Je, kuna baadhi ya Familia zimebarikiwa?

Habari Wakuu.

Hivi inakuje kuna baadhi ya familia unakuta watoto wote wana akili, wamesoma mpaka level za juu kabisa. Au unakuta familia nyingine karibu wote wana uchumi mzuri, wana biashara kubwa na mafanikio kede kede.

Kwa upande mwingine unakuta familia nyingine watu karibuni wote hawaja fanikiwa kielimu wala kiuchumi. Wana umasikini uliotopea.

Je, hizo familia zinazo kuwa na watu wengi wamefanikiwa ni kuwa wamebarikiwa au ni genetics au nini ndugu wajumbe.

Karibuni kwa michango yenu.
Mafanikio ya mtu/jamii/nchi ni matokeo ya mipango mizuri ya muda mrefu kuanzia kizazi cha mababu huko.. Hayana uhusiano wowote na kubarikiwa au kulaaniwa.
 
Katika mafanikio kuna mambo mengi. Umezaliwa wapi, umekulia wapi, umekutana na nani shule, etc.
Lakini kwa hili la familia mchango mkubwa sana unatoka kwa wazazi, jinsi walivyowalea watoto wao, jinsi walivyo wasimamia katika mambo ya shule, na jinsi wanavyo waongoza kwenye mambo mbalimbali.
Familia nyingi hutelekeza watoto wakimaliza shule either darasa la 7 au fom 4. Hivyo watoto hujikuta wakijifanyia mambo bila mpango na hatimaye kuishia kutokufanikiwa.
Lakin hili pia huchangiwa na bahati mkuu japo wazazi wana uwezo mkubwa wa kuwasimamia watoto wakaenda njia nzuri
 
Habari Wakuu.

Hivi inakuje kuna baadhi ya familia unakuta watoto wote wana akili, wamesoma mpaka level za juu kabisa. Au unakuta familia nyingine karibu wote wana uchumi mzuri, wana biashara kubwa na mafanikio kede kede.

Kwa upande mwingine unakuta familia nyingine watu karibuni wote hawaja fanikiwa kielimu wala kiuchumi. Wana umasikini uliotopea.

Je, hizo familia zinazo kuwa na watu wengi wamefanikiwa ni kuwa wamebarikiwa au ni genetics au nini ndugu wajumbe.

Karibuni kwa michango yenu.
Ni kweli baadhi ya familia hufanikiwa endapo tu waanzikishi watamcha bwana Mungu na kuishi katika imani

Mungu huwarehemu na kuwabariki kizazi hadi kizazi na kuwapa utajiri kizazi hadi kizazi

Mfano ni babu yetu Ibrahimu soma biblia utaelewa
 
Misingi inayowekwa ndyo huleta kufanikiwa au kukosa. Jamii nyingi zilizowekeza kwenye biashara au elimu basi vizazi vyao vitanufaika humo... waliowekeza kwenye ufugaji wa ufahari na watoto huiga hivyo halkadhalika waliowekeza kwenye kufuga au kulima kibiashara na jamii yao hukulia hivyo. Ukiwekeza kwenye VIGODORO na MICHIRIKU jamii yako itaenda na hiyo mirindimo.
 
Ni kweli baadhi ya familia hufanikiwa endapo tu waanzikishi watamcha bwana Mungu na kuishi katika imani

Mungu huwarehemu na kuwabariki kizazi hadi kizazi na kuwapa utajiri kizazi hadi kizazi

Mfano ni babu yetu Ibrahimu soma biblia utaelewa
Nahsi key point ya hapa ni kuishi katika Imani ya asili Yao. Hizi Imani za kigeni nmeona wengi zmewatupa kwenye wimbi la umaskini hatari.
 
