Mbona huku Tumeambiwa mengine ??
Marko
23 Basi jilindeni; Nimewaambia yote kabla ya wakati wake (ona pia Luka 2:52: MUNGU alimsamehe Yesu).
24 Lakini katika siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake;
25 nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na viumbe vya mbinguni vitatikisika. [4]
26 “Wakati huo watu watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu akiwa na nguvu nyingi na utukufu.
27 Naye atawatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake kutoka pepo nne, kutoka mwisho wa dunia hadi mwisho wa mbingu.
28“Sasa jifunzeni jambo hili kutokana na mtini: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
29 Vivyo hivyo, mwonapo mambo hayo yakitukia, tambueni kwamba yu karibu, mlangoni.
30 Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakika hakitapita mpaka mambo hayo yote yatimie.
31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Yesu hakuahidi tu kwamba saa ingekuja kabla ya kizazi alichokuwa akiishi kati yao kupita katika kitabu cha Marko, lakini pia alitoa ahadi hiyo hiyo katika kitabu cha Luka:
"Kisha akawaambia wote, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate.
Kwa maana yeyote anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.
Yafaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, na huku akijipoteza au kujipoteza mwenyewe?
Mtu ye yote akinionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na utukufu wa Baba na wa malaika watakatifu.
Amin, nawaambieni, baadhi yao katika papa hapa hawataonja mauti hata kabla ya kuuona ufalme wa Mungu.” (Kutoka Biblia ya NIV, Luka 9:23-27).
Sawa na Marko 13:1-37 kama inavyoonyeshwa hapo juu, Yesu katika Luka 9:23-27 bado anatoa ahadi nyingine kwamba saa ingekuja kabla ya kizazi alichokuwa akiishi kati yake kupita.
Sasa ni zaidi ya miaka 2,000 baada ya Yesu na kizazi alichokuwa akiishi kati yao kufa, na bado, Saa haijafika bado!
Basi katika mafungu yanayofuata yesu hapo ulipoishia kwenye kitabu cha marko yesu amesema lakini hakuna ajuaye saa ya kuja kwake wala hata malaika hawaijui
Marko 13 :32 walakini habari za siku ile na saa ile hakuna aijuaye hata malaika walio mbinguni, wala mwana ila baba.
Hapa yesu amehitimisha kwamba hakuna ajuaye siku wala saa ya kuja kwake ila baba pekee, sasa alipokuwa amesema "hakika kizazi hiki hakita pita hata yote yatimie katika marko 13 :30" alikuwa anamaanisha nini?
Ukisoma kuanzia marko 13 :1 yesu alikuwa amezungumzia mateso ambayo yangewapata watu wake yani hao mitume na kwamba baada ya hayo wakati hule wa mwisho ungekuwa umekalibia lakini hakuna "hajuaye saa ya kuja kwake"
Kwa hakika aliyoyasema yesu ni yale mateso waliyo yapata mitume hao kuminambili ambao yesu aliwaacha wakahubiri injiri na hao mitume waliuwa kwa mateso kwa ajili ya jina la yesu na hapo ndipo yesu anatabiri kuwa mateso hayo aliyo yaeleza kuanzia marko13:1 mpaka 30 anasema kwamba mateso yale yangetokea katika kizazi hiko
Lakini utabiri huu ulitimia baada tu ya yesu kupaa mbinguni mitume walianza kuteswa na kuuwawa kwaajili ya ule ushuhuda waliokuwa nao kama ukipitia historia utaona kwamba kuliwai kuwa na dola la rumi ya kale ambayo ndiyo iliyo wauwa wakristo hao ambao walikuwa ni kizazi kimoja na yesu kristo
Lakini vipi kuhusu ujio wake? Licha ya yesu kutabiri mateso hayo yatakayo wapata watu wake katika kizazi hiko yani hao mitume amesema "kwa hakika hakuna ajuaye saa ile ya kuja kwake ila baba"
Hili ndiyo jibu la swali lako bila shaka nazani umeelewa fungu hilo la marko 13:30 "hakika kizazi hiki hakita pita" hata yote yatimie ni kwamba yalikuwa ni mateso ambayo watayapitia mitume kwa hakika unabii huo ulitimia na mitume waliteswa lakini hakumkana yesu walihubiri injiri wala hawakuogopa hata kufa..
Lakini je, kutumia kwa mqteso hayo ndiyo mwisho ule ungekuwa umefika jibu ni "HAPANA"
Marko 13:7 Nanyi mtakapo sikia habari za vita na uvumi wa vita msitishwe hayo hayana budi kutukia lakini ule mwisho bado.
Yesu amezungumza mambo mengi sana ikiwemo vita, matetemwko njaa n.k kiasi kwamba mtu anaweza akachanganyikiwa asielewe lakini muonapo hayo ule mwisho bado huo ni mwanzo tu,
Marko 13:8 kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali kutakuwa na njaa hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
Swali, je, hivi leo kuna taifa limeondoka kupigana na taifa?, je leo hii kuna sehemu kulikumbwa na matetemeko, je leo kuna sehemu kuna njaa? jibu ni "NDIYO" lakini ule mwisho utakuwa bado ukiyaona hayo ila ni mwanzo tu kwa maana hakuna hajuae saa haijalishi itapita miaka miaka mingapi,
Lakini katika maelezo mengi ya yesu alizungumzia pia habari za hao mitume kuminambili ambao walipewa kazi nzito ya kuhubiri injiri ambao walipitia mateso na kuuwawa lakini haikumaanisha kwamba mwisho huo ungefika katika mateso yao ila huo ni mwanzo tu kwa hakika mitume walitimiza unabii hata hivi leo uwepo wa vita na matetemeko njaa bado yanaendelea kama kawaida lakini tazama yuaja upesi na hakuna ajuaye saa haijalishi itapita miaka elfu 2000 au elfu 19000
Je, ungependa kufahamu unabii wa siku za mwisho kwa undani zaidi basi enenda ukasome kitabu chote cha danieli, alafu nenda ukasome kitabu chote cha yohana yani ufunuo usipo elewa basi nenda kwenye kanisa la waadventista wasabato kwani hao ndio pekee wanao utazamia unabii huo wa siku za mwisho kwa ukaribu sana.
Au kama unaswali lolote niulize hapa nitakujibu moja kwa moja