Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema.

Je, Mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe? Na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo?
 
Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema ,je!mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe?na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo.
Mwanamke hatoi talaka bali huomba talaka na msingi wa yote haya huanzia kwenye
Kutongozwa
Kuchumbiwa
Kutolewa mahari
Kuolewa nk
Kama hayo yakifanywa na mwanamke basi ana haki pia ya kutoa talaka
 
Ukiwa vizuri mwanamke na ukiwa na ushahidi pasi na shaka nenda mahakamani kaombe kutoa talaka, mali zilipatikana ndani ya ndoa unapiga pasu,

Sijui ndo hivyo 🤣🤣🤣
 
Talaka hutolewa na mahakama pekee na si mume wala mke.

Mwanandoa anakwenda mahakamani kuomba mahakama ivunje ndoa yake kwa kuwa mwenzake amekiuka masharti na kufanya ndoa iharibike vipande vipande visivyoweza kutengenezeka tena.

Mahakama ikiridhika na ushahidi wake, inakubali ombi lake na inavunja ndoa hiyo kwa kutoa talaka. Kwa hiyo mwanandoa yeyote (mume au mke) anaweza kuomba mahakama ivunje ndoa yake, talaka inatolewa na mahakama.
 
Kulingana na uzoefu na nimeshawahi kuona pia nadhani inategemea na dini zenu. Dini ya kikristo meanamke anaenda kuomba talaka mahakamani. Lakini dini ya kiislam mwanamke nmeona anaweza kuandika talaka na kumpatia mumewe tu iwe mbele ya mashahidi.

Ila talaka ya kuandika mke Huwa inakua nyepesi kama hakuna Mali za kudai kama zipo Mali ni lazima swala liende mahakamani
 
Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema ,je!mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe?na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo.
Anaeolewa ndie anaepewa talaka

Mwanamke hatoi talaka, ila anapewa yeye
 
Kulingana na uzoefu na nimeshawahi kuona pia nadhani inategemea na dini zenu. Dini ya kikristo meanamke anaenda kuomba talaka mahakamani. Lakini dini ya kiislam mwanamke nmeona anaweza kuandika talaka na kumpatia mumewe tu iwe mbele ya mashahidi. Ila talaka ya kuandika mke Huwa inakua nyepesi kama hakuna Mali za kudai kama zipo Mali ni lazima swala liende mahakamani
Hizo za dini sio halali.
 
Back
Top Bottom