Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Kuna kitu huwa kinanichanganya na kunifikirisha

Mtu akiamua kugombea udiwani, ubunge au hata urais, je, huwa anatafuta kazi kama zilivyo kazi nyingine ili apate kipato cha kujihudumia yeye na familia yake?

Au huo ni uzalendo usiohusisha maslahi yoyote binafsi?

Nauliza hivi kwa sababu mara nyingi ukimwona mwanasiasa anaendesha gari la kifahari au anaishi maisha mazuri, watu wengi hukimbilia kusema ameiba au ni fisadi

Lakini je, mwanasiasa haruhusiwi kuwa na good life?
Maana yupo kazini, analipwa mshahara na stahiki nyingine kama watumishi wengine

Au sisi kama jamii tunaamini kwamba mwanasiasa akionekana ana maisha mazuri, basi lazima kuna jambo lisilo sawa?
👇

NB: Mada hii ni kwa ajili ya mjadala na kubadilishana mawazo, kwa kuzingatia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayompa kila mtu haki ya kuwa na maoni na kueleza fikra zake kwa mujibu wa sheria

So ningependa maoni yasio na matusi ziwe hoja tu itapendeza

Karibuni kwa hoja

ShesRise_1 ✋️
Ukitaka kujua nenda Mbweni Maji chumvi aka Mbweni JKT walipojenga wanasiasa wengi ,pia tathmini nafasi zao /kipato chao kinaendana na majumba ya mabilioni na fleets ya magari ya mabilioni wanayomiliki? Utamkuta ni staff wa serikali lakini ana jumba la Bilioni 5 ,fleets ya magari total bilioni 2 ,ukipiga mshahara wake tangia anaanza kazi hadi hapo alipofikia kwa kukusanya bila kutumia hata 10 haifiki 1B.
 
Shida sio kuwa na good life ebu tueleze huyo mwanasiada analipwa mshahara kiasi gani mpaka aishi maisha tunayoonaga wanasiasa wanaishi
 
Mkuu mshahara na posho halitoshi lakini watu si wanawekeza pia njee na utumishi
 
Shida sio kuwa na good life ebu tueleze huyo mwanasiada analipwa mshahara kiasi gani mpaka aishi maisha tunayoonaga wanasiasa wanaishi
Unadhani wanategemea mshahara pekee?

Mbona unaweza kukuta mtumishi wa serikali ana maduka huko k/koo
Mwanasiasa yeye hawezi?
 
Hapana, kwa ujumla hakuna tatizo la kisheria au la kimaadili kwa diwani kuwa bilionea. Utajiri wa mtu peke yake haumzuii kushika nafasi ya uongozi ikiwa anatimiza masharti yote ya kugombea na kushika wadhifa husika.
Safiiiiii
 
Mkuu mshahara na posho halitosis lakini watu si wanawekeza pia njee na utumishmud

Mkuu mshahara na posho halitosis lakini watu si wanawekeza pia njee na utumishi
Mbona wanaanza kuishi maisha ya kifahari baada tu ya kuanza kazi ni muda gani unakuta wamewekeza na huo uwekezaji umeanza kuwalipa
 
Soma uelewe ili ujifunze. Siasa maana yake zinampa mtu maamuzi juu ya keki ya taifa. Zinampa mtu "advantage over his/her businesses". Ndio maana Nyerere alikuwa anakataa wafanyabiashara kuwa wanasiasa/viongozi. Alifahamu hatari ya mtu kuwa kiongozi na hapo hapo awe mfanya biashara. Lazima utaongoza keki ya taifa kuakisi maslahi/biashara zako.
Kuna mgongano wa maslahi kati ya mwanasiasa/kiongozi na biashara linapokuja suala linalohusu maslahi ya taifa na biashara. Wewe unaweza usijue kwanini mpaka sasa tunavutana juu ya ishu ya Ngorongoro; pale pana vitu vyote, kuna mazigira, siasa na maslahi ya watu/wanasiasa. Kuna viongozi wana maslahi napo pale. 😊
Nasoma , naelewa , najifunza na hii ndiyo sababu kwanini nikafungua huu uzi right?

Kwa mantiki hiyo mwanasiasa asifanye biashara ili kuepuka uvunjifu wa maadili si ndio ?
 
Afrika ndio sehemu pekee wanasiasa wanapesa nyingi na wanaishi maisha ya kifahari kuliko wafanyabiashara
Uki angalia katika angle nyingine kuwa tajiri akuja halalishwa kwa wafanyabiashara pekee
Wanasiasa fedha ya nchi wana access nayo na ni ya uhakika na ndio mfumo tulio jichagulia ingawa sio rasmi na sio dhambi
 
Mkuu mshahara na posho halitosis lakini watu si wanawekeza pia njee na utumishi
Umenisaidia na hapo ana biashara ya Mabilioni haijulikani mtaji kautoa wapi na kwenye "TUME YA MADILI" hajadeclare hizo mali wala biashara....si unajua watumishi wa umma wanataja mali wanazomiliki kwenye kitengo cha maadili?
 
Rudi huko huko kwenye katiba kasome tena miiko/maadili ya wanasiasa na viongozi wa serkali ndo utajua ni wezi au ni kipato chao cha kazi halali kama waajiliwa wengine.
Nipe kipengele mkuu iwe rahisi kwangu
 
Back
Top Bottom