Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Tafsiri yako tunaiweza kuihakiki kupitia chanzo gani?Unaposema nafsi haipo ni kama hujajua maana ya nafsi. Nafsi maana yake ni upekee katika binadamu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tafsiri yako tunaiweza kuihakiki kupitia chanzo gani?Unaposema nafsi haipo ni kama hujajua maana ya nafsi. Nafsi maana yake ni upekee katika binadamu.
Hakuna nafsi ya kuonja mauti wala mboga.
Kwasababu nafsi haipo.
Upo wewe na mimi.
Kifo kipo, ni nature na ndio sifa ya kiumbe hai lazima kipitie njia hiyo.
Japo wanasayansi wanaamini kuwa miaka ya mbeleni huko kunaweza kupatikana ufumbuzi wa kurudisha uhai kwa mtu aliyekufa.
Na ndio maana wanajaribu kuhifadhi miili ya watu isiharibike kwa lengo la kuja kuiwekea uhai huko mbeleni itakapopatikana suluhu.
Kwa nini tuamini ufufuo wakati Paulo katika Warumi 3:7 anakiri kwamba anadanganya ?1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; HATUTALALA SOTE, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Hapo 👆 aliposema kwamba hatulala wote bali wote tutabdilika maana yake ni kwamba hatutakufa wote bali wote tutabadilika.
Wadau, habari ya majukumu bila shaka muwazima wa afya, kama na wale wenye changamoto ya afya, niwaoe pole.
Bila kupoteza muda, twende kwenye mada husika. Hili neno "kila nafsi itaonja mauti," kiuhakika, halijaandikwa kwenye Biblia. Nadhani ni utashi tu wa mwadamu ameamua kutumia hili neno. Sasa turudi kwenye swali letu: Je, ni kweli kila nafsi itaonja mauti?
Kwenye kitabu cha Ufunuo, kinasema parapanda itakapolia, wafu waliolala watafufuliwa kwanza ndipo wataungana na hawa walioko hai kwa wakati huo, ndipo watapaa mawinguni kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Sasa, kama tunasema kila nafsi itaonja mauti, na Biblia nayo inasema parapanda itakapolia itakuta kuna binadamu ambao wapo hai watasubiri kwanza wafu wafufuliwe ndipo waungane nao kwenda kumlaki Bwana mawinguni, je, kwanini hiyo kuna baadhi ya watu hawataonja mauti?
Hakuna nafsi ya kuonja mauti wala mboga.
Kwasababu nafsi haipo.
Upo wewe na mimi.
Kifo kipo, ni nature na ndio sifa ya kiumbe hai lazima kipitie njia hiyo.
Japo wanasayansi wanaamini kuwa miaka ya mbeleni huko kunaweza kupatikana ufumbuzi wa kurudisha uhai kwa mtu aliyekufa.
Na ndio maana wanajaribu kuhifadhi miili ya watu isiharibike kwa lengo la kuja kuiwekea uhai huko mbeleni itakapopatikana suluhu.
Sijakuelewa mkuu, hemu fafanua hapo.Kwa nini tuamini ufufuo wakati Paulo katika Warumi 3:7 anakiri kwamba anadanganya ?
7 Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?
nafsi ni nini exactly
Sijakuelewa mkuu, hemu fafanua hapo.
Sijakuelewa mkuu, hemu fafanua hapo.
Kwamba hao niliwataja ipo siku watakufa? Wanaishi nchi gani?Hapo mkuu hakuna habari zilizopita bora useme kuna watu hadi sasa hawajafa.
Ndivyo ilivyo na muombe Mungu asikufikishe huko mwisho wa dunia maana watu wake watakuwa kama wale mazombi uyaonayo kwenye TV, litakuwa ni Toledo la mwisho la binaadamuJesus...hii ndio kwanza naisikia leo
Uislamu unaamini watu wote watakufa, hata nabii issa atarudishwa duniani aje aonje na yeye mauti, watakaokuwa hai ni malaika tu maana malaika israfil mpuliza parapanda ndiye atakaepuliza kwa amri ya Mwenyezi Mungu mara zote mbili, inamaana lazima atakuwa haiMtoa mada achana na habari zijazo kwanza angalia hata angalia kwanza zilizopita... Kwa mujibu wa biblia Henoko hakufa na Elia pia hakufa. Kwa kuangalia hapo tu unaona huo msemo hauna maana (kwa wakristo). Nadhani waislamu wanaamini hivyo na sisi wakristo tulivyo wepesi wa kudaka vitu hata tusivyovijua tumeiga
Unamaanisha huo ulioandika ni uongo?Mbona huku Tumeambiwa mengine ??
Marko
23 Basi jilindeni; Nimewaambia yote kabla ya wakati wake (ona pia Luka 2:52: MUNGU alimsamehe Yesu).
24 Lakini katika siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake;
25 nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na viumbe vya mbinguni vitatikisika. [4]
26 “Wakati huo watu watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu akiwa na nguvu nyingi na utukufu.
