Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Hapa Tanzania tajiri number moja anaweza kua ni mwanasiasa
 
Umesema huwezi kua mwanasiasa ukawa na pesa safi

Ila unaweza kua raia wa kawaida ukawa na pesa safi
Hii ni maajabu

Hivi ukitoa hilo neno siasa huyo mwanasiasa si raia tu kama wewe?
 
Umesema wanasiasa wote wanafanya biashara ila wanakwepa kodi

Kwahiyo tayari umekiri biashara wanafanya sio kwamba wanachota hela BOT

Hili la kukwepa kodi tutalianzishia uzi wake
 
Wanasiasa karibu wote ambao wafanyabiashara ni wakwepa kodi wakubwa, huo ni ufosadi, kama unaingiza container unatakiwa kulipa ushuru sawa na mfanyabiashara mwingine lakini unatumia nafasi yako kukwepa kodi, wewe ni fisadi kama mafisadi wengine.

Wale wasio wafanyabiashara, hasa waliopo kwenye nafasi za kufanya maamuzi, baadhi hufanya maamuzi kwa faida na maslahi yao. Mtu anakwenda kusaini mkataba kwa niaba ya taifa, akifika huko anarubuniwa ili mkataba uwe favourable kwa mwekezaji, huo ni ufisadi mkubwa.

Hatuna shida wakimiliki ukwasi mkubwa, wala sio tatizo. Ila viwe halali basi.
 
Ahaa kumbe tatizo wao sio kua wamiliki ila uhalali wake ni upi okay

Sasa tufanye je ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…