu?

Na mbona Warusi wanamkubali? Anafanya madudu yepi???
 
Samia hajakaimu miaka ya mtu yeyote, ni Rais kamili wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba na anaweza kugombea tena urais kadri katiba inavyosema.
Kule kwao hata umwenyekiti wa kitongoji uruhusiwi kushika fomu ya kugombea. Huko ni kitonga
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kule kwao hata umwenyekiti wa kitongoji uruhusiwi kushika fomu ya kugombea. Huko ni kitonga
Ukiwa Mzanzibari unaruhusiwa, sisi Tanganyika tulijichanganya wenyewe na yote kwa sababu ya Nyerere alijiona mjanja sana alifikiri vile alivyofanya eti serikali ya Tanganyika ipo humo humo ndani ya serikali ya Muungano ndio automatically tutakuwa tukiitalawa Zanzibar sasa kibao kimegeuka maana katiba haikusema kama rais wa Muungano lazima atoke Tanganyika.
 
Ifike mahali Rais wa Zanzibar atoke Tanganyika
 
Prof Kabudi soma hii maneno
 

Heshima kwako Pascal
Ni kweli mleta mada amekosea kwa kutumia neno kukaimu Uraisi
Pamoja na hilo, ameleta hoja nzuri na fikirishi ( atleast kwa tusio na uelewa wa kutosha wa Katiba, japo najua kuna wengine ni wasomi wa sheria na hawana jibu la uhakika kwenye hili swali)
Mleta mada katoa mifano iliyoibua hoja yake ( maraisi wa Zambia, Burundi nk) hivyo ni swali lenye mashiko na lenye reasoning nyuma yake.
Ni kweli watanzania wengi ni viazi (na huo ndiyo mtaji wa CCM) Na watu ‘viazi’ wanazidi kuongezeka humu jukwaani, lakini swali lililoulizwa hapa lina mashiko maana sio kila mtu ana fursa ya kuijua katiba kama uijuavyo wewe.
Nikuombe sasa atleast utuambie katiba inasemaje kwenye hili au specifically kwanini Mh Rais Samia hawezi kugombea 2030.
 
Katiba sio bibilia inaweza kufanyiwa marekebisho soon tukakaa sawa
 
Mleta mada umetumia neno “kukaimu” vibaya na neno hilo linaweza kupotosha mada nzima. Kukaimu ni kushikilia madaraka kwa muda. Rais SSH alikaimu siku toka JPM alipokufa mpaka siku anaapishwa! Baada ya kuapa alishika madaraka ya uRais.

Katiba ya Tanzania inatambua muhula kuwa miaka mitano na hairuhusu kuongoza kwa zaidi ya mihula miwili, bila kujali mhula mmoja kati ya hiyo miwili ni miaka mitano kamili au pungufu. Ndio maana inaeleza kitakachotokea kama Rais aliye madarakani atakufa na atarithiwa na makamu wake. SSH angekuwa na nafasi ya kuongoza zaidi ya miaka 10 kama Rais JPM angekuwa amekuwa madarakani kwa zaid ya robo tatu ya muhula (JPM alitufa takribani miezi 6 baada ya kuapishwa) na hivo kipindi kilichobaki kitahesabiwa kwa Rais SSH (ndio maana inaitwa Serikali ya awamu ya sita)!! Na awamu ya Rais haizidi mihula miwili.

Namna pekee ya SSH kuwa mgombea wa 2030-35 ni kufanya kama wengine walivofanya - kutumia Bunge kubadilisha matakwa ya Katiba.

Hii ni awamu ya sita na kama anataka kuwa mgombea 2030 aanze kusema hii bado ni awamu ya tano na kwamba bado anakaimu madaraka ya Rais (jambo gumu kusema kwa sababu hawezi kuwa anakaimu wakati yeye sio Makamu wa Rais kama Katiba inavyotaka).
 
Nimefurahi sana,
Na nikupongeze sana la maana waTanzania wengi pia wanahitaji elimu ya Afya ya akili kwa kuwa hawajui madhara ya minyoo inavyoweza kuathiri ubongo na huchukua mpaka miaka ishirini kuja kuona madhara, kwa hiyo waTanzania wengi wanahitaji sana elimu ya afya na namna bora ya kunywa dawa za minyoo kwa kuzingatia ushauri wa daktari. Hivi ushauri wa daktari wako kuhusu dawa za minyoo unaufuata...?
Nakupa pole sana.
Eneo lako la ujasiri, sio eneo langu la ujasiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…