BISMILLAH!
Mwanadamu ni mchanganyiko wa vitu vitatu:
1.الجسد Mwili au kiwiliwili
2. الروح Roho, na
3.النفس Nafsi, ambayo ndio kiini cha Uwanadamu wake, ألإنسان ذاته . Vile Roho ndiyo uhai wake. Ikitolewa roho hana uhai; anasalia na umbo tu, الجسد ambalo halikawii kuoza na kusambaratika. Mzoga, tu جيفة.
Kiwiliwili ni umbo, tu, lenye kuibeba hiyo nafsi, na uhai wake. Na ni NAFSI, kwa maana hiyo, ndiyo mwanadamu mwenye majukumu, myenye dhamana na dhimma, myenye kuamini au kukufuru.
Nafsi, kwa mujibu wa Qur'ani, zipo za aina tatu.
(A) Kwanza ni Nafsi yenye kuamrisha maovu tu. Na hii ndiyo nafsi za watu wengi miongoni mwetu wanadamu. Mwanadamu ni mbinafsi sana; mroho sana; mbaguzi sana, isipokuwa akihisi . Na anapenda kujifurahisha na kujishibisha kwa kila aina ya kila kitu kilicho mbele yake. Hivyo, shauku yetu na matamanio yetu, kila mmoja, ni kushibisha matamanio ya nafsi yake tu. Mwenyezi Mungu ameielezea hulka hii ya manadamu kuwa: إن النفس لأمارة بالسوء
Hakika nafsi, katika asili yake, inapendelea kuamrisha maovu tu.
Mwenyezi Mungu ameielezea nafsi hii, kupitia Ulimi wa Nabii Yusuf, kwa kusema:
وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ (يوسف 12 :53 )
¬_ Na mimi sijitoi lawamani, Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrihs sna maovu, isipo kuwa ile ambayo Mola wangu ameirehemu. Hakika Mola wangu ni Maamehevu Mwingi wa kurehemu._ (Yusuf, 12:53)
Kwa mfano:
Wakati wa swala, kwa mfano, unaweza kuadia, lakini nafsi yako ikakwambia: “Ahh acha! Sasa hivi unaangalia mpira wa timu fulani na fulani, ukiondoka utakosa kuona mbabe wake fulani anavyo funga goli!”
Basi unajiambia: Ukimalizika mcheo tu nitaenda kuswali.
Mchezo unamalizika na unashikwa na mengine na swala imekupita kabisa.
Hawa ndio watu wengi. Na nafsi hapa ndio shetani wako. Na kama inavyosemwa: “Shetani wa mtu ni mtu.” Hiyvo, wewe mwenyewe ndiye shetani wa mwanzo wa nafsi yako.
وقال الشاعر :
والنفسُ كالطفلِ إِن تهمله شبَّ على حُبِّ الرضاعِ وإِن تفطمْهُ ينفطم
وخالفِ النفسَ والشيطانَ واعْصِهما وإِن هما مَحَضاكَ النصحَ فاتِهَّمِ
Mshairi mmoja amesema:
Nafsi ni kama mtoto mchanga. Ukimpuuza atakulia kupenda kunyonya. Na ukimwachisha ziwa ataacha.
Na pingana na nafsi yako na Shetani, na usiwatii! Na endao watakuapia kuwa wanakupa nasaha, basi anza kuwatuhumu! Si wa kweli hao!
(B) Nafsi ya pili inayotajwa na Qur'ani ni النفس اللوامة Nafsi inayo jilaumu na kujittathimini mara kwa mara. Ikifanya kosa tu, basi inajiluaumu na kutubu na kurudi kwa Mola wake. Yaani Nafsi yenye kukumbuka, mara kaw mara, majukumu yake, dhiima yake, na dhamana yake, juu yake na juu ya kila asiyekuwa yeye; khasa Mola wake. Hii ndiyo nafsi ya mwenye kumuamini Mola wake kwa dhati. Na ndiyo nafsi za waja wema wengi. Hawa ndio wale التائبون العابدون الساجدون Wepesi wa kutubu, wepesi wa kuabudu na wepesi wa kusujudu na kushukuru. Ni waja wenye kujirudi mara kwa mara.
Hawa ndio waja wema. Nao wapo wengi vile vile. Hawa ndio wale wanao zainiwa mara moja moja na Ibilisi, wakazainika, lakini hawachelewi kukumbuka kuwa wanafanya makosa, basi papo hapo huacha makosa yao hayo na kurudi kwa Mola wao.
Hawa ndio wanaopendwa na Mwenyezi Mungu. Maana hawa ndio wenye kumuabudu kwa wingi Mola wao, na, kwa kweli, Amewaumba wawe hivyo, ili wamuabudu mara kwa mara.
( C) Nafsi ya tatu inayo zunguzia Qur'ani ni النفس المطمئنة Nafsi iliyotilia tuli, haitikisiki, haizainiki, haipapariki, inamkumbuka Mola wake mara zote na inamuweka Mola wake mble yake, maana inajuwa kuwa inaonekana Naye, hata kama yeye yenyewe haimuoni. Hizi ni nafsi za Mitume صلوات الله وسلامه عليهم
Hawa siku zote wamo katika himaya na ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Miongoni mwao wamo mawalii wa Mwenyezi Mungu, ambao hakuna awajuwao isipokuwa Yeye mwenyewe.
