Hebu tujifunze kutoka nchi jirani kama Uganda. Sheria inasemaje kuhusu nafasi za kazi kwenye teuzi zenye vyeo vya kijeshi (Military/Paramilitary):
- Major General David Tinyefunza V Attorney General of the Republic of Uganda. The Constitutional Court of Uganda 1996
- The Attorney General of Uganda V Major General David Tinyefunza. The Supreme of Uganda 1997
Tinyefunza alikuwa ni mwanajeshi wa Uganda ambaye alistaafu jeshini baada ya kupewa teuzi ya kisiasa kama mshauri wa ulinzi wa Raisi Museveni mwaka 1993. Baada ya kipindi kupita Tinyefunza aliitwa kwenye kamati ya bunge kutoa ushahidi kuhusu uasi unaendelea Kaskazini mwa Uganda.
Tinyefunza alilishambulia mno jeshi la Uganda na serikali ya Raisi Museveni kitu ambacho vyombo vya habari vilitangaza. Hili jambo liliwakera wakubwa wa jeshi na chama, hivyo Tinyefunza akaitwa kwenye mahakama ya jeshi (Court Martial) ili aadhibiwe kwa kukiuka miiko ya kijeshi.
Tinyefunza alikimbilia mahakamani kuweka pingamizi kwenye mahakama ya katiba ya Uganda. Ambapo alisema kwamba alitoa maoni huru kwasababu jeshini aliondoka mwaka 1993 baada ya kuteuliwa kuwa mshauri wa Raisi Museveni. Ila pia kitendo cha kutaka kumpeleka mahakama ya kijeshi kinamlazimishia yeye kuwa bado mwanajeshi hivyo ni kazi ya kulazimishwa (Forced Labour)
Mahakama ya katiba ya Uganda, ilitoa hukumu ikisema kwamba Tinyefunza alikiwa sahihi na kweli kazi yake jeshini iliisha mwaka 1993 baada ya uteuzi wa kwenda Ikulu. Hivyo kumlazimishi na kutaka kumpa adhabu ni kinyume cha katiba ya Uganda.
Mwanasheria Mkuu wa Uganda, alikata rufaa kwenye makahakama ya juu ya Uganda ili kutengua uamuzi wa mahakama ya katiba ya Uganda. Kufika kule lilitokea songombingo kubwa kwasababu Tinyefunza alisema kuna majaji ni wanachama wa NRM na wanamtii Raisi Museveni hivyo wajitoe kwenye kesi lakini wakagoma. Hili sitalizungumzia zaidi ila ntaenda kwenye maamuzi ya mahakama.
Mahakama ya juu ya Uganda ilisema kwamba Tinyefunza bado ni mwanajeshi wa jeshi la Uganda (UPDF), na teuzi zake Ikulu zililenga kazi yake ya uanajeshi maana hakwenda kuwa mwanasiasa. Lakini pia hata alivyoenda kutoa ushahidi bungeni alifanya hivyo akiwa na kofia ya uanajeshi wa Uganda (By virtue of his office), hivyo ilikuwa ni lazima afuate vigezo na masharti vya mwajiri wake (Terms and Conditions) ambaye ni jeshi la Uganda.
Mahakama ilienda mbali zaidi na kusema kwamba askari yoyote yule hatakiwi kabisa kujiamria jambo lolote lile bila maelekezo kutoka juu. Kama atafanya hivyo basi ni lazima angekubali kwanza kujiuzulu nafasi yake jeshini. Tinyefunza hakujiuzulu hivyo bado ni mwanajeshi, na hakutakiwa akiuke amri yoyote ya mwajiri wake kwasababu yeye bado ni askari na siyo mwanasiasa.
Mwanasheria mkuu wa Uganda alisisitiza kwamba kitendo hicho kilikuwa ni uhaini (Treasonous) na mgomo (Mutinous) ukizingatia nafasi yake kijeshi nchini Uganda. Alikuwa ni Major General na mshauri wa Raisi Museveni.
Hoja hapa ni nini: Muhimu kufahamu kwamba nafasi za kwenye vyombo vya dola kama Polisi, Uhamiaji, Zimamoto, Jeshi, Mgambo na Usalama kiasili ni za kijeshi (Military/Paramilitary). Ukipewa mwongozo ni lazima utii na uheshimu huo mwongozo na miiko ya kazi yako ya kazi.