27 Naye atawatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake kutoka pepo nne, kutoka mwisho wa dunia hadi mwisho wa mbingu.
28“Sasa jifunzeni jambo hili kutokana na mtini: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
29 Vivyo hivyo, mwonapo mambo hayo yakitukia, tambueni kwamba yu karibu, mlangoni.
30 Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakika hakitapita mpaka mambo hayo yote yatimie.
31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Yesu hakuahidi tu kwamba saa ingekuja kabla ya kizazi alichokuwa akiishi kati yao kupita katika kitabu cha Marko, lakini pia alitoa ahadi hiyo hiyo katika kitabu cha Luka:
"Kisha akawaambia wote, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate.
Kwa maana yeyote anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Yafaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, na huku akijipoteza au kujipoteza mwenyewe?
Mtu ye yote akinionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu.
Amin, nawaambieni, baadhi yao katika papa hapa hawataonja mauti hata kabla ya kuuona ufalme wa Mungu.” (Kutoka Biblia ya NIV, Luka 9:23-27).
Sawa na Marko 13:1-37 kama inavyoonyeshwa hapo juu, Yesu katika Luka 9:23-27 bado anatoa ahadi nyingine kwamba saa ingekuja kabla ya kizazi alichokuwa akiishi kati yake kupita.
Sasa ni zaidi ya miaka 2,000 baada ya Yesu na kizazi alichokuwa akiishi kati yao kufa, na bado, Saa haijafika bado!
Siyo tu kitabu cha Paulo ndicho chenye mkanganyiko, Biblia almost yote ina mkanganyiko,, na unaposema Paulo hapaswi kuaminiwa, you're wrong brother coz Paulo hakujiandikia tu kama unavyofikiri bali lile ni neno lililotoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.Kwa nini Paulo hapaswi kuaminiwa
Paulo hakuwahi kukutana na Yesu maishani mwake.
Hii ni moja ya sababu kuu ya kutomwamini na kumwamini Paulo.
Kabla ya kujidai kuwa mtume, jina lake lilikuwa Sauli na aliwahi kuwa muuaji wa waumini wa kweli.
Akiwa njiani kuelekea Damasko, akiwa kwenye mgawo wa kuwasumbua waamini wa kweli, anadai kuwa ameona maono ya Kristo, na baada ya hayo, alidai kwamba Yesu alimpa mamlaka ya kufundisha kwa jina lake.
Jee !!!!! kuna ukweli wowote hapa katika maneno yake hayo ??
Kwa vile hakuwahi kukutana na Yesu, akili ya kawaida inasema kwamba yeye hana uhusiano wowote na dini na tunaposoma anachosema tunakuta kwamba hakika yeye hana uhusiano wowote na dini ya kweli ya Nabii Isa (amani iwe juu yake). .
Hebu tuangalie ono la Paulo anapolielezea kwa watu mbalimbali, tofauti wake
1. Katika MATENDO 9:3, imeelezwa kwamba ni Paulo pekee aliyeanguka chini alipoona mwanga. Mstari wa 7 unasema kwamba wengine pamoja naye walisimama bila la kusema.
2. MATENDO 26:14 inasema WOTE walianguka chini.
3. MATENDO 9:7 inasema kwamba watu waliosafiri pamoja na Paulo hawakumwona mtu bali walisikia sauti.
4. MATENDO 22:9 inasema wale waliokuwa pamoja na Paulo waliona nuru lakini HAWAKUsikia sauti ya msemaji.
Hayo hapo juu ni mikanganyiko ya wazi
Mtu ye yote angemkataa Paulo mara moja baada ya kusoma mistari hii.
Ikiwa huu ni uwongo wa wazi tu na Paulo amesahau aliposema nini, basi si zaidi ya ujinga wake lakini ikiwa anatumia mbinu hii kwa makusudi kusimulia hadithi tofauti kwa watu tofauti, basi mbinu hii bado inatumika hata leo.
Mbinu kama hiyo imeweka msingi muhimu sana wa Kanisa, i.e. kupitisha njia inayomfaa mtu.
Hakuna nafsi ya kuonja mauti wala mboga.
Kwasababu nafsi haipo.
Upo wewe na mimi.
Kifo kipo, ni nature na ndio sifa ya kiumbe hai lazima kipitie njia hiyo.
Japo wanasayansi wanaamini kuwa miaka ya mbeleni huko kunaweza kupatikana ufumbuzi wa kurudisha uhai kwa mtu aliyekufa.
Na ndio maana wanajaribu kuhifadhi miili ya watu isiharibike kwa lengo la kuja kuiwekea uhai huko mbeleni itakapopatikana suluhu.
😂😂Namhurumia sasa yule wa mwisho kufa baada ya watu wote duniani kufaMi ninavyo juwa parapanda lita pulizwa Mara mbili
Mara ya kwanza watu wote watakufa Mara ya pili watu wrote watafufuka.