Hawa ndio wanao ambiwa:
﴿ يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ * ارْجِعِي إِلَى رَبِّكِ ﴾
[ سورة الفجر: 27-28]
Ewe Nafsi iliyo tua! Rejea kwa Mola wako umeridhika, na umeridhisha. Basi ingia miongoni mwa waja wangu. Na ingia katika Pepo yuangu.
Hizo ndio nafsi zilizo zungumzwa na Qur'ani.
Tukija upande wa moyo, basi moyon ni sehemu tu ya viungo vya mwanadamu, tofauti na nafsi na roho. Nafsi ndiyo kiini cha mwanadamu, ndiyo uwanadamu wake. Vile roho ni uhai wa mwandamu. Na moyo ni kiungo kimojawapo wa viungo vya mwili wa mwanadamu.
Ila, moyo, ndio Injini na Dira ya mwili wa mwanadamu. Ni doge la nyama tu, ndani ya mwili wake, lenye kazi maalumu mwilini mwake; kuzungusha damu mwilini mwke, na kuisafisha pamoja na viungo vengine. Ni injini ya ujasiri wa uhai wake. Likitengemaa donge hilo basi mwili wake wote utatengemaaa. Na likitetereka au kuharibika au kupootoka basi na mwiliwake wote nao hutetereka na kupotoka.
Moyo, kwa maana hiyo, ni mfano wa kinu cha taa, au Jenereta, katika mwili wa mwanadamu. Ndiyo injini ya kuendesha mwili wa mwanadamu.
Mtume ﷺ ameuelezea MOYO kuwa ni donge la damu. Likitengenea unatengemea mwili wote wa mwanadamu. Na likifisidika basi na mwili wote wa mwanadamu unafisidika. Unakufa, ha kuoza.
Halafu kuna Akili, ubongo. Ubongo ni kompyuta ya mwili wa mwandamu. Ni bohari la kuhifadhin kila kitu ndani yake. Ndiyo hard-disc la mwili na moyo wa mwadamu.
Humo huhifadhiwa maalumat yote uyajuwayo na ujifunjzayo, na hivyo ndiko kunako toka amri kukujiulisha kuwa kuna kitu kimekuuma mguni, na kutokana na muumo huo, basi huyo ni mbu, ect., ect. Mfukuze! Au muue! Maana hiyo ndiyo taafira iliyo ihifadhin katika hard-disc hilo. Vile vile ni ubongo ndio unaokuongoza kuwa ukiona X basi kuna Y inakuja. Maana hiyo ndiyo taarifa iliyo ihifadhi katika hard-disc lako.
Kwa maana hiyo, Mwenyezi Mungu amekupa siyo Nafsi, tu, ambayo ndiyo WEWE na kukupa Roho ili uwe hai, bali amekupa injini ya kukuendesha na kinu chca umema kusaidia mwili wako kufanya kazi. Na wakati huo huo, amekupa Akili, katika sura ya Ubongo, ili kukuwezesha kujuwa mema na maovu, mazuri na mabaya, na juu ya yote hayo akautumia Mitume, na kukupa kumbukumbu za Kitabu au Vitabu Vyake, kukujilisha zaidi nini anakutaka ufanye au usifanye, na kwanini.
Hivyo, mwenye kujichagulia la kufanya au kutokufanya ni WEWEW, na utalipwa kwa uamuzi wako huo. Anapo kunyima Mwenyuezi Mugu uwezo wa kuamua, kwa maana ameifanya akili yako isifanye kazi sawa sawa, basi hakupatilizi. Sisi tunakuita mwenda wazimu. Na Mwenyezi Mungu huwanyanyag'anya baadhi ya waja wake uwezo wa kupambanua jema na baya, ili watambue hivyo wenigine umuhimun wa kutumia ubongo wao sawa sawa.
Katika yote hayo: Mwenyezi Mungu amebainisha, wazi wazi, kuhusu NAFSI na vikorombwero vyake, kwa kusema:
قال تعالى :
﴿ وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَاقَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا*وَقَدْ خَابَ مَنْ دَسَّاهَا ﴾
[ سورة الشمس:7-10]
_Na nafsi na kwa aliye itengeneza! Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Hakika amefanikiwa aliye itakasa Na amehasirika alie iviza.
Kwa maneno mengine:
Kila mtu ajipime yumo katika fungu gani la nafsi. Wala asimsingizie au kumtupia lawama Shetani tu, maana Shetani ni kweli atamzaini, lakini akizainika ni ubwete wake mwenyewe, maana ametumiwa Mitume, ameachiwa Kitabu, ameonya, amefunzwa, ame tahadharisha, na papo akakubali kuzainika, au akajizaini mwenyewe. Kesho hana hoja ya kujitetea. Na akimrushia lawama Shetani, basi Shetani atamjibu kwa ulimi mpana:
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (إبراهيم 12 : 22 )
_
Na Shetani atasema itao tolewa hukumu ya mwisho: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipokuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi; bali jilaumuni NAFSI ZENU. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kushirikishwa na Mwenyezi Mungu. Hakika madhalimu watakuwa na adhabu kali._
والله أعلم
وبالله التوفيق