Mkuu
Dr Akili, hakuna utata wowote. Mambo ya haki ya
kuchaguliwa tena yanaongozwa na ibara ya 9 kufungu cha 15 cha sheria namba 34 ya mwaka 1984 iliyofanyiwa mapitio mwaka 1994
na kuingizwa kwenye Ibara ya 40 ya Katiba, kifungu kidogo cha 4, imeelekeza vizuri na wazi kabisa bila utata wowote.
4) "Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu".
Hii maana yake, kwa vile Samia anashika madaraka kwa kipindi cha zaidi ya miaka mutatu, hivyo hii inahesabiwa ndio awamu yake ya kwanza, bado anayo fursa ya awamu nyingine moja ya mwisho.
Endapo JPM angechomoka baada ya kutumikia urais kwa miaka 2 na nusu, hivyo Samia kushika kwa kipindi kisichozidi miaka 3. Then kipindi hicho Samia angehesabiwa kuimalizia ngwe ya JPM, hivyo Samia angekuwa na fursa za kugombea awamu zake zote mbili, kuanzia 2025-2035.
Hivyo hakuna awamu ya less than 3 years .
P