Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Mke au Mahakama ( iwe ya kidini au ya kiserikali ) hawatoi talaka bali wanaweza kuvunja ndoa.

Kuna tofauti kuvunja ndoa na kutoa talaka ..Anayetoa talaka ni Mume tu na si vinginevyo, kwasababu ndie pekee aliyeimiliki hiyo talaka.

Mke wala Mahakama hawaimiliki talaka hivyo hawawezi kutoa kitu wasichokimiliki..
 
Talaka halali inatolewa na mahakama, hakuna mtu yoyote mwenye uhalali w kutoa talaka.Kwahiyo hata na hizo wanazotoaga wanaume wa kiislamu sio halali.
Kaka Acha kupotosha mambo....Uislamu Una mambo yake na Sheria zake,mwanaume ana haki ya kutoa talaka na mwanamke anaweza omba kuachwa au kupewa talaka.....na ikitokea migogoro yoyote Kati ya wanandoa basi kama kuna mahakama ya kadhi ambayo inaendeshwa na misingi ya Dini ya kiislamu ndio ina haki ya kuamua maswala ya ndoa na mirathi Kwa mujibu wa Sheria za kiislamu,na sio hizo mahakama za kawaida
 
Lakini wanazitumia sana wakishaita mashekhe fasta tuu shughuli imeisha
Talaka Kwa waislamu wala haihitaji sheikh inahitaji mume Tu kwani yeye ndio muoaji....na talaka si lazima iandikwe Bali mume akitamka Tu kuanzia leo Fulani sio mke wangu basi imepita hiyo....kuandika kumekuja Tu kama ushahidi ambao mwanamke atakuwa nao endapo ataenda ktk familia Yao huenda akaulizwa tuonyeshe talaka
 
Kulingana na uzoefu na nimeshawahi kuona pia nadhani inategemea na dini zenu. Dini ya kikristo meanamke anaenda kuomba talaka mahakamani. Lakini dini ya kiislam mwanamke nmeona anaweza kuandika talaka na kumpatia mumewe tu iwe mbele ya mashahidi. Ila talaka ya kuandika mke Huwa inakua nyepesi kama hakuna Mali za kudai kama zipo Mali ni lazima swala liende mahakamani
Mwanamke hatoi talaka Bali anaomba kuachwa au anaomba kupewa talaka
 
Hivi bongo ndo kusema kuna kuoa na kuolewa?

Kwa wenzetu jamii yenye uelewa wa hali ya juu ya mambo kuna “kuoana” tu

Kuridhiana.

Sio kuridhia na kuridhiwa la hasha!
 
Hivi bongo ndo kusema kuna kuoa na kuolewa?

Kwa wenzetu jamii yenye uelewa wa hali ya juu ya mambo kuna “kuoana” tu

Kuridhiana.

Sio kuridhia na kuridhiwa la hasha!
Sio uelewa ni utaratibu wao wa kihuni
 
Ukiwa vizuri mwanamke na ukiwa na ushahidi pasi na shaka nenda mahakamani kaombe kutoa talaka, mali zilipatikana ndani ya ndoa unapiga pasu,

Sijui ndo hivyo 🤣🤣🤣
Mnawazaga mali tu, mwenzenu klyn mambo magum tofauti na alivyofikiria
 
Tuliosoma Cuba tumekuelewa pole sana mkuu yataisha hayo
 
Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema ,je!mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe?na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, katiba yetu ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), inatambua aina kuu mbili za ndoa, yaani ndoa ya mke mmoja na ya wake wangi.

Utofauti upo kwenye taratibu za ufungaji, inaweza kuwa ni Kimila, Kiserikali pamoja na Kidini. Ndoa ni mkataba kama mingine, huvunjwa kulingana na utaratibu uliotumika kuifunga.

Kwa maana hiyo, endapo kuna haja ya kuivunja kama ni ya Kimila zitatumika taratibu za kimila, ya Kiserikali za Kiserikali na Kidini za kidini husika inavyoelekeza.

Swali ni, je ni nani wa kutoa talaka? Jibu liko kwenye utaratibu uliotumika kuifunga ndoa husika.

Kwa mfano, kwa Waisalamu ni mwanaume, Kiserikali wanandoa wote ni sehemu ya mkataba na wanahaki sawa yeyote anaweza kuanzisha mchakato wa kumuacha mwenzie na kwa Wakristo nakuachia wewe unayesoma.

NB: Mahakama inayo nafasi ya kuingilia utaratibu wowote uliotumika kuifunga ndoa, endapo kuna viashiria vya mmoja wapo kutoridhishwa na maamuzi yaliyotumika au yanayozuia kuivunja.
 
Waliofuta jando na unyago walaumiwe sana,,,,,hiki kizazi kinapitia tabu kubwa sana ya kukosa miongozo ya kimaisha!!!!Ni dhahiri kuwa elimu ya mzungu haina maana katika maisha ya kidunia katika kumfanya mwanadamu ayatawale mazingira yake. Asili ya mwanadamu inataka kufutwa kwa nguvu kubwa sana ila haiwezekani.
 
Dunia hii, ni mwanaume pekee mwenye uwezo wa kufikiri vizuri na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Dunia ni mwanaume, mwanamke ni ziada (the other). Na hili ndilo jibu la swali lako.
 
Back
Top Bottom