Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Watu wa idara ya usalama kwa mfano, huwa hawastaafu, hata ukiambiwa umestaafu bado wewe ni usalama tu na unaweza kuhitajika kufanya hili ama lile...pia yuko bwana mmoja wakati wa mzee mwinyi alikuwa balozi uganda akateuliwa kuwa mkuu wa itifaki " akakataa" uteuzi huo.
Kama ndugu yetu kakataa uteuzi, kwangu binafsi hajatumia busara kabisa. Na jambo kama hili raisi yeyote ni lazima atalichukulia kwa uzito mkubwa.
Kwa kifupi nisipindishe maneno, huyu hata kama ana muda gani ameacha kuwa mkurugenzi, bado haifutiki kwamba amekuwa mkurugenzi. Mkurugenzi wa idara nyeti kumgomea raisi, nafikiri unaweza kupata picha maana yake nini. Hasa kwa nchi zetu ambazo idara hizo za PCCB na TISS ziko chini ya raisi.