Akili ya maisha, urithi wa akili&mali ndio sili pekee ya utajiri vizazi na vizazi.
Mwanaume unakwenda kutongoza mwanamke wa hovyo hovyo, tabia za hovyo, background ya familia yao&ukoo wao uko hovyo then utegemee wewe utadumu na huyo mwanamke katika maisha bora&bahati?
Au mwanamke anazaa na kijana mpuuzi asiye na akili timamu wala mindest ya utafutaji&malezi bora kwa watoto, unadhani hapo mkitengeneza familia mtapata watoto timamu? au familia yenu itakuwa na nidhamu ya mali na matumizi sahihi ya pesa?
Utajiri&akili vinakwenda sambamba na waanzilishi wa familia na background kidogo ya hawa waanzilishi wa familia ni namna gani maisha yao, watoto wao na wajukuu wao wataishi vipi na ukoo utakuwa vipi.
Usitegemee kuzaa na fala alafu watoto wasiwe mafala, hapo unakuwa mwendelezo wa ukoo wa mafala wenye maisha ya kifala.
Akili ni mwendelezo wa mafunzo+urithi wa mambo mtoto aliyofunzwa na wazazi wake+ aina ya elimu anayoipata mtoto ili aiendeleze kwa vizazi vingine.
Angalia familia zote mnazoita zina bahati,baraka,utajiri, idadi ya wasomi, utagundua tu ktk hizo familia suala la malezi ni kubwa, adabu, heshima, utii na muendelezo wa mafunzo ya wazazi wao ni mkubwa japokuwa hawakosekanagi watoto mafala ambao husumbua familia&ukoo, hawa watoto wa aina hii wapo kila familia hata kwa makapuku na wale wajawa mikosi huwa hawakosi mitoto mifala ya aina yake.
Usitegemee uzae na mwanamke/mwanaume wa malezi ya kijanjajanja/uswahiliswahili alafu utegemee vizazi vyenu kutengamaa kiakili&kiuchumi hiyo haipo labda mkaishi mbali na uyo mtu wako awe anajielewa, namaanisha awe tayari kujitoa ktk limitation za maisha ya ukoo wake.
Hakuna muujiza katika haya mambo.