Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 13,336
- 12,370
Umenikumbusha kuhusu motivation speakers, watu wanapenda kusikia mafanikio ya motivation speakers wakati hawana sifa kumbe km huna sifa hata moja ya ujasiriamali huwezi kufanya biashara yoyoteNiwaambie kitu ndugu zangu
Wakati mwingine inategemeana na initiator au aliyeaanza alifanya nini.Sasa unakuta wanaofuatia wanafuata nyayo za kuwa masikini sana au kuwa na mafanikio sana.
Nitatolea mfano familia ya kina Mwapachu
Baba yao alikuwa anaitwa Hamza Kibwana Bakari Mwapachu tokea Tanga
Alioa mwaka 1938 alimuoa Juliana ambaye ndio mama wa Harith Bakari Mwapachu na wengine
Walikutana Makerere na bwana mdogo wake Nyerere wakaanzisha tawi la kutetea wanafunzi wa Tanganyika wakati huo TAWA baadae wakabadili chama wakakiita TAA.
Wakiwa Tabora Hamza alikuwa mwenyekiti wa TAA Nyerere akiwa katibu wake hiyo ilikuwa mwaka 1947
Hamza alikuwa tabibu wakati Nyerere alikuwa Mwalimu st Mary
Hamza akaja kuwa waziri wa kwanza wa mambo ya ndani baada ya Uhuru bahati mbaya hakuishi sana alifariki mwaka 1962 mwaka mmoja tu baada ya Uhuru.
Katika utawala wa Nyerere kwa kutambua mtoto wa nyoka ni nyoka alimteua Bakari Mwapachu mtoto wa Hamza kuwa mkurugenzi mkuu wa ATC.
Watoto wa Hamza wengine wote walikuja kuwa na mafanikio makubwa sana kwenye nyanja za kielimu na vyeo watoto wa Hamza wengine ni
Harith Bakari Mwapachu
Bakari Mwapachu
Rahma Mwapachu mjane wa mwanasheria wa kwanza Jaji Mark Bomani huyu Rahama alishakuwa head of marketing communication
Heri Ali Mwapachu
Juliana Mwapachu
Wendo Mtega Mwapachu
Tunu Mwapachu
Jabe Jabiri Mwapachu
Majina niliyoandika hapo Juu nimechanganya watoto wa Hamza na wajukuu zake
wengi hapo juu wamesomea masomo fani mbali mbali na sheria wingereza na wengine bado wako huko
Familia yote hii ni kubwa iliyojaliwa kuwa na Tunu katika nyanja mbali mbali ukitizama kiundani muasisi wa yote haya ni baba yao.
Sikatai ziko familia ambazo muanzilishi alikuwa vizuri lakini waliofuata bado wakawa ni hopeless siwezi kuzitaja hapa maana ni watu maarufu
Hapo sasa ndipo linapokuja kuwa na mkono wa MUNGU katika familia husika
Ipo mifano ya familia nyingi tu mfano familia za kina Mbowe,Mo Dewji,Bakhresa,Marealle,Bomani,Rupia,bila kusahau mimi familia ninayotoka wakati mwingine nashangaa hatutumii nguvu nyingi ila mambo yanakwenda ila kikubwa kwa familia yangu tunajali elimu kuliko kitu chochote mtoto akikosa ada wa familia flani au baba flani tunaweka harambee kumchangia darasa la chini kabisa ni form four std 7 tulishaifuta toka enzi ya ukoloni hata baba zetu hakuna aliyeishia std 7 n.k
Achaneni na motivational speaker wanasema sijui weka malengo fanya hiki sijui malezi mazuri.Unaweza ukafanya yote haya na bado tu mambo yasiende kabisa au yakaenda kwa kusua sua.
Kitu kikubwa MUNGU humnyanyua mtu yeyote anayetaka hata kama alikuwa chini hana upendeleo