Je, kuna mabadiliko yoyote ya riba kwenye Benki?

Je, kuna mabadiliko yoyote ya riba kwenye Benki?

successiful dreamer

Senior Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
103
Reaction score
191
Habari ya uzima wanajamvi?

Natumaini wote tumejaliwa zawadi adhimu ya uhai na Mola yeye atuwezeshaye kufanya yote tuyafanyayo kila siku.

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada au jambo nililopenda kulijua kutoka kwenu.Mimi nipo kijijini kwa mda mrefu sijafika mjini.

Huku niliko hakuna Benki ambapo naweza kwenda kuuliza hii taarifa ninayotaka kuijua kutoka kwenu.

Mwanzoni mwa mwezi July nilisoma habari kwamba Benki kuu imeshusha riba ya kuyakopesha mabenki yetu kwa riba isiyozidi 10%.

Kama taarifa hiyo ni kweli hali ikoje huko katika Benki ambazo sisi tunaoendesha miradi kwa kutegemea mikopo kutoka NMB na CRDB wameshashusha riba kutoka ile 17% au hali bado ni ileile hakijabadilka kitu?

Karibuni mnisaidie pia muwe na siku njema.
 
Ni jambo gani ambalo serikali ya awamu hii sijuhi ya sita au saba imeliagiza/kulifuatilia na likatekelezwa? Anzia ule mzigo wa cocaine tani moja, wezi wa mafuta waliotoboa bomba na kujiunganishia kama maji, tozo za simu, bei ya gesi ya kupikia, nk, nk....
 
Mambo mengi yanakwama kwa sababu ya hii Serikali isiyokua na meno ya kung'ata wanaishia kubweka tu.
 
Ni jambo gani ambalo serikali ya awamu hii sijuhi ya sita au saba imeliagiza/kulifuatilia na likatekelezwa? Anzia ule mzigo wa cocaine tani moja, wezi wa mafuta waliotoboa bomba na kujiunganishia kama maji, tozo za simu, bei ya gesi ya kupikia, nk, nk....
Empty promises
 
Nchi hii hamna bank yenye undugu au ujamaa kakitka ukopeshaji

Nilikopa bank 8 ml nkalipa m15 siwezi kuwasahu nmb kamwe
 
Nchi hii hamna bank yenye undugu au ujamaa kakitka ukopeshaji

Nilikopa bank 8 ml nkalipa m15 siwezi kuwasahu nmb kamwe
Riba ilikua % ngapi?
Mkopo ulikua wa muda gani?
 
Mwezi July benki kuu ilitoa walaka wa wa utekelezaji wa sera wa utekelezaji wa sera ya fedha. Pamoja na mambo mengine, Walaka huo ulikuwa ukizitaka benki kushusha riba ili kuongeza mzunguko wa fedha mtaani ili kukabiana na athari za jangwa la uviko.

Jana tena kumekuwa na kikao cha bodi katika makao makuu ya benk kuu-Dodoma na kikao mabacho kilichosisitiza utekelezajli wa sera hiyo ya fedha. Kuna nini mbona sera hiyo haitekelezwi na benki kuu hapa nchini? Riba bado zipo juu na hazijashuka kama ilivyoagizwa.

Screen_Capture_Img_2125.jpg
 
Mwezi July benki kuu ilitoa walaka wa wa utekelezaji wa sera wa utekelezaji wa sera ya fedha. Pamoja na mambo mengine, Walaka huo ulikuwa ukizitaka benki kushusha riba ili kuongeza mzunguko wa fedha mtaani ili kukabiana na athari za jangwa la uviko...
Ninaambatanisha walaka wao wa jana
 
Back
Top Bottom