Ndiyo maana waajiriwa wa vyombo vya dola Polisi, Jeshi na Usalama hawasimamiwi na sheria za kazi (Employment and Labour Relations Act, The Public Service Act, The Labour Institutions Act etc), wao huwa na sheria zao maalimu na miongozo yao, mingine ikiwa hata ya siri.
Maswali muhimu kisheria :
Mosi: Je, afande wetu bado ni askari wa jeshi la polisi la Tanzania au nafasi yake iliisha pale baada ya kuteuliwa kwenda PCCB na kuwa mkurugenzi wa Usalama ?
Pili: Je, afande wetu kama ameondolewa kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Usalama kabla ya umri na muda wa kustaafu , anaweza kurudi kwenye taaluma yake ya Upolisi na kuendelea kuwa mwajiriwa wa serikali ?
Tatu: Je, kama kweli afande amekataa uteuzi wa cheo ambacho ameteuliwa na Raisi (Ukatibu wa Ikulu ni cheo nyeti, japo siyo kama Ukurugenzi wa Usalama), hili litakuwa ni kosa ikizingatiwa yeye ni askari ambaye anatakiwa kutii amri hata kama hicho cheo hakihusiani kabisa na taaluma zake za upolisi na ujasusi ?
Mambo ni mengi mno, inabidi siasa zifanywe kiuwazi kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini pia sheria ituweka bayana kwenue vyeo kama hivi. Endapo mtu atagoma, hataweza kukutwa kweli na mambo mazito ya General Tinyefunza ambaye aliambiwa yeye bado ni mwanajeshi wa Uganda na alitakiwa kuwa mtiifu hadi kufika mwisho ?
Mwisho kabisa: Haya mambo siyo kwetu nchi za Afrika kama Uganda na Kusadikika, hata Marekani yapo. Nakumbuka mwaka 1975 kulikuwa na The Church Committee, kamati ambayo iliundwa ili kuchunguza michezo michafu ya shirika la kijasusi la mambo ya nje la Marekani (CIA) hasahasa kule Vietnam.
Mkurugenzi wa wakati huo wa CIA bwana William Colby Mkatoliki kindakindaki alipoitwa atoe ushahidi bungeni hakuweza kupindisha maneno na kusema uongo. Msimamo wake na ukweli aliousema uliwakwaza mno wakubwa wenzake kama Rais Gerald Ford, Henry Kissinger, Dick Cheney na Donald Rumsfeld.
Kissinger alinukuliwa akilalama kwamba "Colby is speaking out of school" and "Revealing family jewels". Mwishowe Bwana Colby aliondolewa ghafla CIA na nafasi yake ikachukuliwa na George H.W Bush aliyerudishwa kutoka ubalozini huko Uchina.
Colby aliondoka kazini na alionekana akiendelea na maisha ya kawaida, japo baada ya kuondolewa Ukurugenzi hakuwahi kurudi nyumbani kwake, na alimtelekeza mke wake na mtoto wa kiume na kuoa binti mwingine. Muda ulipita na mwaka 1996 alienda kuendesha mtumbwi wake na hakurudi nyumbani. Mwili wake ulikuja kuokotwa siku chache baadae.
Kama kawaida yalisemwa mengi mno kuhusu kifo chake, wengine wakisema serikali huwa haisahau. Wengine wakisema alijua mambo mengi mno ya serikali hasahasa ya wakina Bush. Wengine walisema ni moyo tu au ajali. Hakuna afahamuye.
Prof Hans Kelsen Mjerumani, aliwahi kusema kwamba ndani ya dola lolote kuna sheria zinazoonekana na zisizoonekana. Nzuri ni zile tuzionazo sisi raia, lakini kuna nyingine hatuzioni ambazo wale ambao dola haliwataki (Undesirables) huziona zikifanya kazi. Mtu alikuwa anakosoa ghafla amepotea tu au ghafla ameanza kushirikiana na serikali.
Hans Kelsen anasisitiza kwamba hizi sheria zipo hata kwa zile nchi ambazo zinajiita ni za kidemokrasia au kisasa, kwasababu hakuna serikali isiyo na maadui inaowachukia na haiwezi kuwasahau..
Afande Sele aliimba: HUU NI MTAZAMO TU.
"
Karibuni sana Babeli...