Je, kukataa uteuzi wa Rais kunaweza kuchukuliwa kama uhaini?

Je, kukataa uteuzi wa Rais kunaweza kuchukuliwa kama uhaini?

..nadhani hili swali ni complex kidogo na huenda halikustahili kuulizwa ktk mazingira ya kilichotokea.

..Ni kweli askari wanakula kiapo kwa amiri jeshi mkuu.

..sasa huu uteuzi sidhani kama unahusiana na mambo ya kiuaskari ambayo wahusika wamekula kiapo kumtii amiri jeshi mkuu.

..pia naamini amiri jeshi mkuu naye hayuko juu ya sheria kwamba kila amri anayotoa ni halali.

..vipi ikiwa amiri jeshi ametoa amri ambayo si halali, je, askari anatakiwa kuitii?
Askari anatakiwa kutii amri kutoka juu yake, kumbuka amri za jeshini huendana kwa rank, maagizo yanatoka juu yanashuka chini mpaka ngazi ya utekelezaji, hivyo amri ikishatoka juu, hata kama sio halali, haiwezi kupingwa na wa cheo cha chini, kijeshi itatekelezwa tu.
 
Kuna baadhi ya kada huapa kiapo cha utii kwa Rais. Je iwapo ikatokea mtu mwenye kiapo hiki amegomea uteuzi alioteliwa na Rais, je anaweza kuchukuliwa kama mhaini?
Kuna mtu alishaukataa uteuzi wa Magu wa kuwa mkuu wa Wilaya....

Hili nalo hebu mkalitazame
 
Ni Masoudi masanya.Alikataa ukuu wa wilaya ya mbozi.Alikuwa ni meneja wa kampuni ya tigo Kanda ya ziwa.
🫵🏻🫵🏻🫱🏻‍🫲🏽🫱🏻‍🫲🏽🫱🏻‍🫲🏽🫱🏻‍🫲🏽😅😅
 
Hata idara ya usalama wa Taifa haimo kwenye katiba, licha ya kwamba majeshi mengine yapo
So, unadhani coz idara haipo kwenye Katiba basi inaweza kufanya mambo yake kivyake, au niseme ipo juu ya sheria za nchi?

Siamini kama mambo yapo hivyo, japo kiuhalisia inaonekana hao jamaa hujifanyia mambo yao pale wakihisi usalama wa taifa uko hatarini, na wanaweza kufanya hivyo hata kwa kuvunja sheria za nchi.

Tukirudi kwenye swali lako kuhusu kosa la uhaini, kisheria hilo la kukataa maagizo ya Rais sio miongoni mwake, lakini kiutaratibu wao, linaweza kuwa miongoni mwake, coz hao jamaa ni kama wana taratibu zao kivyao.
 
Askari anatakiwa kutii amri kutoka juu yake, kumbuka amri za jeshini huendana.kwa rank, maagizo yanatoka juu yanashika chini mpaka ngazi ya utekelezaji, hivyo amri ikishatoka juu, hata kama sio halali, haiwezi kupingwa na wa cheo cha chini, kijeshi itatekelezwa tu.

I stand to be corrected, japo nina hakika na nilichoandika.

..hoja yangu ni kwamba kilichotokea hakikuwa amri au maagizo toka kwa amiri jeshi mkuu kwenda kwa askari.

..raisi hakuwa akitekeleza majukumu au akitoa maelekezo kama amiri jeshi mkuu.
 
Hakuna uhaini hapo!
Ila kutoka Mkurugenzi wa Taifa kwenda kuwa Katibu Mkuu wa ofisi, ni ka demotion hivi.

Watu werevu kama wapare hawawezi kukubali.
 
..hoja yangu ni kwamba kilichotokea hakikuwa amri au maagizo toka kwa amiri jeshi mkuu kwenda kwa askari.

..raisi hakuwa akitekeleza majukumu au akitoa maelekezo kama amiri jeshi mkuu.
Inawezekana agizo halikuwa amri kama shughuli za kiserikali ikiwemo uteuzi, hazihusiani na cheo cha amiri jeshi mkuu alichonacho Rais.
 
Hebu tujifunze kutoka nchi jirani kama Uganda. Sheria inasemaje kuhusu nafasi za kazi kwenye teuzi zenye vyeo vya kijeshi (Military/Paramilitary):

- Major General David Tinyefunza V Attorney General of the Republic of Uganda. The Constitutional Court of Uganda 1996

- The Attorney General of Uganda V Major General David Tinyefunza. The Supreme of Uganda 1997

Tinyefunza alikuwa ni mwanajeshi wa Uganda ambaye alistaafu jeshini baada ya kupewa teuzi ya kisiasa kama mshauri wa ulinzi wa Raisi Museveni mwaka 1993. Baada ya kipindi kupita Tinyefunza aliitwa kwenye kamati ya bunge kutoa ushahidi kuhusu uasi unaendelea Kaskazini mwa Uganda.

