Sijajua kuhusu mambo ya dini kabila au jadi kuhusu wanandoa wawili (mke na mume)hua naona au kusikia kuwa endapo wanandoa upande wa mwanaume ndio anaetoa talaka endapo ataona au sikia kwa ushahidi kuwa labda mkewe kaenda tofauti na masharti ya ndoa yanavyosema ,je!mwanamke nae anaruhisiwa kutoa talaka kwa mumewe?na kama inaruhusiwa ni vigezo gani anatumia hadi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, katiba yetu ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), inatambua aina kuu mbili za ndoa, yaani ndoa ya mke mmoja na ya wake wangi.
Utofauti upo kwenye taratibu za ufungaji, inaweza kuwa ni Kimila, Kiserikali pamoja na Kidini. Ndoa ni mkataba kama mingine, huvunjwa kulingana na utaratibu uliotumika kuifunga.
Kwa maana hiyo, endapo kuna haja ya kuivunja kama ni ya Kimila zitatumika taratibu za kimila, ya Kiserikali za Kiserikali na Kidini za kidini husika inavyoelekeza.
Swali ni, je ni nani wa kutoa talaka? Jibu liko kwenye utaratibu uliotumika kuifunga ndoa husika.
Kwa mfano, kwa Waisalamu ni mwanaume, Kiserikali wanandoa wote ni sehemu ya mkataba na wanahaki sawa yeyote anaweza kuanzisha mchakato wa kumuacha mwenzie na kwa Wakristo nakuachia wewe unayesoma.
NB: Mahakama inayo nafasi ya kuingilia utaratibu wowote uliotumika kuifunga ndoa, endapo kuna viashiria vya mmoja wapo kutoridhishwa na maamuzi yaliyotumika au yanayozuia kuivunja.