Lakin hili pia huchangiwa na bahati mkuu japo wazazi wana uwezo mkubwa wa kuwasimamia watoto wakaenda njia nzuri
Hakuna kitu kinaitwa bahati. Wanasaikolojia walishafanya tafiti kuhusu bahati wakagundua kuwa watu waliokuwa wanadhaniwa wana bahati walikuwa makini katika maamuzi na vitu wanavyofanya, na wale waliodhaniwa wana mikosi ilikuwa ni kinyume.
Watanzania wengi tunapenda kufanya mambo kiholela halafu baadae tunasingizia tuna mikosi au tumerogwa.

Mfano, Imagine jamii inaishi bila choo, wanalala bila net. Wanaumwa mara kwa mara shuguli za uzalishaji mali zina dorola, kwa sababu muda mrefu wanatumia kujiuguza, wanakuwa maskini, watoto wanakufa, halafu tunasema wana mkosi.
 
Naona ni kujipanga vizuri na kusimamia familia vema. Umenena mkuu
 
Habari Wakuu.

Hivi inakuje kuna baadhi ya familia unakuta watoto wote wana akili, wamesoma mpaka level za juu kabisa. Au unakuta familia nyingine karibu wote wana uchumi mzuri, wana biashara kubwa na mafanikio kede kede.

Kwa upande mwingine unakuta familia nyingine watu karibuni wote hawaja fanikiwa kielimu wala kiuchumi. Wana umasikini uliotopea.

Je, hizo familia zinazo kuwa na watu wengi wamefanikiwa ni kuwa wamebarikiwa au ni genetics au nini ndugu wajumbe.

Karibuni kwa michango yenu.
Kipimo cha kufanikiwa na mali kila mtu na kile akipendacho
 
Akili ya maisha, urithi wa akili&mali ndio sili pekee ya utajiri vizazi na vizazi.

Mwanaume unakwenda kutongoza mwanamke wa hovyo hovyo, tabia za hovyo, background ya familia yao&ukoo wao uko hovyo then utegemee wewe utadumu na huyo mwanamke katika maisha bora&bahati?

Au mwanamke anazaa na kijana mpuuzi asiye na akili timamu wala mindest ya utafutaji&malezi bora kwa watoto, unadhani hapo mkitengeneza familia mtapata watoto timamu? au familia yenu itakuwa na nidhamu ya mali na matumizi sahihi ya pesa?

Utajiri&akili vinakwenda sambamba na waanzilishi wa familia na background kidogo ya hawa waanzilishi wa familia ni namna gani maisha yao, watoto wao na wajukuu wao wataishi vipi na ukoo utakuwa vipi.

Usitegemee kuzaa na fala alafu watoto wasiwe mafala, hapo unakuwa mwendelezo wa ukoo wa mafala wenye maisha ya kifala.

Akili ni mwendelezo wa mafunzo+urithi wa mambo mtoto aliyofunzwa na wazazi wake+ aina ya elimu anayoipata mtoto ili aiendeleze kwa vizazi vingine.

Angalia familia zote mnazoita zina bahati,baraka,utajiri, idadi ya wasomi, utagundua tu ktk hizo familia suala la malezi ni kubwa, adabu, heshima, utii na muendelezo wa mafunzo ya wazazi wao ni mkubwa japokuwa hawakosekanagi watoto mafala ambao husumbua familia&ukoo, hawa watoto wa aina hii wapo kila familia hata kwa makapuku na wale wajawa mikosi huwa hawakosi mitoto mifala ya aina yake.

Usitegemee uzae na mwanamke/mwanaume wa malezi ya kijanjajanja/uswahiliswahili alafu utegemee vizazi vyenu kutengamaa kiakili&kiuchumi hiyo haipo labda mkaishi mbali na uyo mtu wako awe anajielewa, namaanisha awe tayari kujitoa ktk limitation za maisha ya ukoo wake.

Hakuna muujiza katika haya mambo.
 
Kwa kweli umeandika vema watu wapitie hapa wajifunze.
 
Back
Top Bottom