Uchaguzi 2020 Je, kauli hizi za 'Tamaa ya Madaraka na kutomtuma mtu kugombea' alizotoa Rais Magufuli ni dongo kwa Makonda na Gambo?

Uchaguzi 2020 Je, kauli hizi za 'Tamaa ya Madaraka na kutomtuma mtu kugombea' alizotoa Rais Magufuli ni dongo kwa Makonda na Gambo?

Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Makonda kakurupuka!

Subirini hii ngoma bado mbichi.
 
Tena kakazia kwamba hajamtuma yeyote kwenda kugombea ubunge.
Hakuna jitu nafiki na liongo kama jiwe, kwa masikio yangu nikiwa natoka kigoma gari letu tulipigwa bin pale kakonko kusubiri jamaa amalize kuhutubia, nusu Saab aliitumia kumsimanga mbunge wa chadema na kuwananga raia kuwa walikosea kuchagua upinzani, alikuwa kaongozana na ndalichako na mipango na akawapigia kampeni 2020 wamchague mipango na ndalichako ndo atawaletea maendeleo, ilikuwa 2017 hiyo aseme sasa na hao kuwa hajawatuma
 
Wacha tungoje tuone. Nchi hii ina maajabu mengi. Let's not jump to conclusion. In the long run I am sure he knows what he is doing, hajakurupuka
Andengenye, Lugola, Nchambi, Lugumi, n.k. wote wanaendelea kuula. Makonda naye "is in the same pipeline".
 
Ukimsikiliza msemaji wa Rais anakwambia wazaramo wanausemi ambao unabamba sana mjini usemao Mwana kulitafuta Mwana kulipata pia Mama Samia naye anakwambia wateule wa Rais wajifunze kuridhika Ukija kwa JPM mwenyewe anawaambia mie sijatuma mtu pia mjifunze kuridhika hapo bado Sijamsikia boss wa ma RC na DC Yani Majaliwa ukirud kuyatafuta maneno ya Polepole kuhusu Kigamboni ndo kabisa utajua Makonda alikuwa analindwa tuu mana mabosi wake wanajua kuwa hapendwi na watu hvyo wamwachie madaraka ili apate kinga Sasa naleo tunaambiwa Mtoto akililia Wembe tumpe au tumnyime
Mkuu nani kakudanganya Makonda hapendwi?
Usifikiri washabiki wachache wanaomtukana Makonda humu mitandaoni na uswahili wako hivyo hapana. Tena Makonda angetia timu jimbo la Ukonga asubuhi tu angeshinda
 
Kauli ya Rais ni sahihi, ukizingatia kwamba kuna umuhimu wa kuwa na uwanja sawa wa ushindani ili kupata wagombea bora.
 
Mkuu nani kakudanganya Makonda hapendwi?
Usifikiri washabiki wachache wanaomtukana Makonda humu mitandaoni na uswahili wako hivyo hapana. Tena Makonda angetia timu jimbo la Ukonga asubuhi tu angeshinda
Sie waswahili n tabu sana yan unamaanisha kule ukonga kwa wakurya wengi au?
 
"Hakuna mtu yotote aliyetumwa na Mimi wala Makamu wa Rais, Wala Waziri Mkuu kugombea Ubunge. Kama ningekutuma si ningekuchagua mimi mwenyewe kwenye nafasi zangu 10", Rais Magufuli.

Magufuli kumteua Makonda ubunge kisha kumteua uwaziri would be too dumb. Hiyo nukuu si kwa ajili ya mtu anayeng’aa kwenye anga za Magufuli kama Makonda. Wako wengine pia wa aina hiyo wameshaingia kugombea majimbo ambao watu wanajiuliza “huyu si angesubiri uteuzi tu?” I believe he’s gotten wiser and smart about toying about with his closest soft spots.
 
Hakuna jitu nafiki na liongo kama jiwe, kwa masikio yangu nikiwa natoka kigoma gari letu tulipigwa bin pale kakonko kusubiri jamaa amalize kuhutubia, nusu Saab aliitumia kumsimanga mbunge wa chadema na kuwananga raia kuwa walikosea kuchagua upinzani, alikuwa kaongozana na ndalichako na mipango na akawapigia kampeni 2020 wamchague mipango na ndalichako ndo atawaletea maendeleo, ilikuwa 2017 hiyo aseme sasa na hao kuwa hajawatuma
Daah noma sana.
 
Usimwamini sana Magu

Kinyume chake huenda ndio ukweli ii msije kusema aliwaandaa ili aje awape uwaziri.

Maneno ya Magu yalikuwa mkwara tu kwa wale asiyewatuma kuchukua fomu na wananafasi nyingine serikalini. Kifupi, aliloliona Magu ni kuwa wakati wa uchaguzi ni wakati wa makundi upende usipende, hivyo alitaka kupunguza tension serikalini kwani kama mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wakalitaka jimbo moja, utawala serikalini utakuwa mgumu. Mfano yaliyotokea Arusha.

Lakini hii haiwahusu akina Makonda walioenda kuomba ushauri kwake naye akawapa baraka zote na hata kuwasaidia huko mbeleni. Waoga hawatachukua fomu, risk takers watachukua fomu bila ridhaa ya mtemi, hawa wanaweza kukatwa mapema. Hili nakuhakikishia.

Kifupi safari hii wagombea wa majimbo yote kupitia chama tawala majina yao yapo tayari ofisini kwa mwenye kiti. Wengine ni wasindikizaji tu.
 
Rais Magufuli baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Dodoma amenena kwamba viongozi mbalimbali hawaridhiki kabisa na madaraka hasa waliozaliwa mwaka 82 (1982).

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole...

Kauli hii imenifanya niangalie mwaka aliozaliwa Paul Makonda na kukuta amezaliwa mwaka 1982. Naamini hii haiwezi kuwa bahati mbaya ila Rais alimaanisha alichokisema.

Nanuia kusema kwamba Makonda mpaka sasa ana hali mbaya na huenda ukawa mwisho wake kisiasa.

Baadhi ya nukuu za Rais Magufuli...

Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982.

Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais, waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829

Nawapongeza waliotia nia lakini niwahakikishie hakuna aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu, kama wapo wanaosema mimi nimewatuma ni waongo na hii meseji iwafikie Wana-CCM wote nyinyi wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanafaa

Sijatuma mtu [kugombea ubunge]. Siwezi nikatuma mtu kupitia mgongo wa pembeni. Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma, kwanini nihangaike kukutuma, si ningesubiri tu kwenye viti vyangu 10 nikakuteua kama ningeshinda.

Acha wafu wazike wafu wao
 
Back
Top Bottom