Je kuna mahusiano yoyote kati ya alama zinazotumika kwenye pesa na shetani?

Je kuna mahusiano yoyote kati ya alama zinazotumika kwenye pesa na shetani?

ASANTE KUNIJUZA VIZURI ILA MKUU NINA SWALI KIDOGO KWANINI MUNGU ALIILISEMA KANISA LA SARDI KUWA HAWAKUTIMILIZA MAKUSUDI YAKE AU AWAKUWA WATU AMBAO WANAMPENDEZA MUNGU INGAWAJE WALLIKUWA HAI KIIMANI ILA TATIZO LAO MOJA LILIKUWA NI KUJICHANGAMANA NA DUNIA NAKUFANYA MAMBO YASIYOMPENDEZA MUNGU SASA KWANINI ALIWAONYA HIVYO KWANINI HILI KANISA LILIKUWA LINAJIHUSISHA NA MAMBO HAYO ILIHALI LILIKUWA HAI ? NISAIDIE HAPA KIDOGO AU KAMA KUNA RAFIKI MWINGINE ANISAIDIE HAPA


NIMEQUOTE MAANDIKO HAYA UELEWE NA UNISAIDIE MAANA SIJAELEWA NINAPOSOMA HAPA:

[h=3]UFUNUO WA YOHANA Mlango 3 [/h] 1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.
6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.
12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.




Hata ukisoma ufunuo wa Yohana utapata mambo mengi yanayotokea sasa na yatakayotokea yameandikwa vizuri humo, mm napenda sn kusoma na hii imenisaidia kujua mambo mengi mapya....hata magonjwa mengi mfano Ukimwi na Ebola yote ni man made na lengo ni kufaidi kiuchumi kwa mataifa fulani pamoja na lengo lao kuu la kupunguza idadi ya watu duniani....Illuminati ni wabaya sana
 
Ukiamini uwepo wa Mungu ni lazima uamini na uwepo wa shetani, ukishindwa kuamini moja kati ya hayo imani yako itakuwa na walakini..

Sawa sawa.....huwa nawashangaa watu wakristo kabisa hawaamini kama uchawi upo...seriously? Wakati hata biblia imeliongelea hilo?
 
Nani shetani?wapi yupo?nani amewahi kumuona?kwangu hizi ni hadithi tu kama zile za kudanganya walale.
 
Sasa wewe umesimamia upande upi ?
au sigara kali ?
au unataka kuchosha watu ili uonekane?
kwa nini uamini uwepo wa shetani ushindwa kuamini uwepo wa mungu ??

Angalia vzr
Ume quote watu wawili tofauti
 
Hata ukisoma ufunuo wa Yohana utapata mambo mengi yanayotokea sasa na yatakayotokea yameandikwa vizuri humo, mm napenda sn kusoma na hii imenisaidia kujua mambo mengi mapya....hata magonjwa mengi mfano Ukimwi na Ebola yote ni man made na lengo ni kufaidi kiuchumi kwa mataifa fulani pamoja na lengo lao kuu la kupunguza idadi ya watu duniani....Illuminati ni wabaya sana



Hapa tupo pamoja
 
Sawa sawa.....huwa nawashangaa watu wakristo kabisa hawaamini kama uchawi upo...seriously? Wakati hata biblia imeliongelea hilo?

Huyo atakuwa mkristo jina tu
Coz ht biblia imeandikwa pia kuwa uchawi upo
 
Pesa haina ushetani wala umungu!

Umungu na ushetani uko kwenye akili za watu.

Kabla ya ku-conclude kwamba pesa ni ya shetani au la, jaribu kwanza kutafuta nini maana ya pesa na chanzo chake.
 
Pesa haina ushetani wala umungu!

Umungu na ushetani uko kwenye akili za watu.

Kabla ya ku-conclude kwamba pesa ni ya shetani au la, jaribu kwanza kutafuta nini maana ya pesa na chanzo chake.

watu wanatia huruma...kwao prsa ni kama viumbe fulani hivi!!
 
Wadau natumai mko salama

Dhumuni la uzi huu ni kutaka kujua kama hizi pesa tunazotumia kama zina mahusiano yoyote na mambo ya kishetani mana nimekua nikisikia kuwa alama zilizopo kwenye pesa zinawakilisha ushetani ila sijawahi kupata uthibitisho wowote

Kama kuna mwenye ujuzi na hili atujuze

Ushetani kwa mujibu wa nani..?

Nimeuliza hivyo nikiamini mada yako ipo kiimani tena labda ya Kikristo mno mno Usabato....

Pesa hiyo inatumiwa na Wakristo, wapagani, Muslims , Wasio amini Mungu (Atheist), Buddhist na imani mamia kwa maelfu...

Ukija kwa Atheist yeye haamini Mungu so automatically kwake yeye hakuna shetani.....Wabudda wanaamini shetani wa mtu ni mtu mwenyewe......Sasa kwa mantiki hiyo labda swali lako ulielekeze kwa kundi la imani fulani...

Halafu kwa mtazamo.wako shetani ni nani..?
 
Jaribu ku-google Illuminati utaona Sera na malengo yao na pia alama ya wazi kabisa ya kishetani ipo kwenye note ya $1 ya USA...utaona kuna pyramid yenye ngazi3 ambazo ni za utawala wao...na namna wanavotawala dunia...kumbuka number 13 ni alama ya Illuminati na Freemason na ndio maana kwenye hotel zote kubwa huwezi kukuta chumba number hiyo,

Hoteli kubwa ni zipi wewe...? Zikoje? Zinapatikana wapi..?

Maana hoteli kubwa zinakuwa na hadhi ya Nyota tano....Hapa Arusha kuna Hoteli za Nyota Tano kama Tano hivi na vyote kuna vyumba vya kutosha vyenye namba 13..

Uhusiano wa hoteli na pesa upo wapi hapo..?
 
Sawa sawa.....huwa nawashangaa watu wakristo kabisa hawaamini kama uchawi upo...seriously? Wakati hata biblia imeliongelea hilo?

Hapi ni swala la kuamini....Usipo amini hata ucheze ngoma za kikwenu hakuna uchawi...

Mimi nataka mtu aniloge sasa hivi ndo nithibitishe maana hapo nitakuwa siamini bali najua...
 
Watu washa tofautiana hapa,topic ishaanza kukosa mwelekeo/mlengo.
 
Ukitaka kujua pesa zina ushetan jifungie ndani alafu xiweke kitandan ziwe nyingi alafu utaona kichwa kinavozunguka na plan za ushetan shetan
 
Nadhani unapaswa kuulizwa wewe hili swali ndugu!?

Kabla ya wewe kuandika upuuzi uliandika mwanzo ungetakiwa kutuambia mambo yafuatayo...

Pesa ni nini..?
Mali ni kitu gani. ?
Hakafu shetani ni nani...? (Hapa kwa shetani kuna ambao hawaani Mungu hivyo shetani hawamjui.....umakini unahitajika hapa)

Baada ya kumaliza hayo yote ndio ungetoa hitimisho Pesa ni Mali ya Shetani....

Kama utashindwa kuelezea yote hayo............Naomba nirudie kukuliza

" Nani katoa akili yako?"
 
Back
Top Bottom