Je mahakama ikatoa talaka na mimi nikaendelea kumtaka mke wangu ana mke nae akakubali hii inakuwaje
Swali zuri sana.
Mpaka talaka inatolewa ni ama mmojawapo mfano mke au wote 2 mke na mume mmeudhishana na kuumizana mioyo pakubwa na sasa inahitajika talaka.
Sasa sijaelewa vizuri swali lako;
Kwamba unauliza iwapo mke alidai talaka na mahakama ikaridhia kutoa mkaachana,
Kwamba baada ya muda mke akasamehe akarudisha moyo na kuanza kukurejea au siyo ?
Kama nimekuelewa hivyo!
Chukulia hata kidini mwanamke akipewa talaka 3 hapo hakuna rejea.
Nikauliza nikaambiwa ataweza kurejea iwapo ataolewa tena na kuachwa.
Sasa sijajua Kwa talaka ilotolewa mahakamani inakuwaje,
Kwamba yenyewe ni final and conclusive au watalaka wanaweza kurejeana iwapo kuna masharti fulani ?
Na hii huenda ndio maana kesi za talaka hazipelekwi haraka,
Huwa wanatoa muda ili hasira zishuke maana talaka ya hasira ni mbaya sana.
Uamuzi unaofanywa wakati wa hasira huwa sio mzuri sana.
Though siku hizi wanarahisha kutoa haraka tofauti na zamani sababu ya kuepuka mauaji ya wanandoa.
Labda wawe wanawatenganisha kwa muda wakati wakisubiri mtendwa kuondoa hasira na uchungu ili aamue akiwa na utulivu wa akili bila kupelekeshwa na hasira.