Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kwa wanaokumbuka mwendazake Magu alivyotaka kuigeuza Chato Ulaya, watajikumbusha kinachoendelea kule Kinzinkazi, siyo jina hali. Kabla ya hapo, hatukuwahi kuona kiongozi akipendelea kwao hata kwa kuchota na kutumia vibaya fedha za umma. Kikwete na uhovyo wake, hakufanya hivyo. Mkapa wala asingefanya kama ambavyo Nyerere hakufanya. Kwa mzee ruksa, ni bahati hakufanya hivyo. Juzi nilimsikia Tundu Lissu akisema kuwa huyu mama ni Magu wa kike. Sasa, tararabu, naanza kumuelewa hata kama huwa siungi mkono staili yake ya kufanya siasa kwa ngebe na kelele sana. Je hii ni halali, mtu kupata uongozi na kupendelea kwao hata kama hakuna umuhimu kimkakati kitaifa?