Basi Kama kweli hao mitume na manabii wa kale walikuwa ni waislam basi na hiwe dini ya kiislam kama dini ya kweli na takatifu
Lakini kama itakuwa ni kweli kwamba hawakuwa waislam labda walikuwa wapagani basi dini ya kipagani na ndiyo iwe dini ya kweli ya mwenyezi mungu
Na kama kweli manabii hao walikuwa labda ni wakristo basi ikawe ukristo ndiyo dini ya kweli
Basi Na ikawe hivyo basi enenda zako hewe mwanadamu ukafuate utakacho kipenda nafsi yako
Baadhi ya Wakristo wengine wanapinga taratibu za dini ya Kiislam. Wanakuwa na shauku ya kupinga waia hawajui
mafundisho ya dini ya Kiislam wala hawajapata nafasi ya kusoma Biblia.
Kama ndugu Wakristo mngesoma tu Biblia mngekuta mafundisho mengi ya kiislamu yanapatikana humo.
Kwa kufupisha somo ninaandika hapa mambo ambayo yanaonekana mageni kwa Wakristo ilhali yamo katika
Biblia.
Udhu
Bwana akanena na Musa na kumwambia fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba ili kuogea, nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu nawe utalitia maji. Na Haruni na mwanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania, watajiosha majini ili wasife au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike kumteketezea Bwana sadaka ya moto basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife na neno hili litakua amri kwao milele kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyote. (Kutoka 30:17-21).
Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. (Yohana 2:6).
Kuvua viatu wakati wa ibada
Huyo Amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, vua viatu vyako miguuni mwako kwa kuwa mahali hapo
usimamapo ni patakatifu, Yoshua akafanya hivyo. (Yoshua 5:15).
Naye akasema usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni mwako maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. (Kutoka 3:5).
Ibada na Sajda
Naye Ezra Kuhani akasimama juu ya mimbari ya mti waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo na karibu naye
akasimama Matithia ....... Ezra akakifungua kitabu machoni pa watu wote (maana alikuwa juu ya wote) na hapo alipokijua, watu wote walisimama Ezra akamhimidia Bwana, Mungu Mkuu. Nao wote wakaitika Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao kisha wakainama vichwa vyao wakamsujudia Bwana vifudifudi. (Nehemia 8:4-12; Mwanzo 17:3).
Akaendelea mbele kidogo akaanguka kifulifuli akaomba ... (Mathayo 26;39).
Msujudie Mungu. (Ufunuo 22:9).
Musa akafanya haraka akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. (Kutoka 34:8; 1 Wakorintho 14:25).
Nyimbo Hazitakiwi
Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu. (Amosi 5:23).
Ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi kama vile Daudi. (Amosi 6:5).
Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana Mungu. Mizoga itakuwa mingi kila mahali wataitupa wakinyamaza kimya. (Amosi 8:3).
Masanamu hayatakiwi
Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, (Kumb. 5:7-9).