Je, kuna baadhi ya Familia zimebarikiwa?

Na kuzaliwa kwenye familia za aina hii ni bahati pia.
 
Tenda wema, usidhulumu,usiibe na mpe Mungu haki yake. Nakuhakikishia uzao wako ijapokuwa hutakuwa na muda wa kuusimamia Mungu atausimamia. Mungu ni muaminifu mno. Ukijua hili hutaacha kutenda wema. Ngoja nitoe mfano mmoja. Miaka hiyo najitafuta kukatokea dili flan la viwanja vya ukweli. Na Mimi nikaviitaji. Sasa kulikuwepo watu wengi walilijua lile dili watu wenye hela zao. Zikapelekwa hela za kiume. Sasa Mimi nikapeleka jina tu na sikutegemea chochote kuendana na mazingira yale. Lakin kama ilivyo kawaida yangu mzee wa kujaribu chochote coz ninaamin kila kitu kinawezekana kwa aaminie. Ndio kanuni yangu kuu. Sasa bana mwenye maamuz ya mwisho ni wazir flan. Sasa nashangaa napigiwa simu nikaulizwa wewe ni mtu flan. Nikajibu ndio, nikaambiwa kesho njoo ofisi flan. Nikaenda, kufika secretary kashapewa maagizo. Nikapelekwa kwa Mh, aliniuliza tu swali moja unamjua mtu flan nikamwambia ni marehem baba yangu mdogo. Nikaona wazir anatoa machoz mbele yangu. To cut short story kumbe mzee akiwa katibu ofis flan huyu wazir akiwa kijana mdogo amemaliza chuo hana hili wala lile akaajiriwa ofisini kwa mzee. Na kwasababu hakuwa na kitu mzee alikaa nae kwake miaka 6 Bure bila kutoa chochote,anasema upendo alioupata pale nyumban aliupata kwa Mama yake tu kwao. So baada ya miaka 6 mzee alienda kusoma Canada na hakurud tena mpaka anakuja kufa. Hakuwah kukutana nae au wanae. Nilipewa vile viwanja kwasababu ya wema wa mzee sio kwasababu nilikuwa na hela. Nikakumbuka kuwa Mungu anaweka kumbukumbuk kwaajili ya vizazi. Nilikuja kuwakutanisha na ile familia baadhi walisharud wengine wapo Canada washakuwa raia.
 
Interesting!
 
Mfano ni wale Vijazi.

1.Katibu Mkuu Kiongozi (RIP)
2.Boss TMA
3.Boss NCAA
 
Msingi mkuu wa mafanikio yoyote katika familia ni

Kumtanguliza Mungu Mbele
Kuwa serious na masuala ya elimu
Na kujituma

Ni ngumu kukuta familia yenye misingi hiyo halafu haijatoboa, inaweza isiwe kwenye levo ya mamilionea lakini utaona tu mafanikio
 
Msingi mkuu wa mafanikio yoyote katika familia ni

Kumtanguliza Mungu Mbele
Kuwa serious na masuala ya elimu
Na kujituma

Ni ngumu kukuta familia yenye misingi hiyo halafu haijatoboa, inaweza isiwe kwenye levo ya mamilionea lakini utaona tu mafanikio
Kweli mkuu
 
Watoto ni product ya wazazi genetically

Mazingira yanachangia pia,ila kama mzazi ana IQ ya kutosha kufanya tu maamuzi ya kumuwekea mtoto mazingira mazuri tayari huyo mzazi ana akili haijalishi aliishiaga la saba au Chuo Kikuu

Mzazi akishakua na intellect ya kufanya maamuzi sahihi kila wakati,basi probability ya watoto kua na intellect ni kubwa

Kikwazo kikubwa ni wazazi kuchaguana ambao hawana akili au hawana genetics bora wote wawili au mmoja wapo

Chanzo kabisa ni wazazi uchaguzi wao wa wenza ndio tatizo namba moja maana ndio inatoa fvcked up kids genetically

Baada ya kupata best genetics then mazingira ni juhudi za wazazi,then the rest ni history.

Watoto walio hovyo mara nyingi wazazi aidha wote au mmojawapo hakuaga na akili naturally hivyo wanatoa inferior offsprings

Binadamu ni animals kama walivyo ng'ombe au chochote,mbegu bora watoto bora,you cant cheat biology.


Mazingira ni juhudi binafsi za kila mzazi sasa
 
Sure bro, mbegu ikiwa bora itatoa kilicho bora hasa mazingira nayo yakichangia.
 
Sure bro, mbegu ikiwa bora itatoa kilicho bora hasa mazingira nayo yakichangia.
Ni kweli mkuu

Mbegu ikishakua bora mazingira ni ya kupambania tu kwa juhudi binafsi,hapo ndipo umuhimu wa maadili na familia imara ambazo hazijavunjika unapofanya kazi

Kuna mzee,naturally hakuaga na akili yeye na mkewe,wataratibu na religion obsessed na kwake maadili full,ila wanae aisee akili ndio hakuna kabisa,wanawake wameishia kua bar attendants na wavulana wawili became bodaboda guys,wazazi are still wondering why
 
Dah kwa wazazi imewauma sana, ila nadhani ni upeo wa kufikiri wa watoto upo chini sana. Pamoja na malezi ya dini lakini haijafua dafu, Ila wangekuwa navyo vyote wangekuwa vizuri sana.

Ina sikitisha sana Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…