Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Ukiwa vizuri mwanamke na ukiwa na ushahidi pasi na shaka nenda mahakamani kaombe kutoa talaka, mali zilipatikana ndani ya ndoa unapiga pasu,

Sijui ndo hivyo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hadi mahakamani tena? Kwani mbona upande wa dini kama islam naonaga mwanaume anatandika hadi takala 3bila kwenda mahakamani
 
Talaka hutolewa na mahakama pekee na si mume wala mke.

Mwanandoa anakwenda mahakamani kuomba mahakama ivunje ndoa yake kwa kuwa mwenzake amekiuka masharti na kufanya ndoa iharibike vipande vipande visivyoweza kutengenezeka tena.

Mahakama ikiridhika na ushahidi wake, inakubali ombi lake na inavunja ndoa hiyo kwa kutoa talaka. Kwa hiyo mwanandoa yeyote (mume au mke) anaweza kuomba mahakama ivunje ndoa yake, talaka inatolewa na mahakama.

Sasa hawa nawaonao wanatoa kwa maandishi bila kwenda huko mahakamani hii imekaaje? Nasemea mwanaume
 
Kulingana na uzoefu na nimeshawahi kuona pia nadhani inategemea na dini zenu. Dini ya kikristo meanamke anaenda kuomba talaka mahakamani. Lakini dini ya kiislam mwanamke nmeona anaweza kuandika talaka na kumpatia mumewe tu iwe mbele ya mashahidi. Ila talaka ya kuandika mke Huwa inakua nyepesi kama hakuna Mali za kudai kama zipo Mali ni lazima swala liende mahakamani

Ahaa kwa hiyo kwa upande wa dini inawezekana. Je vigezo gani vinaangaliwa kuwa huyo mwanamke kweli talaka yake imekubaliwa
 
Talaka halali inatolewa na mahakama, hakuna mtu yoyote mwenye uhalali w kutoa talaka.Kwahiyo hata na hizo wanazotoaga wanaume wa kiislamu sio halali.

Nimeshughudia nyingi sana na mwanamke anakubali na anatimka kumbe sio halali?
 
Kuna wanandoa hudhani kuwa watawakomoa wenzi wao Kwa kukataa kutoa talaka ili kuwakomoa wasiwe huru na kuendelea kufurahia maisha na wapenzi wengine kwa uhuru na mali walizochuma,

Kumbe hawajui kuna chombo cha haki mahakama inauwezo wa kutoa talaka halali kabisa.

Na hata ukiitwa na mahakamani ukagoma kujitokeza Kuna utaratibu ukifika talaka inatoleea kwa mwenza mwenye kuhitaji talaka .

Mambo ya kuwekeana usiku nani anayataka?!
 
Halafu jamii haijui iwapo mahakama ndio inayotoa talaka.

People are not informed.

Wanawake wanaonewa hawajui waende wapi wakapate haki zao za talaka.

Wanabaki kuchanganyikiwa.

Ndugu wanawaambia rudi kwa mumeo ,

Sasa urudi vipi Kwa asokupenda?

Urudi Kwa anayekuumiza moyo ?

Urudi Kwa Mwanaume ambaye unajua ukiwa naye usalama wako uko mashakani?

Maisha ni furaha
 
Ukitaka talaka nenda ofisi ya Kata ,

Kamuone afisa ustawi muulize utaratibu wa kupata talaka.

Atakuelekeza,

Atakusikiliza,

Atamwita mwenza na kuzungumza naye,

Kisha atawaelekeza Baraza la usuluhishi,

Aloumizwa akiendelea kutaka talaka kukaa usuluhishi atapewa form namba 3 atapeleka mahakani.

Mahakama wataipokea form ataitwa taratibu za talaka zitaendelea hadi mwisho.

Siku hizi mahakama haicheleweshi maamuzi ya talaka sababu wamegundua mauaji yameongezeka.

Kwa hiyo ni faster tu cheti cha kuachana kinatolewa.

Usimuumize mwenzi wa ndoa yako Kwa makusudi ya kujirudia rudia pamoja na kukuonya mara nyingi.
 
Talaka inatolewa ili uwe huru ujirishe na michepuko yako kwa raha zako [emoji108][emoji108]

Maana ulivyokuwa na mke ilikuwa ili kwenda kwa michepuko hadi umfunge kamba mkeo ,
Umdanganye weee,

Mara nasafiri,

Mara naenda mashambani ambako hakuna network nitarudi jioni,

Mara naingia kwenye kikao/mkutano,

N.k.

Sasa anaonaka akupe Uhuru ikibidi ingiza michepuko ndani muishi kama mke na mume!
 
Back
Top Bottom