Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Je, katika wanandoa mwanamke anaruhisiwa kutoa talaka?

Kuna wanandoa hudhani kuwa watawakomoa wenzi wao Kwa kukataa kutoa talaka ili kuwakomoa wasiwe huru na kuendelea kufurahia maisha na wapenzi wengine kwa uhuru na mali walizochuma,

Kumbe hawajui kuna chombo cha haki mahakama inauwezo wa kutoa talaka halali kabisa.

Na hata ukiitwa na mahakamani ukagoma kujitokeza Kuna utaratibu ukifika talaka inatoleea kwa mwenza mwenye kuhitaji talaka .

Mambo ya kuwekeana usiku nani anayataka?!

Je mahakama ikatoa talaka na mimi nikaendelea kumtaka mke wangu ana mke nae akakubali hii inakuwaje
 
Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema.

Je, Mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe? Na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo?
Nadhan kwa kuwa asilimia kubwa ya ndoa huwa zina maegeo ya kidini ukiacha za kimila au Kiserikal.
Uvunjikaji wake mfano kwa Uislam, Mwanamke hawezi kutoa talata ila anaweza kuiomba au hata kujivua kwenye ndoa na, Mume akatakiwa kuitoa kwa lazma na msimamizi ambaye kwa Tz nadhan ni BAKWATA.
 
Je mahakama ikatoa talaka na mimi nikaendelea kumtaka mke wangu ana mke nae akakubali hii inakuwaje



Swali zuri sana.

Mpaka talaka inatolewa ni ama mmojawapo mfano mke au wote 2 mke na mume mmeudhishana na kuumizana mioyo pakubwa na sasa inahitajika talaka.

Sasa sijaelewa vizuri swali lako;

Kwamba unauliza iwapo mke alidai talaka na mahakama ikaridhia kutoa mkaachana,

Kwamba baada ya muda mke akasamehe akarudisha moyo na kuanza kukurejea au siyo ?

Kama nimekuelewa hivyo!

Chukulia hata kidini mwanamke akipewa talaka 3 hapo hakuna rejea.

Nikauliza nikaambiwa ataweza kurejea iwapo ataolewa tena na kuachwa.

Sasa sijajua Kwa talaka ilotolewa mahakamani inakuwaje,

Kwamba yenyewe ni final and conclusive au watalaka wanaweza kurejeana iwapo kuna masharti fulani ?

Na hii huenda ndio maana kesi za talaka hazipelekwi haraka,

Huwa wanatoa muda ili hasira zishuke maana talaka ya hasira ni mbaya sana.

Uamuzi unaofanywa wakati wa hasira huwa sio mzuri sana.

Though siku hizi wanarahisha kutoa haraka tofauti na zamani sababu ya kuepuka mauaji ya wanandoa.

Labda wawe wanawatenganisha kwa muda wakati wakisubiri mtendwa kuondoa hasira na uchungu ili aamue akiwa na utulivu wa akili bila kupelekeshwa na hasira.
 
Back
Top Bottom