Ambivert88
JF-Expert Member
- Aug 16, 2022
- 3,609
- 6,388
Ni filamu inayosimulia kisa cha msafiri anayejaribu kumshawishi kimafia afisa mmoja wa usalama kitengo cha Transportation Security Administration(TSA) ili akubali kupitisha kifurushi flani hatari kwenye ndege siku ya mkesha wa Krismasi.
Fikiria unatazama filamu, iwe peke yako na familia au umewa’downlodia watoto, halafu katikati unaona mwanaume anasema kwa kulalama, “My husband. He took him from my house and he gave me that case.”
USHOGA KWENYE FILAMU
Inaitwa CARRY-ON, ilitoka rasmi juzi tu, Disemba 13, 2024, imeongozwa na Jaume Collet-Serra na kuandikwa na T.J. Fixman, ina muda wa takribani dakika 119, na hayo maneno niliyoandika hapo juu utayaona kuanzia muda wa 1:09:03 mpaka 1:10:25.
Katika pirikapirika hiyo, star wa filamu Ethan akicheza kama afisa usalama, (Jina halisi Taron Egerton) anakutana na Bwana Mateo Flores (ambaye ndiye aliyebebeshwa kifurushi hatari na anatakiwa akipitishe kama abiria wa kawaida kwenye mlango aliopo Ethan). Mateo aliingizwa kinguvu kwenye mpango huu na mwamba Jason Bateman (The traveler).
Eti sasa, kilichosababisha Mateo Flores aingizwe kinguvu ni baada ya ‘The traveler’ kumteka nyara mume wa Mateo anayeitwa Jesse….. ambaye pia ni mwanaume. Sasa hiyo para ya kwanza hapo juu ndio analalamika akiwa na Ethan walipokutana kwenye heka heka hiyo kuwa mumewe katekwa akiwa kwenye nyumba yake.
Mateo na Jesse baadae walikuja kuzungumza kwa njia ya simu walipounganishwa na ‘The traveler’ na kumhakikishia Mateo kuwa mumewe Jesse atakuwa salama ikiwa mpango wake utakamilika, kuanzia muda wa 1:18:07 mpaka 1:18:34.
Sasa ndio umekaa nyumbani na mtoto au watoto mnatazama filamu kama hii, halafu wanauliza inakuwaje mwanaume anamwita mwanaume mwenzake mume wake? Tuweni makini, mbinu ni nyingi siku hizi.
Je kuna filamu nyingine kama hii unaijua!? Kwenye vitabu je!?