Tinyefunza alilishambulia mno jeshi la Uganda na serikali ya Raisi Museveni kitu ambacho vyombo vya habari vilitangaza. Hili jambo liliwakera wakubwa wa jeshi na chama, hivyo Tinyefunza akaitwa kwenye mahakama ya jeshi (Court Martial) ili aadhibiwe kwa kukiuka miiko ya kijeshi.

Tinyefunza alikimbilia mahakamani kuweka pingamizi kwenye mahakama ya katiba ya Uganda. Ambapo alisema kwamba alitoa maoni huru kwasababu jeshini aliondoka mwaka 1993 baada ya kuteuliwa kuwa mshauri wa Raisi Museveni. Ila pia kitendo cha kutaka kumpeleka mahakama ya kijeshi kinamlazimishia yeye kuwa bado mwanajeshi hivyo ni kazi ya kulazimishwa (Forced Labour)

Mahakama ya katiba ya Uganda, ilitoa hukumu ikisema kwamba Tinyefunza alikiwa sahihi na kweli kazi yake jeshini iliisha mwaka 1993 baada ya uteuzi wa kwenda Ikulu. Hivyo kumlazimishi na kutaka kumpa adhabu ni kinyume cha katiba ya Uganda.

Mwanasheria Mkuu wa Uganda, alikata rufaa kwenye makahakama ya juu ya Uganda ili kutengua uamuzi wa mahakama ya katiba ya Uganda. Kufika kule lilitokea songombingo kubwa kwasababu Tinyefunza alisema kuna majaji ni wanachama wa NRM na wanamtii Raisi Museveni hivyo wajitoe kwenye kesi lakini wakagoma. Hili sitalizungumzia zaidi ila ntaenda kwenye maamuzi ya mahakama.

Mahakama ya juu ya Uganda ilisema kwamba Tinyefunza bado ni mwanajeshi wa jeshi la Uganda (UPDF), na teuzi zake Ikulu zililenga kazi yake ya uanajeshi maana hakwenda kuwa mwanasiasa. Lakini pia hata alivyoenda kutoa ushahidi bungeni alifanya hivyo akiwa na kofia ya uanajeshi wa Uganda (By virtue of his office), hivyo ilikuwa ni lazima afuate vigezo na masharti vya mwajiri wake (Terms and Conditions) ambaye ni jeshi la Uganda.

Mahakama ilienda mbali zaidi na kusema kwamba askari yoyote yule hatakiwi kabisa kujiamria jambo lolote lile bila maelekezo kutoka juu. Kama atafanya hivyo basi ni lazima angekubali kwanza kujiuzulu nafasi yake jeshini. Tinyefunza hakujiuzulu hivyo bado ni mwanajeshi, na hakutakiwa akiuke amri yoyote ya mwajiri wake kwasababu yeye bado ni askari na siyo mwanasiasa.

Mwanasheria mkuu wa Uganda alisisitiza kwamba kitendo hicho kilikuwa ni uhaini (Treasonous) na mgomo (Mutinous) ukizingatia nafasi yake kijeshi nchini Uganda. Alikuwa ni Major General na mshauri wa Raisi Museveni.

Hoja hapa ni nini: Muhimu kufahamu kwamba nafasi za kwenye vyombo vya dola kama Polisi, Uhamiaji, Zimamoto, Jeshi, Mgambo na Usalama kiasili ni za kijeshi (Military/Paramilitary). Ukipewa mwongozo ni lazima utii na uheshimu huo mwongozo na miiko ya kazi yako ya kazi.

Ndiyo maana waajiriwa wa vyombo vya dola Polisi, Jeshi na Usalama hawasimamiwi na sheria za kazi (Employment and Labour Relations Act, The Public Service Act, The Labour Institutions Act etc), wao huwa na sheria zao maalimu na miongozo yao, mingine ikiwa hata ya siri.

Maswali muhimu kisheria :

Mosi: Je, afande wetu bado ni askari wa jeshi la polisi la Tanzania au nafasi yake iliisha pale baada ya kuteuliwa kwenda PCCB na kuwa mkurugenzi wa Usalama ?

