Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Sasa umeingia kwenye mfumo wangu

Wanasiasa wote wanaofanya biashara wanakwepa kodi ndo Ufisadi wenyewe
Wanapata tenda kwa upendeleo ndo Ufisadi wenyewe
Pia wanapata taarifa mapema za miradi ya kuwa financed na taasis za fedha za serikali ndo Ufisadi wenyewe

1. Mwigulu
2. Rostam Azizi
3. Samia suluhu na familia yake
4. Kikwete na familia
5. Msukuma kasheku
6. Na wengine wengi tuna mafaili yao
huu ndio ukweli mtupu....imagine mtu anapata taarifa ya mipango ya serikali miaka 10 kabla
 
Weka hoja kwanini mwanasiasa akiwa tajiri ni fisadi ila mtu wa kawaida asie mwanasiasa akiwa tajiri sio fisadi
Neno fisadi limeonekana kuwa kidogo ni la kistaarabu na lisilomvunjia sana heshima mtu kama vile huyo mtu angeitwa Mwizi 😳 !

Maneno ya Kiswahili yanachanganya sana Akili 😁 kama kusema fulani amezaa badala ya kusema fulani amejifungua !
 
kwenye taifa la wafanyabiashara wenye mabillion wengi zaidi ya maelfu watu wanaumia kuona mawaziri 40 wamiliki na wenyewe hizo billion..kwa sababu kama kuna wafanyabiashara wanafunga million 10 faida hapo kariakoo utashangaaje kuona waziri amiliki nyumba ya million 500 au gari la million 100
Ndge njaa, utumishi wa Umma ni wito na sio njia ya kujitajirisha.
 
Kuna kitu huwa kinanichanganya na kunifikirisha

Mtu akiamua kugombea udiwani, ubunge au hata urais, je, huwa anatafuta kazi kama zilivyo kazi nyingine ili apate kipato cha kujihudumia yeye na familia yake?

Au huo ni uzalendo usiohusisha maslahi yoyote binafsi?

Nauliza hivi kwa sababu mara nyingi ukimwona mwanasiasa anaendesha gari la kifahari au anaishi maisha mazuri, watu wengi hukimbilia kusema ameiba au ni fisadi

Lakini je, mwanasiasa haruhusiwi kuwa na good life?
Maana yupo kazini, analipwa mshahara na stahiki nyingine kama watumishi wengine

Au sisi kama jamii tunaamini kwamba mwanasiasa akionekana ana maisha mazuri, basi lazima kuna jambo lisilo sawa?
👇

NB: Mada hii ni kwa ajili ya mjadala na kubadilishana mawazo, kwa kuzingatia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayompa kila mtu haki ya kuwa na maoni na kueleza fikra zake kwa mujibu wa sheria

So ningependa maoni yasiyo na matusi ziwe hoja tu itapendeza

Karibuni kwa hoja

ShesRise_1 ✋️
Ndiyo, kupepeta tu mdomo unakuwa tajiri?
 
Neno fisadi limeonekana kuwa kidogo ni la kistaarabu na lisilomvunjia sana heshima mtu kama vile huyo mtu angeitwa Mwizi 😳 !
Kumbe fisadi ni neno laini ?
Maneno ya Kiswahili yanachanganya sana Akili 😁 kama kusema fulani amezaa badala ya kusema fulani amejifungua !
Wewe kweli ni wa wawakati ule😁
 
Wanaodai wanasaisa wanajitajirisha kwa ufisadi ni kwamba wana mianya mingi ya kujipatia pesa isivyo halali zaidi ya raia wa kawaida.

Fisadi wapo kote uraiani na kwenye siasa maana hao wanasiasa wakifuja hawafuji peke yao.

Tushaona mara kibao serikali zetu tu za vijiji wakijimegea ardhi au kufanya michakato isiyo ya haki kuwapa wenye ukwasi huku wao wakilamba mchuzi mnono.

Hivyo sio kila mwanasiasa anachota pesa hazina au kwenye miradi ya maendeleo ila kuna mianya mbalimbali ambayo sio halali yake wala haki yake yeye kujinufaisha ila hufanya hivyo kwa maslahi yake.
 
Sawa asante kwa maoni mkuu karibu tena
 
Back
Top Bottom