kwanza si kweli kwamba,
kila mwanasiasa tajiri ni fisadi.
Lakini nikiri tu kwamba kuna hiyo dhana ambayo sitaki kusema ni potofu miongoni mwa jamii mbalimbali ulimwenguni, hususani hapa Tanzania.
Kiujumla siasa ni maisha na maisha ni siasa. Ndio maana mapioneer wa falsafa hii ya siasa walisema, human beings are political animals. Na kwamba hayupo mwanadamu mwenye uwezo wa kuikwepa siasa maishani mwake ispokua labda awe manafiki tu. Unaweza kudhani umekwepa siasa za vyama vyama vya siasa majukwaani, badala yake lazima utakutana na siasa za kwenye familia yako, kwenye dhehebu lako la dini, zaidi sana utakutana na siasa kwenye michezo uipendayo, utakutana na siasa kwenye biashara, kwenye kilimo, mahusiano na chochote kile kinachohusisha jamii fulani inayochangamana na kuahidiana mambo mbalimbali n.k.
hii ikimaanisha kwamba,
ukiamu kujizatiti kwenye aina fulani ya siasa kikamilifu, mathalani kwenye siasa ya biashara, vyama, kilimo au ufugaji kadiri nilivyoelezea hapo juu unaweza kutajirika vizuri sana na jamii ikaibua dhana mbalimbali dhidi ya utajiri wako. Wengine watadhani, watasema au kudai kwamba utajiri wako ni kutokana na kutoa kafara ndugu zako, freemanson, ujambazi, ufisadi n.k, dhana ambazo zinaweza kua hazina uthibitisho kabisa.
Sote ni mashahidi jinsi ambavyo waTanzania hujenga dhana mbalimbali dhidi ya utajiri wa wa kutupwa wa viongozi mbalimbali wanaofanya siasa za kidini kama vile mitume, manabii na makuhani humu nchini.
So,
mi nadhani mtu yeyote yule hapa Tanzania ana haki ya kuchagua aina ya siasa aipendayo na kuifanya. Lakini pia ana haki ya kutajirika kadiri awezavyo kulingana na bidii na maariafa yale akonayo. Na mtu yeyote yule anayefanya aina yoyote ya siasa na akatajirika kiudanganyifu au kinyume na sheria atawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi ikiwa itathibitishwa na vyombo husika vya kutoa haki. Natamani kueleza zaidi but kwasababu ya muda naomba kuishia hapo.
Otherwise,
nakupongeza sana ndugu madau,
kwa namna ambavyo uanabuni hoja zako, unajenga hoja, unatetea hoja zako na kuibua falsafa zenye concepts muhimu na nzito sana jukwaani. Una uwezo mkubwa mno wa kudevelop theories za kutafakarisha na kuibua hisia mseto za kusisimua sana ubongo.
well done and,
God bless you