Pili: Je, afande wetu kama ameondolewa kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Usalama kabla ya umri na muda wa kustaafu , anaweza kurudi kwenye taaluma yake ya Upolisi na kuendelea kuwa mwajiriwa wa serikali ?

Tatu: Je, kama kweli afande amekataa uteuzi wa cheo ambacho ameteuliwa na Raisi (Ukatibu wa Ikulu ni cheo nyeti, japo siyo kama Ukurugenzi wa Usalama), hili litakuwa ni kosa ikizingatiwa yeye ni askari ambaye anatakiwa kutii amri hata kama hicho cheo hakihusiani kabisa na taaluma zake za upolisi na ujasusi ?

Mambo ni mengi mno, inabidi siasa zifanywe kiuwazi kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini pia sheria ituweka bayana kwenue vyeo kama hivi. Endapo mtu atagoma, hataweza kukutwa kweli na mambo mazito ya General Tinyefunza ambaye aliambiwa yeye bado ni mwanajeshi wa Uganda na alitakiwa kuwa mtiifu hadi kufika mwisho ?

Mwisho kabisa: Haya mambo siyo kwetu nchi za Afrika kama Uganda na Kusadikika, hata Marekani yapo. Nakumbuka mwaka 1975 kulikuwa na The Church Committee, kamati ambayo iliundwa ili kuchunguza michezo michafu ya shirika la kijasusi la mambo ya nje la Marekani (CIA) hasahasa kule Vietnam.

Mkurugenzi wa wakati huo wa CIA bwana William Colby Mkatoliki kindakindaki alipoitwa atoe ushahidi bungeni hakuweza kupindisha maneno na kusema uongo. Msimamo wake na ukweli aliousema uliwakwaza mno wakubwa wenzake kama Rais Gerald Ford, Henry Kissinger, Dick Cheney na Donald Rumsfeld.

Kissinger alinukuliwa akilalama kwamba "Colby is speaking out of school" and "Revealing family jewels". Mwishowe Bwana Colby aliondolewa ghafla CIA na nafasi yake ikachukuliwa na George H.W Bush aliyerudishwa kutoka ubalozini huko Uchina.

Colby aliondoka kazini na alionekana akiendelea na maisha ya kawaida, japo baada ya kuondolewa Ukurugenzi hakuwahi kurudi nyumbani kwake, na alimtelekeza mke wake na mtoto wa kiume na kuoa binti mwingine. Muda ulipita na mwaka 1996 alienda kuendesha mtumbwi wake na hakurudi nyumbani. Mwili wake ulikuja kuokotwa siku chache baadae.

Kama kawaida yalisemwa mengi mno kuhusu kifo chake, wengine wakisema serikali huwa haisahau. Wengine wakisema alijua mambo mengi mno ya serikali hasahasa ya wakina Bush. Wengine walisema ni moyo tu au ajali. Hakuna afahamuye.

Prof Hans Kelsen Mjerumani, aliwahi kusema kwamba ndani ya dola lolote kuna sheria zinazoonekana na zisizoonekana. Nzuri ni zile tuzionazo sisi raia, lakini kuna nyingine hatuzioni ambazo wale ambao dola haliwataki (Undesirables) huziona zikifanya kazi. Mtu alikuwa anakosoa ghafla amepotea tu au ghafla ameanza kushirikiana na serikali.

Hans Kelsen anasisitiza kwamba hizi sheria zipo hata kwa zile nchi ambazo zinajiita ni za kidemokrasia au kisasa, kwasababu hakuna serikali isiyo na maadui inaowachukia na haiwezi kuwasahau..

Afande Sele aliimba: HUU NI MTAZAMO TU.
"
Karibuni sana Babeli...
Umejitahidi kuelimisha
 
Kuna Nini kimetokea huko[emoji848][emoji848][emoji848]
Yaheeee wazanzibar wameanza kutiana vidole vya macho wakigombea ugali wa bara yaheee.....
Yaheee ugali wa bara mtamu shehee[emoji1787][emoji1787]
 
Inategemea msingi , labda afya n.k uhaini ni kukutendea ndivyo ulichokiapa! I.e utii kwa rais na kutokutoa siri
Shida huyu ni Kachero. Anajua mengi ya mtungini kama si yote. Kuanzia upolisi, utakukuru, RAS, TISS . Sio wa kawaida.
 
..hapana.

..kuna jamaa mmoja aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa DC akakataa.

..aliendelea na kazi yake ya ualimu baadae Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Kamishna wa Elimu.
Kuna yule afisa masoko sijui wa Tigo mkoa wa Mwanza aligomea teuzi ya JPM
 
Back
Top Bottom